Global News

Rais Magufuli Atoa Agizo  kwa wanaodaiwa na JWTZ
Global News

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt John Pombe Magufuli leo Alhamisi Mei 17, 2018 amefungua kituo cha Uwekezaji cha Suma JKT kilichopo Mgulani. Hafla hiyo imehudhuriwa na viongozi mbalimbali wa serikali pamoja na vyombo vya ulinzi na usalama wakiwemo mawaziri, pamoja na maafisa mbalimbali wa majeshi ya ulinzi na usalama hapa nchini. Katika hafla hiyo, Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi na Usalama, Jenerali Venance Mabeyo ameeleza kuwa JWTZ linazidai sekta binafsi kiasi cha shilingi bilioni 40, huku taasisi...

Like
684
0
Thursday, 17 May 2018
RAIS TRUMP AWATUMIA SALAAM ZA MWEZI MTUKUFU WAISLAM WASHIO MAREKANI
Global News

Rais wa Marekani, Donald Trump ametuma ujumbe kwa Waislamu wote nchini Marekani na kwingineko duniani kwa kuadhimisha kuanza kwa mwezi mtukufu wa Ramadhan. Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na White House, wakati ambapo watu wengi wanaungana pamoja kusherehekea mwezi mtukufu wa Ramadhan, Rais Trump na mkewe Melania wana matumaini kuwa mwezi huu utakuwa wa baraka. Taarifa imesema kuwa Marekani imebarikiwa kuishi kwa mujibu wa katiba ambayo inaheshimu uhuru wa dini na inaheshimu uhuru wa kuabudu wa kila mwananchi. Katiba yetu...

Like
535
0
Thursday, 17 May 2018
Burundi wanapiga kura ya maoni leo kutoa maamuzi ya muda wa muhula wa Rais kukaa madarakani kutoka miaka tano hadi saba
Global News

Burundi inafanya kura ya maamuzi hapo inayopania kuongeza muhula wa rais kutoka miaka tano hadi saba. Marekebisho hayo ya katiba yakiidhinishwa na wananchi huenda rais Pierre Nkurunziza akaongoza taifa hilo hadi mwaka wa 2034. Lakini kampeni hizo zimechafuliwa na tishio za upinzani kususia kura hiyo ya maamuzi huo na pia madai kwamba serikali imekuwa ikiwatisha wafuasi wa upinzani. Umoja wa mataifa unahofia huenda ghasia zikazuka baada ya mauaji ya watu 26 hivi majuzi. Wiki jana, washambuliaji ambao serikali imewataja kuwa...

Like
475
0
Thursday, 17 May 2018
Ukidanganya Kwenye Mtandao Kenya Adhabu dola 50,000 za Kimarekani
Global News

Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta ameidhinisha Mswada wa Sheria za Uhalifu wa Kompyuta na Mtandaoni wa 2018 kuwa Sheria, hatua itakayotoa adhabu kali kwa watakaopatikana na makossa ya mtandaoni. Sheria hiyo inatoa adhabu ya faini ya dola 50,000 za Marekani au kifungo cha miaka miwili jela, au adhabu zote mbili, kwa atakayepatikana na kosa la uenezaji wa habari za uzushi. Mtu atakayepatikana na kosa la kueneza taarifa ambazo zinaweza kuzua taharuki au kuzua vurugu atafungwa jela zaidi ya miaka kumi....

Like
746
0
Wednesday, 16 May 2018
Kim Jong-un atishia kufuta mkutano wake na Trump
Global News

Korea Kaskazini imesema huenda ikaufuta mkutano kati ya kiongozi wake Kim Jong-un na Rais wa Marekani Donald Trump iwapo Marekani itaendelea kusisitiza kwamba taifa hilo la bara Asia ni lazima liharibu au kusalimisha silaha zake za nyuklia. Mkutano huo ambao umesubiriwa kwa hamu kati ya Bw Trump na Bw Kim unatarajiwa kufanyika mnamo 12 Juni. Hayo yamejiri baada ya Korea Kaskazini kusema imejitolea kuhakikisha silaha za nyuklia zinaondolewa katika rasi ya Korea. Maandalizi ya mkutano huo wa Trump-Kim yamekuwa yakiendeleza,...

Like
460
0
Wednesday, 16 May 2018
JINSI RAIS MAGUFULI ALIVYOFANYA ZIARA YA GHAFLA BANDARINI DAR ES SALAAM KUKAGUA MATANKI YA MAFUTA YA KULA
Global News

  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akiwasili eneo lenye matanki ya kuhifadhia mafuta ya kula baada ya kushushwa melini alipofanya safari ya ghafla kukagua uingizwaji na ugawaji wa ulipiaji wa ushuru  bidhaa hiyo kwenye bandari ya Dar es salaam leo Mei 15, 2018  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akitoa maelekezo na kuulia maswali alipowasili eneo lenye matanki ya kuhifadhia mafuta ya kula baada ya kushushwa melini alipofanya safari ya...

Like
960
0
Tuesday, 15 May 2018
WAMAMA KENYA WAANDAMANA KISA MMAMA MMOJA KUFUKUZWA KAZI KWA KOSA LA KUNYONYESHA MTOTO WAKE
Global News

Nchini Kenya Wamama wameandamana leo mjini Nairobi kulalamika tuhuma za mwanamke mwenzao kufukuzwa eneo lake la kazi (Mgahawani) kwa sababu alinyonyesha mtoto wake akiwa kazini, jambo ambalo liliinua hasira kwa wakina mama wengi nchini humo na kufikia hatua ya kuanza kuingia barabarani wakielekea katika mgahawa huo, ambako mama huyo anatuhumu kuwa aliambiwa ajifunike wakati anamnyonyesha mtoto wake mwenye umri wa mwaka mmoja. Mama huyo alieleza kwamba yeye alipokuwa ananyonyesha mtoto wake aliambiwa akanyonyeshee chooni, jambo lililomfanya...

Like
597
0
Tuesday, 15 May 2018
Melania Trump afanyiwa upasuaji wa figo
Global News

Mama wa Taifa nchini Marekani Melania Trump amefanyiwa upasuaji wa figo. Ofisi yake ilisema kuwa madaktari walifanya upasuaji huo kwenye hospitali ya Walter Reed National Military Medical Center. Upasuji huo ulikuwa wenye mafaninikio na hakukuwa na matatizo yoyote kwa mujibu wa msemaji wake. Bi Trump, 48, anatarajiwa kutumia muda mwingi wiki hii kupata nafuu hospitalini huko Bethesda, Maryland. Alisema kampeni hiyo ina lengo la kuhakikisha maisha yenye afya na kuzuia dhuluma. Pia ilitangazwa Jumatatu kuwa aliyekuwa kiongozi wa wengi wa...

Like
480
0
Tuesday, 15 May 2018
Marekani Kufungua Ubalozi Mpya leo Mjini Jerusalem
Global News

Marekani itafungua ubalozi wake mpya mjini Jerusalem hatua ambayo imesifiwa na Israel na kulaaniwa na Wapalestina ambao wanakusanyika kwa maandamano makubwa. Maafisa wa vyeo vya juu kutoka Marekani watahudhuria sherehe hiyo leo akiwemo binti ya Rais wa Marekani Donald Trump Ivanka na mumewe Jared Kushner. Wengi wa maafisa kutoka Muungano wa Ulaya hawatahudhuria. Uamuzi wa Trump wa kuhamisha ubalozi huo kutoka Tel Aviv umewakasilisha Wapalestina amboa wanadai eneo la Jerusalem Mashariki ni mji wao mku wa badaye. Ambao waliudhibiti toka...

Like
522
0
Monday, 14 May 2018
Zaidi ya watu 40 wafariki baada ya bwawa la Patel kuvunja kuta zake Nakuru Kenya
Global News

Zaidi ya watu 40 wamefariki na maelfu wengine wameachwa bila ya makaazi wakati bwawa moja mjini Nakuru nchini Kenya lilipovunja kuta zake Jumatano usiku. Shirika la kupambana na majanga nchini Kenya linasema watu wengine wengi hawajulikani waliko kufikia sasa. Eneo hilo la Solai katika kaunti ya Nakuru Kenya, lina mabwawa saba yanayotumika katika kilimo cha umwagiliaji. Waziri wa mambo ya ndani Kenya Fred Matiang’i amesema serikali imeanzisha uchunguzi kubaini uthabiti wa mabwawa mengine sita yaliosalia. Maafisa wa uokozi kutoka...

Like
646
0
Friday, 11 May 2018
Chombo cha Satelaiti kilichoundwa Kenya kitarushwa katika anga za juu leo kutoka Japan
Global News

Wanasayansi wa anga za juu kutoka Kenya waliokiunda chombo hicho tayari wako katika makao ya Uchunguzi wa Sayansi ya Anga za juu nchini Japan, (JAXA) ambapo chombo hicho kitarushwa kutoka huko. Nchini Kenya kwenyewe raia wataweza kufuatilia shughuli hiyo moja kwa moja kwenye mtandao wa You Tube, na sherehe maalumu ya kushuhudia imeandaliwa katika chuo kikuu cha Nairobi. Satelaiti hiyo ndogo ni ya thamani ya dola milioni moja – gharama inayoonekana kuwa ndogo kifedha kwa kiwango cha sayansi ya anga...

Like
560
0
Friday, 11 May 2018