WAKATI mapigano yakiendelea mashariki mwa Ukraine, viongozi wa nchi za magharibi wamependekeza mipango mipya kujaribu kumaliza mgogoro kati ya Majeshi ya Serikali na waasi wanaoungwa mkono na Urusi. Rais wa Ukraine Petro Poroshenko amesema mapendekezo mapya yaliyotolewa na kiongozi wa Ujerumani Kansela Angela Merkel, na rais wa Ufaransa Bwana Francois Hollande, yameongeza matumaini ya kumaliza mapigano. Mpango huo utawasilishwa kwa Urusi Ijumaa, ambako Urusi imeahidi mazungumzo yenye manufaa. Lakini hatua ya Urusi kuwaunga mkono waasi wa...
WITO umetolewa kwa Uingereza kuongeza nguvu za kupambana na Wanamgambo wa Islamic State, ambapo Wabunge wan chi hiyo wamesema Wanamgambo hao wamejiimarisha sehemu za nchi ya Iraq na Syria . Kamati ya kuteuliwa ya maswala ya Ulinzi ndani ya Bunge hilo imesema Uingereza imeshiriki asilimia 6 tu ya mashambulizi ya anga dhidi ya kundi hilo la Jihad na kusema kuwa wanashangazwa kwa kuwa haifanyi jitihada za hali ya juu. IS imekuwa ikishikilia maeneo mengi na imekuwa ikijihusisha na vitendo vya...
SHIRIKA linalojihusisha na maswala ya usalama na ushirikiano barani Ulaya-OSCE limesema hali ya Mashariki ya Ukraine inazidi kuwa mbaya na mashambulizi dhidi ya Raia yanazidi kuongezeka. Msemaji wa Shirika hilo amesema wanafuatilia hali ilivyo nchini Ukraine na kwamba silaha zilizopigwa marufuku kimataifa zilitumika juma lililopta katika mji unaoshikiliwa na waasi . Baadae hii leo, Mkuu wa Shirika la OSCE atahutubia Baraza lake la kudumu, ambapo anatarajiwa kutoa wito wa kusitisha mapigano kwa muda katika Mji unaodhibitiwa na Serikali wa...
HABARI kutoka Libya zinasema kuwa idadi kadha ya wafanyakazi katika kisima kimoja cha mafuta wameuawa katika shambulio moja Jumanne usiku. Afisa mmoja mwandamizi wa kijeshi amesema kuwa watu kumi na watatu wameuawa katika kisima cha Mabrook. Watano ni raia wa kigeni, watatu wakiwa ni Wafilipino na wawili wanatoka Ghana. Afisa huyo amesema kuwa wote waliouawa walikatwa koromeo, mbali na Mlibya mmoja ambaye alipigwa risasi. Hakuna kundi lililodai kuhusika na shambulio hilo, ingawa taarifa za watu walioshuhudia tukio hilo wanasema watu...
MFALME wa Jordan ameahidi mapambano yasiyo na huruma dhidi ya wapiganaji wa Islamic State kufuatia kuuawa kwa rubani wa nchi hiyo. Baada ya mkutano wa makamanda wa juu wa jeshi na maafisa usalama, Mfalme Abdullah amesema vita hivyo vitaelekezwa dhidi ya kundi hilo na damu ya rubani huyo wa ndege za kivita Muath al-Kasasbeh haitapotea bure. Hapo jana, Jordan iliwanyonga wafungwa wawili wapiganaji wenye msimamo mkali waliokuwa katika orodha ya adhabu ya kifo, kama kulipiza kisasi cha kuuawa kwa rubani...
MAAFISA wa Marekani wamesema vikosi vya jeshi la Marekani vimefanya shambulio nchini Somalia dhidi ya kiongozi mwandamizi wa kundi la al-Shabaab. Shambulio hilo lililofanywa Januari 31 kwa kutumia ndege isiyo na rubani kusini mwa mji mkuu Mogadishu lilimlenga Yusef Dheeq , mkuu wa operesheni za nje na mipango ya upelelezi na usalama wa kundi hilo. Hata hivyo haijathibitishwa iwapo ameuwawa katika operesheni hiyo. Shambulio hilo ni kampeni ...
SERIKALI ya Jordan imewanyonga Wairaq wawili kwa kulipiza kisasi kwa kuuliwa raia mmoja wa nchi hiyo na kundi la Dola la Kiislamu. Hatua hiyo ya kunyongwa imekuja saa chache baada ya kutolewa video inayoonesha rubani wa jeshi la Jordan akichomwa moto akiwa hai. Ripoti za televisheni ya taifa zinasema rubani huyo aliuwawa kiasi mwezi mmoja uliopita. Mchambuzi wa masuala ya mashariki ya kati Randa Habib amesema mauaji hayo ...
NDEGE inayomilikiwa na Shirika la Ndege la Taiwan, la TransAsia imepata ajali na kuangukia kwenye mto katika mji mkuu, Taipei. Vyombo vya habari vya Taiwan vimesema watu zaidi ya 50 walikuwa ndani ya ndege hiyo, wakati ajali ilipotokea na idadi kubwa ya watu wameripotiwa kujeruhiwa. Shirika la Habari la Taiwan limeonesha picha ya ndege hiyo ikiwa imezama kwa kiasi kikubwa katika mto Keelung. Watu kadhaa wameokolewa na kupelekwa hospitali na wengine 10 bado wamenasa katika ndege hiyo. Chanzo cha ajali...
WAZIRI MKUU mpya wa Ugiriki Alexis Tsipras anaendelea na ziara ya mataifa ya Ulaya tangu aingie madaraka wiki moja iliyopita, katika jitihada za kutafuta kuungwa mkono mpango wa kutaka suala la kuiokoa nchi yake na mzigo wa madeni lijadiliwe upya. Anakwenda Italia leo kwa mazungumzo na waziri mkuu Matteo Renzi. Jana waziri mkuu huyo aliondoa uwezekano wa kufanyakazi pamoja na kundi la pande tatu la wakopeshaji wa ...
UMOJA wa Ulaya umesema leo kuwa mahakama nchini Misri imekiuka majukumu yake ya kimataifa kuhusu haki za binadamu kwa kuwahukumu watu 183 adhabu ya kifo jana kwa kuwauwa polisi 13. Idara ya mambo ya kigeni ya Umoja wa Ulaya imesema katika taarifa yake kuwa uamuzi uliotolewa na mahakama ya Misri kuwahukumu washitakiwa 183 adhabu ya kifo kufuatia kesi ya jumla ni ukiukaji wa majukumu ya Misri ya haki za binadamu. Hukumu iliyotolewa ...
LEO ni mwezi mmoja tangu wapiganaji wa Boko Haram waliposhambulia miji ya Baga na Doron Baga kaskazini mashariki mwa Nigeria. Idadi kamili ya watu waliokufa haijulikani lakini inadaiwa kuwa ni kati ya watu mia moja na hamsini hadi elfu mbili. Wakati wapiganaji wa Boko Haram wakivamia kutoka upande wa magharibi wa Baga, kundi la vijana waliodhamiria kupambana na kundi hilo walijaribu kuulinda mji wao. ...