Global News

SENETA WA NEBRASKA AKATAA KUMUUNGA MKONO TRUMP
Global News

SENETA wa Nebraska- Ben Sasse amesema hatamuunga mkono mgombea urais anayeongoza miongoni mwa wagombea wa chama cha Republican Donald Trump. Sasse ndiye mwanachama wa kwanza wa ngazi ya juu wa chama cha Republican aliyejitokeza kutangaza hadharani kwamba hatamuunga mkono Trump. Amesema amesikitishwa sana na kuvunjwa moyo na mfanyabiashara huyo na kwamba atamtafuta mgombea mwingine wa kumuunga mkono iwapo Trump atashinda uteuzi wa Republican....

Like
293
0
Tuesday, 01 March 2016
ZUMA ALAANI MATUKIO YA KUCHOMA MOTO VYUO AFRIKA KUSINI
Global News

RAIS wa Afrika Kusini Jacob Zuma amelaani matukio ya kuchomwa moto kwa vyuo vikuu nchini humo.   Rais Zuma amesema hasira haipaswi kuwafanya baadhi ya  wanafunzi kufanya vitendo vinavyoweza kuwakosesha kupata huduma ya elimu pamoja na wenzao.   Kauli hiyo ya Rais Zuma inafuatia matukio ya hivi karibuni yanayodaiwa kufanywa na wanafunzi nchini humo ya  kuyachoma moto majengo ya vyuo kadhaa kwa madai ya kupinga ongezeko la ada za masomo pamoja na masuala ya...

Like
249
0
Friday, 26 February 2016
BAGHDAD: SHAMBULIZI LA KUJITOA MUHANGA LAUA WATU 15
Global News

  KIASI cha watu 15 wameuawa kufuatia shambulizi la kujitoa muhanga linalodaiwa kufanywa na watu wawili wanaoshukiwa kuwa   na mahusiano na wanamgambo wa  kundi la itikadi kali la Dola la Kiisilamu katika eneo la msikiti wa kishia mjini Baghdad.   Kwa mujibu wa vyanzo vya habari vya madaktari na polisi   watu wengine 50 wanadaiwa kujeruhiwa katika tukio hilo.   Duru zinaarifu kuwa mtu wa kwanza  alijitoa muhanga na kufuatiwa  na wa pili ambaye pia alijilipua baada ya maafisa usalama kufika...

Like
276
0
Friday, 26 February 2016
WFP LATOA MSAADA DEIR EL-ZOUR
Global News

MKUU wa Umoja wa Mataifa anayehusika na utoaji wa misaada ya kibinaadamu, Stephen O’Brien, amesema shirika la Mpango wa Chakula duniani, WFP, limedondosha chakula kutoka angani katika mji wa Deir el-Zour, ambao umekuwa ukizingirwa na kundi la Dola la Kiislamu. O’Brien ameliambia baraza la usalama la umoja huo mjini New York kwamba tani 21 za msaada zilidondoshwa. Hata hivyo msemaji wa WFP Bettina Luescher amesema katika taarifa yake kwamba operesheni nzima ilikabiliwa na changamoto za...

Like
243
0
Thursday, 25 February 2016
WANAJESHI 180 WA KENYA WALIUAWA NA AL-SHABAB
Global News

RAIS wa Somalia Hassan Sheikh Mohamoud ametoa maelezo kuhusu idadi ya wanajeshi wa Kenya waliofariki kufuatia shambulio la al-Shabab katika kambi yao huko el-Adde mwezi uliopita.   Rais huyo ametoa idadi hiyo kuwa kati ya wanajeshi 180 na 200 katika mahojiano na runinga moja ya Somali ,Cable TV.   Wapiganaji hao wa al-Shabab wamesema kuwa wanajeshi 100 walifariki na Kenya bado  haijatoa idadi yoyote ya wanajeshi wake...

Like
239
0
Thursday, 25 February 2016
OBAMA ATOA MSUKUMO WA MWISHO WA KUFUNGWA KWA GEREZA LA GUANTANAMO BAY
Global News

RAIS  Barack Obama  wa  Marekani  ameanzisha  msukumo wa  mwisho leo kulishawishi  baraza  la  Congress kulifunga  gereza  la  kijeshi  la Guantanamo Bay nchini Cuba. Rais Obama  amelitaka  baraza  la  Congress kulijadili  kwa kina  pendekezo  lake na  kuongeza  kwamba  hataki kuliacha  suala  hilo  kwa  mrithi  wake mwezi ...

Like
323
0
Wednesday, 24 February 2016
DONALD TRUMP ASHINDA KATIKA JIMBO LA NEVADA
Global News

MGOMBEA wa urais wa chama cha Republican Donald Trump ameshinda katika jimbo la Nevada nchini Marekani, na hivyo basi kuimarisha uongozi wake katika mchujo wa kuwania tiketi ya chama hicho. Tajiri huyo sasa ameshinda mara tatu ,kufuatia ushindi wake katika jimbo la New Hampshire na Carolina kusini. Seneta Marco Rubio na Ted Cruz ambao wamekuwa wakishambuliana wiki hii wanapigania nafasi ya...

Like
219
0
Wednesday, 24 February 2016
NEPAL: NDEGE YA ABIRIA YATOWEKA
Global News

NDEGE ndogo iliyowabeba abiria 21 imetoweka ikiwa maeneo yenye milima nchini Nepal. Ndege hiyo ilikuwa safarini kutoka Pokhara, magharibi mwa mji mkuu Kathmandu, kwenda Jomsom, eneo ambalo watu wengi wanaoenda kukwea milima ya Himalaya huanza safari yao ya kukwea milima hiyo. Hakuna viwanja vya ndege kati ya maeneo hayo mawili na inahofiwa kwamba ndege hiyo ya shirika la ndege la Tara Airlines imeanguka....

Like
233
0
Wednesday, 24 February 2016
IS YATHIBITISHA KUHUSIKA NA MASHAMBULIZI KATIKA MIJI YA DAMASCUS NA HOMS
Global News

KUNDI la kislamu la Islamic State limesema kuwa limetekeleza mashambulizi katika mji mkuu wa Syria Damascus na mji wa Homs, na kusababisha vifo vya watu 140. Kwa mujibu wa taarifa zilizotolewa kwa vyombo vya Habari zimeeleza kwamba Mapema huko Homs watu 57, wengi wao raia wa kawaida wameuawa katika mashambulizi mawili ya magari.   Mashambulizi hayo mawili yamelenga maeneo yaliyozingirwa na waislamu wachache, kama ilivyoelezwa na kundi la waislamu la Sunni la...

Like
254
0
Monday, 22 February 2016
BESIGYE AKAMATWA TENA
Global News

KIONGOZI wa chama cha upinzani cha Forum for Democratic Change (FDC) nchini Uganda Kizza Besigye amekamatwa tena na maafisa wa polisi nchini humo. Watu walioshuhudia kukamatwa kwake wamesema kwamba Kizza amekamatwa alipokuwa akijaribu kuondoka nyumbani kwake alipokuwa amewekwa kizuizini. Awali kulikuwa na habari kwamba kiongozi huyo angefika makao makuu ya Tume ya Uchaguzi kuonesha matokeo rasmi ya uchaguzi wa urais ingawa tayari Tume ya Uchaguzi ilishamtangaza Rais Yoweri Museveni kuwa mshindi wa uchaguzi wa urais uliofanyika Alhamisi wiki...

Like
282
0
Monday, 22 February 2016
140 WAUAWA KWA MILIPUKO YA MABOMU SYRIA
Global News

TAKRIBAN watu 140 wameuawa kwa milipuko ya mabomu katika miji ya Homs na Damascus nchini Syria, waangalizi na vyombo vya habari vya serikali wameeleza.   Inaelezwa kuwa milipuko minne ilitokea katika eneo la Sayyida Zeinab mjini Damascus na kuua takriban watu 83, ambapo awali mjini Homs Watu 57 wengi wao raia waliuawa kwa mashambulizi ya mabomu yaliyokuwa yametegwa kwenye magari mawili.   Wanamgambo wa Islamic State wamekiri kutekeleza mashambulizi hayo katika miji hiyo yote...

Like
236
0
Monday, 22 February 2016