MFANYAKAZI za Ndani wa Uganda ambaye alinaswa kwenye kanda ya video akimchapa na kumkanyaga mtoto mdogo amepatikana na hatia ya ukatili na hivyo atafikishwa Mahakamani siku ya Jumatatu Disemba 15 mwaka huu. Jolly Tumuhirwe ameiambia Mahakama kuwa alilazimika kufanya kitendo chake kwa sababu mamake mtoto huyo aliwahi kumchapa mara kadhaa. Hata hivyo waandishi wa habari wamezungumza na mama wa mtoto aliyefanyiwa ukatili huo ambaye amekanusha madai ya Jolly akisema hajawahi kumgusa Jolly hata wakati mmoja huku akihoji madai ya Jolly...
MABOMU mawili yameripuka katika mji wa Jos nchini Nigeria, hilo likiwa ni shambulizi la pili kuukumba mji huo na kuwaua watu 40 huku wengine wakijeruhiwa. Taarifa zimeeleza kuwa hakuna kundi ambalo limekiri kuhusika na mashambulizi hayo lakini inashukiwa ni waasi wa kundi la Boko Haram wamefanya mashambulizi hayo. Mnamo mwezi Mei mwaka huu Boko Haram iliushambulia mji huo wa Jos ulioko kati mwa Nigeria na kuwaua watu 118. ...
MKURUGENZI wa Shirika la Ujasusi la Marekani CIA, JOHN BRENNAN, kwa mara nyingine ametetea matumizi ya mbinu za kikatili wakati wa kuwahoji watuhumiwa wa ugaidi baada ya shambulio la Septemba 11 nchini Marekani. BRENNAN amekiri kuwa baadhi ya mbinu zilizotumika zilikuwa za kuchukiza. Lakini amesisitiza kuwa baadhi ya wafungwa ambao walipitia mbinu hizo, ambazo zilikuwa ni pamoja na kuwazamisha kwenye maji, kuwafadhaisha na kuwanyima usingizi zimesaidia kuokoa maisha ya Wamarekani na zilisaidia kumpata OSAMA BIN LADEN. Amejibu ripoti ya Kamati...
SHIRIKA la afya la Kimataifa WHO, limesema idadi ya waliokufa kutokana na maradhi ya Ebola imeongezeka na kufikia watu 5689. Jumla ya watu 16, 000 wameripotiwa kuugua ugonjwa huo katika nchi nne-shirika hilo la Umoja wa mataifa linasema. Mataifa matatu ya Afrika Magharibi, Guinea, Sierra Leone na Liberia ndio yaliyoathirika zaidi na maradhi hayo. Katika hatua nyingine Watafiti wa chanjo ya Ebola nchini Marekani wamesema kuwa wametiwa moyo na matokeo ya awamu ya kwanza ya majaribio ya chanjo ya ugonjwa...
MISIKITI minne iliofungwa na maafisa wa polisi wiki iliopita baada ya kuchukuliwa na vijana wenye itikadi kali za kiislamu hatimaye imefunguliwa. Hatua ya kuifungua misikiti hiyo ya Minaa, Sakina, Musa na Swafaa inajiri baada ya siku mbili za mazungumzo kati ya viongozi wakuu wa kiislamu, wataalam na uongozi wa kaunti ya Mombasa. Maelezo ya mazungumzo hayo yalioandaliwa na Gavana wa Mombasa Hassan Joho na kaunti kamishna Nelson Marwa yamefanywa kuwa siri. Kabla ya misikiti hiyo kufunguliwa ,viongozi wa kiislamu pamoja...
RAIS wa Ufaransa Francois Hollande anatarajia kuanza ziara yake nchini Guinea kesho, itakayomfanya kuwa kiongozi wa kwanza wa magharibi kuitembelea nchi iliyoathirika kwa kiasi kikubwa na ugonjwa hatari wa Ebola. Guinea tayari imewapoteza watu 1,200 kutokana na ugonjwa huo, ambao kufikia sasa umewaua zaidi ya watu 5,600 na kuwaambukiza wengine 16,000 hasa katika eneo la Afrika Magharibi, kwa mujibu wa Shirika la Afya ulimwenguni – WHO. Katika hatua nyingine Watafiti wa chanjo ya Ebola nchini Marekani wamesema kuwa wametiwa...
KIONGOZI wa Kanisa Katoliki Papa Francis amelitaka bara la Ulaya kutayarisha sera moja na ya haki katika suala la uhamiaji. Amesema mamia kwa maelfu ya wahamiaji wanaowasili katika mataifa hayo kila mwaka kupitia baharini wanahitaji kukubalika na msaada, na sio kuwa na sera zenye maslahi binafsi ambazo zinahatarisha maisha na kuchochea mzozo wa kijamii. Papa Francis ametoa kauli hiyo katika bunge la Ulaya wakati wa ziara fupi iliyokuwa na lengo ...
WATU 78 wameuawa katika mashambulio mawili ya kujitoa mhanga yaliyofanywa sokoni, katika mji wa Maiduguri kaskazini mwa Nigeria. Watu walioshuhudia tukio hilo wamesema mlipuko wa kwanza ulitokea wakati washambuliaji hao walipomuwekea mlipuko mwanamke mmoja mwenye matatizo ya akili. Kundi la kiislamu la wapiganaji la Boko Haram ambalo linadhibiti maeneo mengine ya miji ya kaskazini mwa nchi hiyo na vijiji, linadhaniwa kuhusika na shambulio...
WATU KUMI wamepoteza maisha baada ya jengo la ghorofa kuanguka mjini Cairo nchini Misri, maafisa wameeleza kuwa Watu saba wamejeruhiwa pia baada ya jengo la ghorofa nane kuanguka usiku. Mkuu wa Idara ya dharula Jenerali Mamdouh Abdul Qader amesema vikosi vya uokoaji vinawasaka Watu 15 wanaokisiwa kunasa kwenye kifusi. Mara kadhaa majengo yameanguka nchini humo, sababu kubwa ikiwa ni ujenzi usiofuata kanuni na Sheria pia usimamizi mbovu wa taratibu za ujenzi. Wakazi wa majengo ya karibu na lilipoanguka jengo...
WAZIRI wa Fedha wa Urusi, ANTON SILUANOV, amesema Urusi imepoteza Dola Bilioni 40 kwa mwaka kutokana na vikwazo ilivyowekewa na nchi za Magharibi kwa madai ya kuhusika katika mzozo wa Ukraine. Hata hivyo, Rais VLADIMIR PUTIN amesema hasara hiyo sio madhara makubwa kwa Uchumi wa taifa lake. SILUANOV ambaye alikuwa akitoa hotuba katika Kongamano la Kiuchumi mjini Moscow amebainisha kuwa wamepata hasara ya Mabilioni ya fedha kutokana na vikwazo vinavyohusishwa na siasa za Urusi kuelekea eneo hilo na kuongeza kuwa...
GHASIA zimezuka nchini Marekani, baada ya Wanasheria kuamua kutomfungulia Mashtaka Polisi wa Kizungu aliyeua Kijana Mweusi. Taarifa zaidi zimeeleza kuwa Vitu mbalimbali vimechomwa moto, baada ya jopo la Wanasheria nchini humo kuamua kutomfungulia Mashtaka polisi DAREN WILSON, ambaye amemuua kwa kumpiga risasi kijana Mweusi MICHAEL BROWN. Tukio hilo lilitokea katika mji wa Ferguson mwezi Agusti mwaka huu. Kwa upande wake Rais wa Marekani BARACK OBAMA ametaka kuwepo kwa amani, licha ya kueleweka kwamba baadhi ya raia wa nchi hiyo watakuwa...