Global News

UN YAANZA MIKAKATI KUIWEKEA VIKWAZO KOREA KASKAZINI
Global News

SIKU moja baada ya Korea Kaskazini kufanya jaribio la bomu la haidrojeni, Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa limekubaliana kuanza mikakati ya kuiwekea vikwazo. Hata hivyo baadhi ya Wataalamu wameonyesha kuwa na wasi wasi kuhusu jaribio la sasa la nyuklia la Korea Kaskazini ambalo ni la nne katika mwongo mmoja, wakisema huenda lisiwe la haidrojeni kutokana na mlipuko uliotokea. Bomu la hydrojeni ni moja ya mabomu hatari ya jamii ya atomiki au nyuklia yenye nguvu zaidi. Wataalam wanasema bomu...

Like
233
0
Thursday, 07 January 2016
NIGERIA: MHUBIRI WA KIISLAM AHUKUMIWA KIFO
Global News

MAHAKAMA moja ya Kiislamu nchini Nigeria imemhukumu kifo mhubiri anayetuhumiwa kukufuru kwa kumtukana Mtume  Muhammad.   Abdul Inyass amehukumiwa katika kikao cha faragha cha mahakama katika mji wa Kano, kaskazini mwa Nigeria.   Afisa wa mashtaka Lamido Abba Soron-Dinki ameliambia shirika la AFP kuwa Kikao hicho kimefanyika faraghani kuzuia “fujo kutoka kwa umma” sawa na ilivyoshuhudiwa wakati wa kikao cha...

Like
242
0
Wednesday, 06 January 2016
KOREA KASKAZINI YATHIBITISHA KUFANYA JARIBIO LA BOMU LA HAIDROJENI
Global News

KOREA KASKAZINI imesema kwa mara ya kwanza imefanikiwa kufanya majaribio ya bomu la nguvu ya maji, maarufu kama bomu la haidrojeni.   Tangazo hili limetolewa na runinga ya taifa baada ya kusikika mitetemeko ya ardhi ya kipimo cha tano nukta moja, karibu na eneo kuliko na kinu cha nyukilia.   Wataalamu wa Marekani wanafanya uchunguzi ikiwa yalikua majaribio ya bomu hilo au ilikua zana nyingine ya nyuklia isiyokuwa na nguvu....

Like
343
0
Wednesday, 06 January 2016
MAREKANI YAWEKA MIKAKATI YA KUDHIBITI SILAHA
Global News

RAIS wa Marekani Barack Obama ametangaza hatua kadhaa zinazonuwiwa kukabiliana na matumizi mabaya ya silaha nchini humo, zikiwemo upatikanaji wa lazima wa leseni kwa wauzaji silaha na kufanya ukaguzi wa historia za wateja.   Obama ametangaza hatua hizo katika ikulu ya White House akiwa amezungukwa na manusura wa mashambulizi ya silaha yanayouwa karibu Wamarekani 30,000 kila mwaka.   Hata hivyo Obama amekiri kuwa hatua hizo alizozipitisha mwenyewe bila kulishirikisha bunge la Congress, hazitomaliza kabisa tatizo la matumizi mabaya ya...

Like
176
0
Wednesday, 06 January 2016
MZOZO WA RIYADH NA TEHRAN WATAJWA KUTOATHIRI MAZUNGUMZO YA AMANI SYRIA
Global News

WAZIRI wa Mambo ya nje wa Saudi Arabia amesema kuwa mzozo unaozidi kufukuta kati ya Riyadh na Tehran hautaathiri mazungumzo ya amani ya Syria.   Taarifa yake ilikuja wakati Kuwait nayo ikimrudisha balozi wake kutoka Iran, kuiunga mkono Saudi Arabia.   Saudi Arabia pamoja na mataifa mengine kadhaa ya Kiarabu, yamechukuwa hatua dhidi ya Iran, baada ya ubalozi wake kushambuliwa na kuchomwa moto na waandamanaji waliokuwa wanapinga kuuawa kwa kiongozi wa Kishia na mkosoaji wa serikali ya Saudi Sheikh Nimr...

Like
184
0
Wednesday, 06 January 2016
KUWAIT YAMUONDOA BALOZI WAKE IRAN
Global News

Kuwait imetangaza kwamba inamuondoa balozi wake kutoka Iran huku mvutano kuhusu kuuawa kwa mhubiri wa Saudi Arabia nchini Saudi Arabia ukizidi.   Ubalozi wa Saudi Arabia nchini Tehran ulivamiwa na kuchomwa moto na waandamanaji waliokuwa wakilalamikia kuuawa kwa mhubiri wa madhehebu ya Shia Sheikh Nimr al-Nimr na watu wengine 46 nchini Saudia Jumamosi.   Saudi Arabia ilivunja uhusiano na Iran baada ya tukio hilo, na washirika wake wa karibu Bahrain na Sudan wakafuata....

Like
195
0
Tuesday, 05 January 2016
WASHUKIWA WA UGAIDI WASAKWA MOMBASA
Global News

MAAFISA wa usalama nchini Kenya wanawasaka washukiwa wanne wa ugaidi ambao wanadaiwa kukwepa msako wa polisi katika nyumba moja Mombasa.   Polisi walipata bunduki mbili na vilipuzi baada ya kuvamia nyumba iliyokuwa ikitumiwa na wanne hao Jumatatu.   Kamishna wa jimbo la Mombasa Nelson Marwa anasema bunduki moja iliyopatikana ilitumiwa kumuua afisa wa polisi mjini humo mwaka...

Like
239
0
Tuesday, 05 January 2016
UINGEREZA YAMTAMBUA MTU WA IS
Global News

VYANZO vya kiintelijensia nchini Uingereza vimeiambia BBC kwamba vinaamini wamemtambua mwanaume mwenye asili ya nchi hiyo ambaye anaonekana katika mkanda wa video wa hivi karibuni wenye kupigia chapuo propaganda za kundi la kigaidi la wanamgambo wa Islamic State.   Vyanzo hivyo vimemtaja mtu huyo kuwa ni Siddhartha Dhar, ambaye anaaminika alikuwa akiishi Mashariki mwa London.   Kwa asili Siddhartha anatajwa kuwa ni Mhindi ambaye aliamua kubadilisha dini yake ya awali na kuwa Mwislamu na inafahamika kuwa baada ya hapo aliamua...

Like
226
0
Tuesday, 05 January 2016
OBAMA KUTANGAZA UHAKIKI WA SILAHA
Global News

RAIS Barack Obama wa Marekani anatarajiwa kutangaza mpango wa kuhakiki silaha katika masoko ya sihala hii leo wakati atakapotangaza mpango huo.   Akizungumza na waandishi wa habari baada ya kukutana na Mwanasheria Mkuu wa nchi hiyo amesema anataka kutumia mamlaka yake ya urais kwa sababu bunge la congress limeshindwa kushughulikia tatizo hilo.   Rais Obama ana matumaini kuwa jambo hilo limepokelewa na wamerekani wengi wakiwemo wamiliki wa silaha, wanaounga mkono na...

Like
215
0
Tuesday, 05 January 2016
BAHRAIN YAVUNJA UHUSIANO WA KIBALOZI NA IRAN
Global News

BAHRAIN imetangaza kwamba imevunja uhusiao wa kibalozi na Iran, saa chache baada ya Saudi Arabia kuchukua hatua.   Saudi Arabia iliwapa maafisa wa ubalozi wa Iran siku mbili kuondoka nchini Saudi Arabia kufuatia mvutano uliotokana na kuuawa kwa muhubiri maarufu wa Kishia.   Muhubiri huyo Sheikh Nimr al-Nimr aliuawa pamoja na watu wengine 46 baada ya kupatikana na makosa yanayohusiana na...

Like
270
0
Monday, 04 January 2016
KENYA: CHUO KIKUU CHA GARISSA CHAFUNGULIWA
Global News

CHUO KIKUU cha Garissa kilichofungwa mwaka uliopita baada ya watu 148 kuuawa kwenye shambulio lililotekelezwa na wanamgambo wa al-Shabab, kimefunguliwa tena leo.   Wafanyakazi wamefika kazini leo huku usalama ukiwa umeimarishwa.   Kila aliyekuwa akiingia katika chuo kikuu hicho kilichoko eneo la kaskazini mashariki mwa Kenya amepekuliwa na maafisa wa usalama. Na Kituo cha polisi, ambacho kitakuwa na maafisa zaidi ya 20 wa kutoa ulinzi, kimejengwa ndani ya chuo kikuu...

Like
281
0
Monday, 04 January 2016