BOTI mbili za doria za Marekani zikiwa na wafanyakazi 10 zimekamatwa nchini Iran. Maafisa wa Marekani wamesema boti hizo zilikuwa katika mazoezi kati ya Kuwait na Bahrain kwenye eneo la Ghuba, baada ya moja wapo kupata matatizo ya kiufundi na kupoteza mwelekeo hadi katika maji ya Iran. Waziri wa Mambo ya Nje ya Marekani John Kery amewasiliana na mwenziye wa Iran Mohammad Javad Zarif, ambaye amemhakikishia kwamba wanamaji wa boti hiyo watarudishwa mara...
SHIRIKA linalohudumia watoto la Umoja wa Mataifa limesema zaidi ya nusu ya watoto walioko Sudan kusini hawako shule. Kwa mujibu wa UNICEF, idadi hiyo ni kubwa kuliko nchi yoyote ile duniani. Shirika hilo limesema watoto wa kike na wakiume wapatao milioni 1.8 hawajapata elimu darasani na kwamba tangu kuzuka kwa vita vya wenyewe kwa wenyewe mwaka 2013 zaidi ya shule mia nane...
RAIS wa Ufaransa Francois Hollande na Meya wa mji wa Paris Anne Hidalgo waliweka bango la taarifa katika eneo la Place de la Republique kuwakumbuka watu 147 waliouawa katika mashambulizi ya kigaidi katika mji mkuu wa Ufaransa, Paris mnamo mwezi Novemba mwaka jana. Rais Hollande aliungana na viongozi wengine na maelfu ya raia kuwakumbuka wahanga hao wa mashambulizi ya kigaidi ambayo kundi la wanamgambo wenye itikadi kali wa Dola la Kiislamu IS lilidai kuhusika. Wiki nzima iliyopita, Ufaransa...
UMOJA wa mataifa umesema kuwa misafara ya magari iliyobeba chakula cha mwezi mzima na dawa leo umeanza kuelekea nchini Syria katika mji wa Madaya eneo ambalo limeathiriwa na njaa ambapo baadhi yao wamekufa kutoka na hali hiyo. Watu zaidi ya elfu 40 wamezuiwa na serikali kutoka katika maeneo hayo na hawajahi kupokea msaada wa chakula tangu mwezi Oktoba mwaka jana. UN wanasema kuwa wanaushahidi kwamba baadhi wamekufa kwa njaa katika mji huo wa Madaya nchini Syria kutokana na...
JESHI la Israel limesema kwa Wapalestina wanne wameuawa kwa kupigwa risasi baada ya kujaribu kuwachoma visu wanajeshi wa Israel katika matukio mawili tofauti eneo la Ukingo wa Magharibi. Watatu waliuawa katika makutano ya barabara ya Gush Etzion, ambako visa kama hivyo vimewahi kutokea awali na mwingine aliuawa karibu na Hebron lakini hakuna mwanajeshi aliyejeruhiwa. Maafisa wa afya wa Palestina wamethibitisha vifo...
RAIS wa Sudan Kusini Salva Kiir kwa mara ya kwanza amewaomba radhi raia wa nchi hiyo kutokana na mateso na dhiki ambayo wamepitia wakati wa mzozo wa kisiasa uliodumu miaka miwili. Rais Kiir amesema kuomba msamaha ndiyo hatua ya kwanza katika kufanikisha maridhiano nchini humo. Amechukua hatua hiyo wakati wa kufungua rasmi mkutano mkuu wa chama tawala cha SPLM. Jana, pande zilizohusika katika mzozo huo ziliafikiana kuhusu kugawana nyadhifa za uwaziri katika baraza la mawaziri la serikali ya...
WATU 70 wameuwawa wakati lori lililokuwa limewekewa miripuko kuripuka katika kambi ya polisi Kaskazini Magharibi ya Libya katika mji wa pwani wa Zliten. Watu wengi wamejeruhiwa katika shambulio hilo la kujitoa muhanga, ambalo lilishambulia kundi la maafisa wa polisi waliokuwa wamekusanyika jana katika kambi . Kwa mujibu wa watu walioshuhudia, lori hilo lililokuwa na miripuko liligonga katika lango la kambi hiyo ambayo inatumiwa kuwapa ...
HATIMAYE, RAIS wa Sudan Kusini Salva Kiir na kiongozi wa waasi Riek Machar wamefikia makubaliano ambapo pande hizo mbili zimekubaliana kuhusiana na muundo wa serikali ya mpito. Kwa mujibu wa makubaliano hayo, serikali inaruhusiwa kuteua mawaziri 16, ambapo upande wa waasi wanaruhusiwa kuteua mawaziri 10. Serikali ya mpito iliyokubaliwa itakuwa madarakani kwa miaka 3 kabla ya uchaguzi mpya kufanyika. Sudan Kusini imekumbwa na vita vya ...
WAFUNGWA wawili waliokuwa wakizuiliwa katika gereza la Guantanamo Bay, Cuba, wamehamishiwa Ghana. Wizara ya Ulinzi ya Marekani imesema idhini ilitolewa kwa Khalid al-Dhuby kuachiliwa huru 2006 na kwa Mahmoud Omar Bin Atef mwaka 2009. Wawili hao, wanaotoka Yemen, wamezuiliwa kwa zaidi ya mwongo mmoja na hawajawahi kufunguliwa...
MZOZO wa kidiplomasia kati ya Saudi Arabia na Iran unazidi kufukuta, huku Iran ikiitaka Saudi Arabia kuachana na msimamo wake wa makabiliano. Waziri wa mambo ya nje wa Iran Javad Zarif, ameitaka Saudi Arabia kuacha kuchochea wasiwasi na kujibu hatua zake za karibuni, ambazo zilisababisha mkwamo...
RAIS Alassane Ouattara wa Ivory Coast amekubali kujiuzulu kwa Waziri Mkuu na Serikali yake. Akituma ujumbe kupitia mtandao wa Twitter, Outtarra amesema waziri mkuu aliwasilisha hati ya kujiuzulu na ile ya serikali naye akairidhia. Ouattara, mwanauchumi mwenye umri wa miaka 74, aliyewahi kulitumikia shirika la fedha la kimataifa na amechaguliwa kwa muhula wa pili wa miaka mitano kama rais, mwezi Oktoba mwaka...