Waziri mkuu wa zamani wa Malaysia Dr.Mahathir Mohamad amepata ushindi wa kihistoria katika uchaguzi mkuu uliofanyika katika hilo. Kiongozi huyo ameweza kukiangusha chama ambacho kimekuwa madarakani tangu mwaka 1957 ambacho kimekuwa kikidaiwa kujihusisha na nasuala ya rushwa na ufisadi. Dr.Mahathir ameshinda kwa idadi ya uwingi kura,na kukibwaga chama cha Barisan Nasional kilichotawala kwa zaidi ya miaka 60. Akiwa na umri wa miaka 92 Mhathir ameachana na kuitwa mstaafu na amerejea tena kuchukua nafasi ya mfuasi wake huyo wa zamani yaani...
Viongozi wa mataifa ya magharibi wanasema kuwa wataendelea kuuunga mkono makubaliano ya kinyuklia ya Iran muda mfupi baada ya Marekani kutangaza kuwa inajiondoa katika makubaliano hayo. Uingereza, Ufaransa na Ujerumani zinasema kuwa watafanya kazi pamoja na matiafa yote yaliosalia katika mkataba huo huku ikiitaka Marekani kutovuruga utekelezwaji wake. Mataifa mengine yalioweka mkataba huo wa 2015- Urusi na China pia yamesema yataendelea kuunga mkono makubaliano hayo. Iran imesema kuwa inafanya kazi kunusuru makubaliano hayo bila ya ushirikiano...
Mazungumzo ya muungano wa vyama nchini Italia yameshindikana,hivyo kuiacha nchi ikitakiwa kufanya uchaguzi mpya ama kuwa na serikali ya mpito hadi mwishoni mwa mwaka huu. Rais Sergio Mattarella amesema mazungumzo hayo ilikuwa ndiyo tegemeo la kulifikisha taifa hilo kwenye makubaliano kufuatia vyama vyote vilivyoshiriki uchaguzi mkuu mwezi machi kutofanikiwa kupata ushindi. Hakuna chama chochote binafsi kilichopata kura za kukiwezesha ushindi kama chama. Hata hivyo vyama viwili maarufu vya Five Star na The League,ndivyo vinavyochuana kwa...
Mji wa Nairobi umekumbwa na ukosefu mkubwa wa maji. Wakaazi wengi wa jiji hulazimika kununua maji kwa bei ghali kutoka kwa wachuuzi. Hali hii inaendelea licha ya mvua kubwa inayoendea kunyesha. Katika eneo la Rongai nje kidogo ya mji mkuu Nairobi, mmoja wa wakaazi wa eneo hili anaeleza jinsi imekuwa vigumu kapata maji. ”Nimeishi mtaa huu tangu miaka ya 80 na mpaka sasa, hatujawahi kuona tatizo kubwa la maji kama hili. Shida ya maji ni kubwa kiasi kwamba kutoka mwezi...
Mchezo wa pili wa El Clasico kati ya mahasimu Fc Barcelona na Real Madrid kwa msimu wa La Liga wa 2017/2018 uliopigwa katika dimba la Camp Nou ulimalizika kwa sare ya kufungana magoli 2-2. Mshambuliaji wa Barcelona Luis Suarez, ndio alianza kuipatia timu yake goli la kuongoza katika dakika ya kumi, ya mchezo, iliwachukua dakika nne kwa Madrid kusawazisha goli hilo kupitia kwa nyota wake Cristiano Ronaldo. katika dakika ya 52, mshambuliaji Lionel Messi, aliipatia klabu yake goli la pili...
Vladimir Putin anatarajiwa kuapishwa kwa muhula wa nne kama rais wa Urusi leo Jumatatu baada ya kushinda uchaguzi mnamo Machi. Amekuwa madarakani kwa miaka 18 kama rais na hata waziri mkuu, na wapinzani wameufananisha muda wake wa uongozi kama utawala wa mfalme. Polisi wa kupambana na fujo walikabiliana na waandamanaji wanaopinga utawala wake mjini Moscow na katika miji mingine Jumamosi. Kumekuwa na hofu kwamba huenda kutazuka ghasia tena leo Jumatau wakati anapoapishwa. Sherehe hiyo ya kuapishwa kwake itafanyika Kremlin mjini...
Aliyekuwa daktari wa Donald Trump amesema kwamba si yeye aliyeiandika barua iliyomweleza mgombea huyo wa chama cha Republican wakati huo kuwa aliyekuwa na “afya nzuri ajabu”, vyombo vya habari Marekani vinasema. “ alitunga na kuamrisha kuandika kwa barua yote,” Harold Bornstein aliambia runinga ya CNN Jumanne. Ikulu ya White House haijazungumzia tuhuma hizo za daktari huyo. Bw Bornstein pia amesema maafisa wa serikali walitekeleza “uvamizi” katika afisi zake Februari 2017 na kuondoa nyaraka zote...
Kim Jong-un ameahidi ‘historia mpya’ katika uhusiano na jirani yake wakati akiwa kiongozi wa kwanza wa Korea kaskazini kuingi Korea ksuini tangu kumalizika kwa vita vya Korea mnamo 1953. Katika hatua ilioshangiliwa kwa mbwembwe za kila aina kiongozi wa Korea Kusini na mwenzake wa Korea Kaskazini walisalimiana kwa mikono katika mpaka huo. Kim amesema huu ni ‘mwanzo’ wa amani, baada ya kuvuka eneo la mpaka wa kijeshi unaoigawanya rasi hiyo ya Korea. Ziara hii inajiri wiki kadhaa baada ya Korea...
Watu tisa wameuawa mjini Toronto, nchini Canada baada kugongwa na gari la mizigo ambalo lilielekea katika mtaa wenye watu wengi. Wengine 16 wamejeruhiwa pia. Mashuhuda wanasema kuwa dereva huyo aliendelea kuliendesha gari takribani umbali wa kilomita moja hivi. Diego de Matos yeye alikuwa akiendesha gari lake karibu na eneo hilo,ameiambia BBC kuwa aliona watu wawili wakigongwa na gari hilo la mizigo. “Lori hilo liliwagonga mwanamke na mwanaume.Hata hivyo baada ya kuwagonga watu hao dereva wa gari hilo aliendelea kuendesha gari...
Utafiti umevumbua kwa nini baadhi ya maradhi ya saratani ni hatari kuliko aina nyingine ya saratani ingawa zinaonekana kufanana Taasisi ya wanasayansi ya Francis Crick ilianzisha uchambuzi wa historia ya saratani kwa ajili ya kutabiri mustakabali wake Utafiti kwa wagonjwa wa saratani ya figo unaonyesha kuwa baadhi ya uvimbe ”ni hatari” huku nyingine zikiwa hazina madhara na wakati mwingine hazihitaji matibabu Taasisi ya utafiti la Cancer Research ya Uingereza imesema utafiti huu unasaidia wagonjwa kupata uangalizi mzuri wa kitabibu...
Mwanaharakati wa maswala ya wanawake nchini Rwanda Godelive Mukasarasi amewekwa kwenye orodha ya wanawake 10 mashuhuri duniani. Tuzo aliyopewa na Marekani Bi Godelive Mukasarasi inatokana na juhudi za shirika aliloanzisha nchini Rwanda la SEVOTA kusaidia wakinamama walionusurika na mauaji ya kimbari ya mwaka 1994. Amewekwa kwenye orodha hiyo na nchi ya Marekani ambao hivi karibuni walitunukiwa tuzo ijulikanayo kwa jina”International women of Courage ” kutokana na shughuli za shirika lake la SEVOTA ambalo husaidia wanawake...