Global News

OBAMA KUHUTUBIA TAIFA LEO
Global News

Ikulu ya Marekani imesema Rais BARRACK OBAMA atatumia muda ambao watazamaji wa Televisheni nchini humo wanaangalia zaidi matangazo siku ya Alhamisi kutangaza mabadiliko makubwa ya mfumo wa uhamiaji wa nchi hiyo. Inatarajiwa kuwa Rais OBAMA atasema kuwa atatumia madaraka yake aliyopewa Kikatiba kuzuia wahamiaji wapatao Milioni Tano kurejeshwa makwao na badala yake wapatiwe vibali vya kufanya kazi nchini humo. Rais OBAMA amesema hayo katika video iliyotumwa katika ukurasa wa Facebook kabla ya hotuba yake. Tangu kuingia Madarakani OBAMA amekuwa...

Like
347
0
Thursday, 20 November 2014
EBOLA: MFUKO WA BILL NA MELINDA GATES UMEAHIDI KUTOA DOLA MILONI 5.7
Global News

MFUKO wa Bill na Melinda Gates umeahidi kutoa kiasi cha dola milioni 5.7 kwa ajili ya mradi kusaidia matibabu dhidi ya maradhi ya Ebola nchini Guinea na nchi nyingine zilizoathiriwa na ugonjwa huo. Mfuko huo pia umesema msaada huo utasaidia kutathimini dawa za majaribio. Zaidi ya Watu 5,000 wamepoteza maisha kutokana na Ebola, karibu wote kutoka Afrika Magharibi. Hata hivyo kuna chanjo kadhaa za majaribio na dawa za kutibu maradhi ya Ebola, lakini hazijajaribiwa kwa ajili ya kuona usalama wake...

Like
335
0
Wednesday, 19 November 2014
UN: KOREA KASKAZINI INASTAHILI KUFIKISHWA KWENYE MAHAKAMA YA KIMATAIFA YA UHALIFU
Global News

BARAZA la Umoja wa Mataifa la haki za binadamu limesema Korea Kaskazini inastahili kufikishwa katika mahakama ya kimataifa ya uhalifu kutokana na kukiuka haki za binadamu. Katika baraza hilo zimetolewa tuhuma dhidi ya Korea Kaskazini kwamba serikali yake imekuwa ikifanya vitendo vya ukiukaji haki za binadamu. Mapendekezo hayo yaliyopitishwa na baraza la haki za binadamu la kimataifa yanapaswa kupigiwa kura ili kupitishwa na bunge yaweze kuhalalishwa. Ripoti ya mwezi Februari mwaka huu iliyotolewa na umoja wa mataifa ilibainisha kuwa watu...

Like
288
0
Wednesday, 19 November 2014
MAREKANI YAIPONGEZA BURKINA FASO
Global News

SERIKALI ya Marekani imewapongeza wananchi wa Burkina Faso na viongozi wao kwa kutia saini mkataba utakao ongoza serikali ya mpito kuelekea serikali iliyochaguliwa kidemokrasia. Aidha Marekani imesema inampongeza Michel Kafando kwa kuapishwa kuwa rais wa mpito wa Burkina Faso na kuendeleza kasi iliyoanza wiki mbili zilizopita na kuwachagua watu watakaosaidia kuendesha serikali ya mpito ambao wamejitolea kujenga serikali ya kiraia na kidemokrasia. Hata hivyo imeyataka majeshi ya Burkina Faso kuendelea na jukumu lao la msingi la kulinda mipaka...

Like
352
0
Wednesday, 19 November 2014
SHAMBULIO LAUA WANNE NA NANE KUJERUHIWA ISRAEL
Global News

TAKRIBAN waisreli wanne wameuawa na wengine 8 kujeruhiwa katika kile polisi wanasema ni shambulio la kigaidi dhidi ya Sinagogi eneo la magharibi ya Jerusalem. Kwa mujibu wa Polisi wanaume waliojihami kwa visu na mapanga wanaoshukiwa kuwa Wapalestina ndio waliofanya mashambulizi hayo. Israel imekuwa katika hali ya tahadhari kuu baada ya mashambulio kadhaa na Wapalestina wakizozana na Waisraeli kuhusiana na eneo takatifu ambalo wamekuwa wakizozania kwa muda mrefu....

Like
315
0
Tuesday, 18 November 2014
WANNE WAUAWA KWA VISU KENYA
Global News

WATU wanne wameuawa kwa kuchomwa visu na vijana waliokuwa wamejihami mjini Mombasa Pwani ya Kenya. Watu kadhaa pia wamejeruhiwa katika shambulio hilo la usiku wa kuamkia leo kwenye vituo vya basi Kisauni. Bado haijajulikana waliouawa lakini inaaminika walikuwa raia wa kawaida waliokuwa kwenye shughuli zao. Aidha inadaiwa vijana hao walikuwa wameziba nyuso zao, wakipeperusha bendera nyeusi sawa na ile iliyopatikana katika msako wa jana kwenye misikiti ya Musa na Sakinah, jijini Mombasa....

Like
291
0
Tuesday, 18 November 2014
AFRIKA MAGHARIBI KUPATA MSAADA WA EURO MILIONI 12
Global News

UMOJA wa Ulaya umeahidi kutoa euro milioni 12 kama msaada kwa mataifa yanayopakana na nchi zilizoathiriwa na ugonjwa hatari wa Ebola Afrika Magharibi. Mali, Senegal na Ivory Coast zitanufaika na fedha hizo kuzisadia kujiandaa kukabiliana na kitisho cha mlipuko wa Ebola kupitia kampeni ya kuuhamasisha umma na kutambua mapema maambukizi. Msaada huo mpya umetangazwa na mratibu wa juhudi za kudhibiti Ebola wa Umoja wa Ulaya Christos Stylianides kufuatia ziara yake mwezi huu katika nchi zilizoathirika sana na Ebola, Sierra Leone,...

Like
335
0
Tuesday, 18 November 2014
HRW: POLISI CONGO WAFANYA MAUAJI
Global News

SHIRIKA la kutetea haki za binadamu la Human Rights Watch limesema polisi katika mji mkuu wa Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo, Kinshasa, walifanya mauaji kadhaa katika operesheni iliyodumu miezi mitatu dhidi ya makundi ya kihalifu. Shirika hilo limesema operesheni hiyo iliyopewa jina Likofi iliyozinduliwa Novemba mwaka uliopita ililenga kukomesha ongezeko la wizi wa kutumia silaha na uhalifu mwingine unaofanywa na makundi madogo yanayojulikana kama kuluna. Katika ripoti iliyotolewa leo shirika la Human Rights Watch linasema polisi walioshiriki...

Like
444
0
Tuesday, 18 November 2014
BURKINA FASO: WAZIRI WA MAMBO YA NJE ATAJWA KUWA RAIS WA MPITO
Global News

ALIYEKUWA Waziri wa mambo ya nje wa Burkina Faso Michel Kafando, ametajwa kuwa rais wa mpito nchini humo. Jitihada zimekuwa zikiendelea nchini humo kumchagua kiongozi wa mpito kufuatia kuidhinishwa hapo jana na jeshi na viongozi wa mashirika ya kiraia kwa mpango wa mwaka mzima utakaohakikisha kufanyika uchaguzi. Kafando alikuwa mmoja kati ya watu wanne ambao wangechukua wadhifa huo, wakiwemo waandishi wawili na msomi mmoja. Michel Kafando, Sasa anatakiwa amchague waziri mkuu ambaye anaweza kuwa raia au afisa wa jeshi kuongoza...

Like
324
0
Monday, 17 November 2014
POLISI KENYA YAKAMATA MABOMU KWENYE MISIKITI INAYODAIWA KUTOA MAFUNZO YA ITIKADI KALI
Global News

  POLISI nchini Kenya wanasema kuwa wamenasa mabomu ya kurusha na silaha mbalimbali usiku wa kuamkia leo katika msako mkali walioanza kufanya dhidi ya misikiti inayodaiwa kutoa mafunzo ya itikadi kali za kidini mjini Mombasa Pwani ya Kenya. Mtu mmoja ameuawa na wengine zaidi ya 250 kukamatwa katika msako huo unaolenga misikiti inayosemekana kutoa mafunzo kuhusiana na harakati za wapiganaji wa kiisilamu wa Al Shabaab nchini Somalia. Polisi wanadai kuwa misikiti hiyo ikiwemo Masjid Musa inatumika kwa kuwasajili vijana wanaojiunga...

Like
354
0
Monday, 17 November 2014
MAFUA YA NDEGE TENA UINGEREZA
Global News

MLIPUKO wa Mafua ya Ndege umethibitishwa katika Shamba moja la kuzalishia Bata Mashariki mwa Yorkshire, nchini Uingereza, wamesema maafisa. Wizara ya Mazingira, Chakula na Masuala ya Vijijini -DEFRA imesema kuwa Mafua ya Ndege hatari yake ni ndogo sana kwa Afya ya umma. Taarifa zaidi zimebainisha kuwa Ndege wasiohitajika wanatakiwa kuondolewa kutoka eneo hilo na kuwaweka sehemu maalum ambayo itakuwa imeandaliwa. Tatizo hilo bado halijathibitishwa, lakini aina ya Kirusi cha H5N1 hakijaweza kubainishwa na maafisa wa...

Like
271
0
Monday, 17 November 2014