Global News

EBOLA: WAFANYAKAZI 600 WAKUJITOLEA WATASHIRIKI KWENYE AWAMU YA KWANZA YA MAJARIBIO YA CHANJO
Global News

CHANJO ya ugonjwa wa Ebola imeanza kufanyiwa majaribio nchini Liberia, ambapo wafanyakazi 600 wa kujitolea wanatarajiwa kushiriki katika awamu ya kwanza ya majaribio hayo. Chanjo hiyo inayolenga kupunguza kasi ya maambukizi ya virusi vya Ebola, imeanza kutolewa jana kwenye mji mkuu wa Liberia, Monrovia. Ingawa Waliberia wengi wameonyesha wasiwasi, wataalamu wa afya wamesema chanjo hiyo tayari imeonyesha mafanikio na ni salama kwa matumizi ya binaadamu....

Like
259
0
Tuesday, 03 February 2015
JESHI LA NIGERIA LAFANIKIWA KUSAMBARATISHA SHAMBULIO LA PILI LA BOKO HARAM
Global News

JESHI la Nigeria limesema kuwa limefaulu kusambaratisha shambulio la pili la Boko Haram, juma moja tu baada ya kusambaratisha jaribio jingine la mashambulizi katika eneo la kaskazini mashariki mwa Maiduguri. Msemaji wa jeshi hilo Meja Jenerali Chris Olukade, amesema kuwa waliwauwa waasi wengi wa Boko Haram katika shambulio hilo lililotokea mapema Alfajiri leo, huku wakipata bunduki, risasi na magari yaliyokuwa yakitumika na waasi hao wa Boko Haram. Lakini wapiganaji wa vijijini wameliambia Shirika la Utangazaji la BBC kuwa wanakanusha hilo...

Like
248
0
Monday, 02 February 2015
EBOLA: MAJARIBIO MAKUBWA YA CHANJO KUANZA LIBERIA
Global News

HATIMAYE majaribio makubwa ya chanjo ya ugonjwa hatari wa Ebola, yamepangwa kuanza nchini Liberia. Matarajio ni kuwa zaidi ya watu elfu thelathini watajitokeza katika zoezi hilo kubwa la majaribio ya chanjo hiyo iliyotengezwa na kampuni mbili za GSK na Merck. Katika kipindi cha mwaka mmoja uliopita, zaidi ya watu elfu tisa wamefariki katika mlipuko huo mkubwa wa Ebola ambapo Mataifa yaliyoathirika zaidi magharibi mwa Afrika ni pamoja na Guinea, Sierra Leone na...

Like
262
0
Monday, 02 February 2015
JORDAN YAAHIDI KUOKOA MAISHA YA RAIA WAKE ANAESHIKILIWA NA IS
Global News

SERIKALI ya Jordan imesema  imedhamiria kutumia kila njia kuyaokoa maisha ya raia wao anaeshikiliwa na wafuasi wa itikadi kali wa dola ya kiislam IS. Habari hizo zimetangazwa na shirika la habari la Jordan-Petra. Hapo Jana wanamgambo hao wa IS walimuonyesha katika kanda ya video mwandishi wa habari wa Japan Kenji Goto waliyemkata kichwa Serikali ya Japan imesema kanda hiyo ni ya kweli. Hapo awali wafuasi hao wa itikadi kali walionya watawauwa mahabusi wote wawili wa Japan ikiwa serikali mjini Amman...

Like
220
0
Monday, 02 February 2015
BOKO HARAM YAFANYA SHAMBULIZI KASKAZINI MASHARIKI MWA NIGERIA
Global News

shambulio la wanamgambo wa itikadi kali wa Boko Haram katika mji wa kaskazini mashariki ya Nigeria-Maiduguri,limeangamiza maisha ya watu wasiopungua wanane. Mashahidi wanasema Boko Haram wamepambana na vikosi vya serikali vinavyosaidiwa na raia katika mapigano ambayo yalianza saa tisa za alfajiri ya leo. Vikosi vya serikali vinasaidiwa na jeshi la nchi kavu, na lile la wanaanga. Katika siku za hivi karibuni Boko Haram wameeneza hujuma zao hadi katika nchi jirani ya Cameroon....

Like
266
0
Monday, 02 February 2015
KAMPUNI YENYE MAHUSIANO NA CHINA YATUHUMIWA KUWADHILI WANAMGAMBO SUDANI KUSINI
Global News

SHIRIKA la utafiti kuhuhusu silaha ndogondogo, limesema kuwa Kampuni ya mafuta iliyo na mahusiano na China inawafadhili wanamgambo nchini Sudani kusini. Wanamgambo takriban mia saba wanaelezwa kupelekwa katika maeneo ya machimbo ya mafuta yanayomilikiwa na Kampuni hiyo ambayo Shirika la Petroli la Kenya lina hisa kubwa zaidi. Hakukuwa na majibu yoyote kuhusu utafiti uliotolewa na Kampuni ya...

Like
373
0
Friday, 30 January 2015
MKUTANO WA WAKUU WA NCHI ZA UMOJA WA AFRIKA UMEANZA LEO
Global News

MKUTANO wa Wakuu wa Nchi za Umoja wa Afrika umeanza leo nchini Ethiopia ambapo viongozi wa Afrika wanatarajiwa kujadili masuala muhimu yanayolikumba bara la Afrika kwa sasa. Baadhi ya maswala yatakayopewa kipaumbele kwenye mkutano huo ni harakati za kundi la Boko Haram nchini Nigeria, pamoja na juhudi za kupambana dhidi ya ugonjwa hatari wa Ebola. Licha ya kauli mbiu ya mkutano huo wa siku mbili kuwa swala la kuwawezesha wanawake, viongozi kutoka nchi 54 wanachama wa Muungano huo watalazimika kangazia...

Like
244
0
Friday, 30 January 2015
26 WAUAWA MISRI
Global News

MAAFISA wa Jeshi nchini Misri wamesema takriban watu 26 wameuawa katika mfululizo wa mashambulizi yaliyofanywa na kundi la wapiganaji la Islamic State Kaskazini mwa Misri katika eneo la Sinai Wamesema gari lililokuwa na mabomu lilipiga kituo cha kijeshi kaskazini mwa Sinai katika mji wa El-Arish yakilenga hoteli ya jeshi na kuwaua wanajeshi kadhaa. Mashambulizi mengine kama hayo yalifanyika katika mji jirani wa Sheik Zuwayid na mji wa Rafah katika mpaka wa Gaza. Wakati huo huo kundi la wapiganaji la Ansar...

Like
256
0
Friday, 30 January 2015
NIGERIA YATUMIWA UJUMBE KUSIMAMIA UCHAGUZI
Global News

MWENYEKITI wa kamati ya Umoja wa Afrika Bibi Nkosazana Dlamini-Zuma ameidhinisha kutuma ujumbe wa waangalizi wa umoja huo nchini Nigeria ili kusimamia uchaguzi mkuu wa nchi hiyo unaotarajiwa kufanyika mwezi Februari mwaka huu. Taarifa kutoka Umoja wa Afrika zimesema kabla ya waangalizi 50 wa muda mfupi wa Umoja huo kwenda Nigeria, umoja huo utatuma wataalam 15 kuwa waangalizi wa muda mrefu, ambao watakuwepo nchini humo hadi tarehe 11 Machi ili kuangalia vipindi mbalimbali vya mchakato wa...

Like
314
0
Friday, 30 January 2015
MALAYSIA YASITISHA SHUGHULI YA UTAFUTAJI WA NDEGE YA MH370
Global News

SERIKALI ya Malaysia imesitisha shughuli ya kuitafuta ndege ya iliyopotea ya MH370 na kuitaja kama ajali huku ikisema hapakuwa na manusura wa ajali hiyo. Maafisa wakuu wanasema shughuli ya kuipata ndege hiyo, bado inaendelea lakini inasemekana abiria 239 waliokuwa kwenye ndege hiyo walifariki. Ndege hiyo bado haijulikani iliko na wala kujulikana ilikopotelea licha ya shughuli kubwa ya kimataifa kuitafuta kusini mwa bahari ya hindi. Tangazo la serikali ya Malaysia, lililotolewa leo, linatoa fursa kwa jamaa wa waathiriwa wa ajali hiyo...

Like
280
0
Thursday, 29 January 2015
RAIS KIIR AKIMBIZWA HOSPITALINI ETHIOPIA
Global News

MKUTANO wa viongozi wa kikanda ulioandaliwa kujadili mgogoro wa mwaka mmoja ulioko nchini Sudan Kusini, umecheleweshwa baada ya Rais Salva Kiir kuugua na kukimbizwa hospitalini mjini Addis Ababa, Ethiopia. Afisa mmoja wa shirika la IGAD, ambalo linafanya juhudi za kuwakutanisha viongozi wa Sudan Kusini kwa lengo la kumaliza vita, ameliambia shirika la Utangazaji la BBC, kwamba Rais Kiir, alianza kuvuja damu kutoka puani. Kabla ya kuugua, hapo jana Rais Kiir alifanya mazungumzo na kiongozi wa waasi Riek Machar ambapo alimtaka...

Like
269
0
Thursday, 29 January 2015