Global News

AL SHABAAB WASHAMBULIA ASKARI KENYA
Global News

ASKARI MMOJA ameuawa na mwingine yupo mahututi baada ya kushambuliwa kwa kupigwa risasi Kaskazini mwa Kenya. Askari hao wanadaiwa kushambuliwa na watu wanaosadikiwa kuwa ni wafuasi wa kundi la Al Shabaab. Askari hao wa jeshi la Polisi kikosi cha ziada wamekutwa na kisa hicho mjini Wajir Kaskazini mwa Kenya usiku wa kuamkia leo.  ...

Like
337
0
Tuesday, 23 December 2014
ESSEBSI AJITANGAZIA USHINDI TUNISIA
Global News

MGOMBEA WA URAIS nchini Tunisia, anayepinga Itikadi Kali za Kiislamu, BEJI CAID ESSEBSI, amejitangazia ushindi mkubwa katika uchaguzi wa kwanza huru. Hata hivyo, mpinzani wake, Rais aliyeko madarakani, MONCEF MARZOUKI, amepuuza madai hayo akisema hayana msingi na amekataa kukubali kuwa ameshindwa. Wananchi wa Tunisia wamepiga kura katika awamu ya Pili, huku wengi wao wakiuita uchaguzi huo kama uchaguzi wa Kihistoria wa Demokrasia katika nchi hiyo ambapo vuguvugu la mageuzi katika nchi za Kiarabu limeanzishwa....

Like
286
0
Monday, 22 December 2014
MAREKANI YATAFAKARI KUITANGAZA KOREA KASKAZINI KAMA TAIFA LINALOFADHILI UGAIDI
Global News

Rais wa Marekani BARACK OBAMA amesema Serikali yake inatafakari kuiorodhesha upya Korea Kaskazini kama taifa linalofadhili ugaidi. Hatua imekuja kufuatia uingiliaji wa Mtandao wa Kampuni ya Filamu ya Sony, hatua iliyoilaazimu kufuta uzinduzi wa filamu yake inayoonyesha mauaji ya kutungwa ya kiongozi ya Korea Kaskazini KIM JONG UN. Maafisa mjini Pyongyang wamekanusha kufanya mashambulizi hilo la...

Like
303
0
Monday, 22 December 2014
RAIS KENYATTA AIDHINISHA SHERIA MPYA YA USALAMA
Global News

RAIS wa Kenya Uhuru Kenyatta, ameidhinisha sheria mpya ya usalama ambayo inawezesha majasusi kunasa mawasiliano kisiri au kufanya udukuzi pamoja na kuwazuia washukiwa wa ugaidi kwa mwaka mmoja kabla ya kuwafungulia mashitaka. Kenyatta amesema kuwa sheria hiyo mpya inahitajika kwa ajili ya kukabiliana na tisho la ugaidi kutoka kwa kundi la wapiganaji wa kiisilamu la Al Shabaab. Amesisitiza kuwa sheria hiyo haikiuki haki za binadamu wala kuwapokonya watu uhuru wa kujieleza. Hapo jana, wabunge wa serikali na wa upinzani walipigana...

Like
270
0
Friday, 19 December 2014
WAPIGANAJI WA KIKURDI WAPELEKA KIKOSI IRAQ KUPAMBANA NA IS
Global News

WAPIGANAJI wa Kikurdi wamesema wamepeleka kikosi Kaskazini mwa Iraq ili kupambana na wapiganaji wa kundi la Islamic State-IS. Kikosi cha Wakurd elfu nane 8, kimeanzisha Mashambulizi endelevu kuvunja zuio katika Mlima Sinjar ili kuwakomboa maelfu ya watu ambao wamezuiwa huko na Kundi la Islamic State. Operesheni hiyo imeanza Jumatano wiki hii kwa ushirikiano na vikosi vya Marekani na wafuasi wanaounga mkono harakati hizo....

Like
251
0
Friday, 19 December 2014
VIONGOZI WA ULAYA WAUNGANA KUIKABILI URUSI
Global News

VIONGOZI wa Ulaya wamemaliza kikao chao mjini Brussels Ubelgiji, wakisema kwa sasa wameungana zaidi kuliko ilivyokuwa katika kuikabili Urusi. Viongozi hao wameonyesha kuwa vikwazo vya kiuchumi havitadhoofishwa licha ya matatizo ya kifedha yanayoikabili Urusi. Rais mpya wa Baraza la Ulaya, DONALD TUSK akifunga kikao cha viongozi wa EU amesema Urusi na vitendo vyake ni tatizo kubwa la kimkakati linaloikabili Ulaya....

Like
274
0
Friday, 19 December 2014
NIGERIA: ASKARI 54 WAHUKUMIWA KIFO KWA KUKATAA KUPAMABANA NA BOKO HARAM
Global News

MAHAKAMA moja ya kijeshi nchini Nigeria imewahukumu kifo askari 54 kwa kukataa kupigana na kundi la wapiganaji wa Kiislamu la Boko Haram.   Wanajeshi hao ambao walipatikana na kosa la uasi,walituhumiwa kukataa kuikomboa miji mitatu iliyokuwa imetekwa na Boko Haram mwezi Agosti.   Wakili wa wanajeshi hao 54 amesema kuwa watawauwa kwa kupigwa risasi huku wengine watano wakiachiliwa huru.   Hata hivyo Wanajeshi hao wamelalamika kuwa hawapewi silaha na mabomu ya kutosha kupigana na kundi hilo la Boko Harm.  ...

Like
342
0
Thursday, 18 December 2014
WABUNGE WA KENYA WARUSHIANA NGUMI BUNGENI NA KUCHANIANA NGUO
Global News

WABUNGE Nchini Kenya wametofautiana vikali bungeni na kuvuana mashati huku wakirushiana ngumi kufuatia mjadala kuhusu mswaada tatanishi wa usalama ambao wabunge wa upinzani wanasema unakiuka uhuru wa Wakenya.   Bunge limelazimika kuahirisha vikao vyake kwa dakika 30 badala ya kujadili mswada tatanishi kuhusu usalama wa nchi. Kikao cha leo kilikuwa kikao maalum ambacho kilipaswa kupitisha mswada huo ambao baadaye utaidhinishwa na Rais kuwa sheria.   Mwenyekiti wa kamati ya usalama wa bunge, Bwana Asman Kamama, alijaribu kufaya...

Like
364
0
Thursday, 18 December 2014
MAREKANI NA CUBA KUREJESHA MAHUSIANO YA KIDIPLOMASIA
Global News

BAADA ya nusu karne ya siasa za Vita Baridi, hatimaye Marekani na Cuba zimetangaza nia ya kurejesha mahusiano ya kidiplomasia. Hatua hiyo inayochukuliwa kama tukio la kihistoria baina ya mahasimu hao, ilitangazwa jana na Rais Barack Obama wa Marekani, ambaye sasa nchi yake itaacha mtazamo wa kikale ambao kwa miongo kadhaa umeshindwa kuendeleza maslahi ya taifa. Mjini Havana, Rais Raul Castro wa Cuba naye amelihutubia taifa akisema mataifa hayo mawili yamekubaliana kurejesha mahusiano, hata kama bado tatizo kuu lingalipo. Tangazo...

Like
273
0
Thursday, 18 December 2014
TUNISIA KUINGIA AWAMU YA PILI YA UCHAGUZI
Global News

AWAMU ya pili ya Uchaguzi wa rais nchini Tunisia inatarajia kufanyika siku ya Jumapili. Taarifa zaidi zimeeleza kuwa Rais aliyeko madarakani, MONCEF MARZOUKI atapambana na mkongwe wa siasa, BEJI CAID ESSEBSI. Kwa mara ya kwanza Watunisia wataruhusiwa kumchagua Rais wao kwa uwazi tangu nchi hiyo ilipopata Uhuru wake kutoka kwa Ufaransa, mwaka 1956. Awamu ya kwanza ya uchaguzi wa Rais imefanyika Novemba 23, na Bwana ESSEBSI, mwenye umri wa miaka 88, amepata asilimia 39 ya kura, kiwango ambacho hakikutosha kumpa...

Like
374
0
Thursday, 18 December 2014
UGANDA YATENGA BILIONI 20 KUONGEZA MIFUGO
Global News

SERIKALI ya uganda imetenga shilingi bilioni 20 kwa ajili ya kuongeza mifugo kwenye eneo la Nile Magharibi katika mwaka wa fedha wa 2014 na 2015. Kwa mujibu wa Kamishna Ofisi ya waziri mkuu anaesimamia mipango ya mifugo Kaskazini mwa Uganda Gonzaga Mayanja, amesema asilimia 97% za fedha hizo zitatumika kwa ajili ya ununuzi wa mifugo na nyingine kwa gharama za uendeshaji . Mayanja amebainisha kuwa watoa huduma hizo tayari wamekwisha kusaini mikataba na ifikapo Januari mwakani ugawaji wa mifugo katika...

Like
627
0
Wednesday, 17 December 2014