Local News

BAN KI MOON ATUMA SALAMU ZA PONGEZI KWA MAGUFULI
Local News

KATIBU Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki Moon ametuma salamu za pongezi kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa dokta John Pombe Magufuli kwa kuchaguliwa kuwa Rais wa Tanzania wa awamu ya Tano.   Katika salamu zake katibu Mkuu huyo amesema kuwa Uchaguzi wa mwaka huu ni uthibitisho wa wazi na dhamira ya muda mrefu ya Watanzania kwa demokrasia, Amani na utulivu.   Mbali na hayo Ban Ki Moon amesema anaamini kuwa, chini ya uongozi wa Rais...

Like
202
0
Wednesday, 11 November 2015
WANAWAKE WALIOCHAGULIWA KATIKA NAFASI ZA UONGOZI WAMETAKIWA KUWAJIBIKA KIKAMILIFU
Local News

MTANDAO wa Jinsia Tanzania-TGNP-pamoja na wanaharakati wa ngazi ya jamii wamewataka wanawake waliochaguliwa kwenye nafasi mbalimbali za uongozi kuwajibika kikamilifu kwa kuitumikia jamii kwani ndiyo iliyowapa ridhaa. Hayo yamesemwa Jijini Dar es salaam jana na mkurugenzi wa-TGNP- Bi. Lilian Liundi wakati akizungumza na waandishi wa habari na kusema kuwa wamekuwa wakifuatilia kwa karibu mchakato wa uchaguzi kuanzia hatua ya awali hadi mwisho lengo ikiwa ni kuangalia ushiriki wa wanawake kwenye uchaguzi. LIUNDI amebainisha kuwa kulingana na...

Like
239
0
Wednesday, 11 November 2015
WAFANYAKAZI MUHIMBILI WAMETAKIWA KUWAHI NA KUFANYA KAZI KWA BIDII
Local News

KAIMU Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH), Profesa Lawrence Mseru ameanza kazi rasmi na kuwataka wafanyakazi wa hospitali hiyo kuwahi kazini kwa wakati na kufanya kazi kwa bidii.   Profesa Mseru ametoa kauli hiyo jana Jijini Dar es salaam baada ya kukutana na menejimenti ya hospitali hiyo ambayo inajumuisha Wakurugenzi 14.   Profesa Mseru ameteuliwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania hivi karibuni kuwa Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa hospitali hiyo baada ya dokta Hussein Kidanto kuhamishiwa wizara ya...

Like
254
0
Wednesday, 11 November 2015
106 WAPOTEZA MAISHA KWA KIPINDUPINDU TANGU AGOSTI 15
Local News

IMEELEZWA kuwa tangu Agosti 15 Mwaka huu jumla ya Wagonjwa 106 wa kipindupindu wameshapoteza maaisha sawa na asilimia 1.3 ya idadi yote ya Wagonjwa 7825 walioripotiwa kuwa na ugonjwa huo.   Akizungumza na wanahabari jijini Dar es salaam Mkurugenzi wa Elimu ya Afya kwa umma kutoka Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii Hellen Semu amesema jumla ya Wagonjwa 53 waliokuwepo katika Manispaa ya Ilala, Temeke na Kinondoni wamepoteza maisha huku bado kukiwa na Wagonjwa katika vituo mbalimbali vinavyotumika kutibu...

Like
409
0
Tuesday, 10 November 2015
TANZANIA KUENDELEA KUSHIRIKIANA NA UMOJA WA NCHI ZA ULAYA
Local News

IKIWA  ni miaka  40  tangu  kuwepo kwa ushirikiano kati ya Serikali ya Jamuhuri ya muungano wa  Tanzania   na jumuiya ya umoja wa nchi  za ulaya, wito umetolewa kwa serikali ya Tanzania kuhakikisha inaendeleza  ushirikiano na jumuiya ya umoja huo.   Rai hiyo imetolewa leo Jijini  Dar es salaamu  na balozi wa jumuiya ya umoja wa nchi za ulaya Filiberto Sebregondi wakati wa uzinduzi wa kitabu chenye kuelezea ushirikiano kwa vitendo  baina ya jumuiya ya  ulaya na nchi za Afrika Mashariki....

Like
224
0
Tuesday, 10 November 2015
NYAMAGANA: WAZEE WAIOMBA SERIKALI KUANGALIA UPYA TARATIBU ZA UTOAJI WA HUDUMA YA AFYA
Local News

BAADHI ya wazee wilayani Nyamagana Mkoani Mwanza wameiomba serikali kuangalia upya utaratibu wa utoaji huduma za Afya katika hospitali ya wilaya hiyo kwani haukidhi mahitaji. Wakizungumza na Efm wazee hao wamesema kuwa tangu utaratibu wa kutolewa huduma bure kwa wazee uanze  suala hilo limekuwa ni kitendawili kwao  kutokana na kutopatiwa huduma hiyo kama inavyoelekezwa. Aidha wamesema kuwa serikali imefanya suala zuri la kuanzisha dirisha maalumu kwa ajili yao lakini utaratibu huo kwa baadhi ya hospitali na zahanati bado haujawa mzuri...

Like
259
0
Tuesday, 10 November 2015
UCHAGUZI MKUU: VYOMBO VYA HABARI VYAPONGEZWA
Local News

VYOMBO vya habari nchini vimepongezwa kwa kazi kubwa waliyoifanya ya kutoa taarifa kwa wananchi hasa wakati wa uchaguzi mkuu uliofanyika oktoba 25 mwaka huu. Pongezi hizo zimetolewa jana na Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Profesa Elisante Ole Gabriel wakati akizungumza na viongozi wa menejimenti ya wizara na taasisi zake kwenye kikao cha kazi kilichofanyika Jijini Dar es Salaam. Profesa Gabriel amesema kuwa kipindi cha uchaguzi vyombo vya habari vimefaya kazi kubwa ya kuwapa habari za...

Like
230
0
Tuesday, 10 November 2015
VYAMA VYA SIASA VIMETAKIWA KUFANYA KAZI KWA KUSHIRIKIANA
Local News

VYAMA vya siasa nchini vimetakiwa kufanya kazi kwa kushirikiana ili kujenga umoja wa kitaifa utakaoleta mshikamano wa kudumu kati ya  viongozi wa vyama hivyo na wafuasi wao.   Wito huo umetolewa na diwani wa kata ya Ilala Saady Khimji kweye hafla fupi ya kuwashukuru wananchi kwa kumpa ridhaa ya kuwaongoza kupitia nafasi hiyo.   Khimji amebainisha kuwa ili kuleta maendeleo katika kata ni vyema kwa kila mwananchi kuhakikisha anatoa ushirikiano wa kutosha kwenye shughuli za...

Like
234
0
Monday, 09 November 2015
CHAMA CHA PTF MASHUJAA CHAPATA USAJILI WA MUDA
Local News

CHAMA cha Tanzania Patriotic Front-TPF-MASHUJAA kimepata usajili wa muda kutoka ofisi ya msajili wa vyama vya siasa wakati kikijiandaa kupata usajili wa kudumu kwa kuzingatia na kutimiza mashari na sheria ya usajili wa vyama vya siasa nchini.   Akizungumza leo Jijini Dar es Salaam baada ya usajili wa chama hicho Msajili wa Vyama vya siasa Jaji Francis Mutungi amewataka viongozi wa chama hicho kutambua kuwa chama ni kwa ajili ya wanachama na si kwa jili ya maslahi ya viongozi wa...

Like
325
0
Monday, 09 November 2015
SIMANJIRO: MADIWANI WATEULE WATAKIWA KUTATUA MIGOGORO YA ARDHI BILA UCHOCHEZI
Local News

MKUU wa Wilaya ya Simanjiro Mkoani Manyara, Mahmoud Kambona amesema atawachukulia hatua kali, baadhi ya madiwani wateule wa wilaya hiyo ambao watasababisha vurugu na kuchochea migogoro kwa wananchi. Kambona ameyasema hayo wakati akizungumza na wananchi wa kijiji cha Loiborsoit A, kata ya Emboreet, ambapo amewataka madiwani hao watatue migogoro ya Ardhi bila kuathiri usalama uliopo kwa watu. Aidha amewataka viongozi hao kutowashawishi wananchi na kusababisha vurugu badala yake watumie hekima na busara kutatua migogoro ya ardhi...

Like
315
0
Monday, 09 November 2015
MAKTABA NCHINI KUJENGEWA UWEZO
Local News

BODI ya huduma za maktaba nchini-TLSB-imeanzisha mradi wa Maktaba kwa maendeleo wenye thamani ya zaidi ya shilingi milioni 630 ili kuzijengea uwezo wa utendaji kazi bora maktaba zote nchini. Akizungumza katika mradi huo Mkurugenzi mkuu wa-TLSB-dokta Ali Mcharazo amesema Mradi huo ambao utatumia zaidi teknolojia ya habari na Mawasiliano-(Tehama)-kwa kutumia maktaba zinazohamishika, utawafikia walengwa moja kwa moja katika maeneo yao ya uzalishaji na kuwawezesha kupata taarifa muhimu za kuendeleza shughuli zao za kila siku. Kwa Upande wao...

Like
228
0
Monday, 09 November 2015