MGOMBEA ubunge Jimbo la Iringa mjini kupitia chama cha mapinduzi-CCM Fredrick Mwakalebela amesema endapo akipata ridhaa ya kuongoza Jimbo hilo atahakikisha anatenga ofisi maalamu kwa ajili ya kusikiliza matatizo ya watu wenye ulemavu. Akizungumza katika kikao na chama cha walemavu mkoa wa Iringa Mwakalebela amesema kuwa atahakikisha kundi hilo maalumu linapewa kipaumbele katika sekta mbalimbali ikiwemo Afya na...
CHUO cha elimu na mafunzo ya ufundi Stadi (VETA) kimekuwa miongoni mwa taasisi kumi bora za Afrika katika utoaji wa mafunzo ya ufundi stadi. Afisa habari wa Chuo hicho, DORA TESHA amekiambia kituo hiki kuwa, tuzo hizo ambazo zimeandaliwa na umoja wa Afrika (AU) kwashirikiana na mashirikia ya USAID na FHI 360 zilizoshirikisha taasisi zaidi ya arobaini kwa lengo la kutambua taasisi bora zinazotoa elimu ya mafunzo ya ufundi stadi katika Afrika. Amesema kuwa sababu ya kuanzishwa mchakato...
KATIKA kuhakikisha jitihada za kuboresha Sekta ya elimu nchini zinaleta mafanikio, asasi ya utafiti ya -TWAWEZA-kupitia mradi wake wa uwezo imeendesha mafunzo ya siku mbili katika wilaya ya mwanga yenye lengo la kuwapa ujuzi wa kufanya kazi za kujitolea vijana wapatao 60 ili waweze kufanya tathmini juu kwa watoto katika nyanja za kuhesabu pamoja na kusoma kiswahili na kingereza. Akizungumza na E-FM Mratibu wa Mradi huo George Madundo amesema mafunzo hayo yatachangia katika shughuli za ukusanyaji wa taarifa za kubaini...
JUMUIYA ya wanafunzi waliosoma shule ya sekondari ya Mtakatifu Joseph kwa wameungana na wanafunzi wa sasa wa shule hiyo kuichangia damu hospitali ya Taifa ya muhimbili ili kuwasaidia watanzania wenye mahitaji ya kuongezewa Damu. Akizungumza na waandishi wa habari mmoja wa wanafunzi wa jumuiya hiyo Mariam Zialo ameeleza kuwa wamefanya zoezi hilo pamoja na wanafunzi wa sasa wa shule hiyo baada ya kuona uhitaji mkubwa wa damu uliokuwepo katika hospitali hiyo. Kwa upande mwingine mkuu wa kitengo cha mawasiliano kutoka...
WAFUGAJI nchini wanatarajia kuondokana na hasara ya vifo vya mifugo yao ikiwemo ng’ombe, baada ya kuzinduliwa dawa mpya ijulikanayo kwa jina la Vectoclor Plus, inayodhibiti magonjwa yanayoenezwa na Kupe. Akizungumza katika uzinduzi huo, Kaimu Mkurugenzi Msaidizi wa Kitengo cha Udhibiti wa wadudu na magonjwa yaenezayo kutoka Wizara ya Maendeleo ya Mifugo na Uvuvi, Dokta Martin Ruheta, amesema uzinduzi huo umekuja wakati muafaka, kwani utapunguza vifo vya mifugo ambapo kila mwaka wanyama wanakufa kwa asilimia 70 kwa sababu ya magonjwa ya...
MWILI wa aliyekuwa Mwenyekiti Mwenza wa vyama vinavyounda Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa) Dokta Emmanueli Makaidi unatarajiwa kuagwa leo katika viwanja vya Karimjee jijini Dar es Salaam. Akizungumza na waandishi wa habari Jijini Dar es Salaam jana mtoto wa marehemu Mhandisi Emmanueli Makaidi amesema mwili huo baada ya kutoka Masasi ulipelekwa Hospitali ya Jeshi Lugalo ambapo jana jioni ilifanyika ibada fupi nyumbani kwa marehemu. Shughuli ya kuuaga mwili wa marehemu itahudhuriwa na viongozi mbalimbali wa kisiasa na...
ILI Kuhakikisha Amani inakuwepo hususani katika kipindi hiki cha Uchaguzi mkuu October 25 watanzania wameshauriwa kufuata sheria zote za uchaguzi kama zilivyoelezwa na tume ya uchaguzi nchini na kuhakikisha kuwa hawafanyi matendo yoyote yatakayopelekea uvunjifu wa Amani. Hayo yamesemwa leo jijini Dar es salaam Katika vikao vya Kamati ya wabunge wa nchi za ukanda wa Maziwa makuu- ICGLR waliopo nchini kwa ajili ya kuangalia mchakato mzima wa uchaguzi unavyoendeshwa. Rais wa kamati hiyo PETER OLE MOSITE ameeleza kuwa...
KUFATIA upotoshawaji wa Taarifa juu ya idadi sahihi ya watu waliojiandikisha katika daftari la kudumu la wapiga kura uliofanywa na baadhi ya vyombo vya habari, Tume ya Taifa ya Uchaguzi Nchini-NEC-imevitaka vyombo hivyo kupata Taarifa sahihi kupitia tume kabla ya kutoa taarifa potofu kwa jamii. Wito huo umetolewa na Mwenyekiti wa Tume hiyo Jaji Damian Lubuva kupitia Taarifa maalum kwa vyombo vya habari ambapo amesema baadhi ya vyombo vya habari ikiwemo gazeti la Mawio, vimetoa taarifa kuwa walioandikishwa katika...
KAMATI ya maudhui ya mamlaka ya mawasiliano Tanzania –TCRA imetoa rai kwa vyombo vya utangazaji nchini kuendelea kutangaza habari zenye kudumisha amani ya watanzania kwa siku hizi chache zilizo baki kuhitimisha zoezi la upigaji kura. Hayo yamebainishwa Jijini Dar es salaam leo na Mwenyekiti wa kamati hiyo Bi MARGARET MUNYANGI wakati akizungumza na waandishi wa habari juu ya mwenendo wa vituo vya utangazaji katika kutangaza habari za kampeni za vyama vya siasa kupitia vituo...
WATANZANIA wametakiwa kuilinda na kuidumisha Amani iliyopo hasa kuelekea kipindi cha Uchaguzi bila kujali itikadi zao za vyama kwani Amani ndiyo msingi wa maendeleo kwa Taifa. Akizungumza na Efm jijini Dar es salaam, mgombea wa nafasi ya Udiwani kata ya Kunduchi kupitia chama cha mapinduzi-CCM-Michael Urio amesema kuwa ili kila mwananchi awe na uhuru wa kufanya kazi ni muhimu Amani kuwepo. Kwa upande wa wafanyabiashara Urio amebainisha kwamba mara baada ya kupewa ridhaa ya kuongoza kata hiyo atahakikisha...
BAADHI ya Taasisi za Serikali ikiwemo hospitali na shule kadhaa za Wilaya ya Babati Mkoani Manyara, zimepatiwa bure huduma ya mtandao wa simu mpya ya kampuni ya Halotel kwa ajili ya kuwarahisishia wapate huduma bora. Akizungumza kwenye sherehe za uzinduzi wa mtandao huo, Meneja wa Halotel Mkoa wa Manyara Adolf Kiwale amesema kuwa wameweka mitandao ya intanenti bure kwa taasisi hizo muhimu ili kurahisisha kazi zao. Amesema licha ya kuzisaidia taasisi hizo wataendelea kutoa misaada kwenye taasisi mbalimbali za kiserikali na...