MAKAO MAKUU ya Vatican yemedhibitisha kwamba mshindi wa tuzo ya amani ya Nobel na mtawa Marehemu ‘Mother Teresa’ atatangazwa mtakatifu. Taarifa ya Vatican inasema Papa Francis ameridhia utaratibu wa kumtangaza mtakatifu mtawa huyo baada ya kutambua muujiza wa pili uliohusishwa naye. Muujiza huo alipokea mwanamme raia wa Brazil ambaye alipona saratani kwenye ubongo wake....
MUUNGANO wa Afrika umetangaza mpango wa kutuma walinda amani nchini Burundi kuzuia machafuko zaidi nchini humo. Muungano huo umepanga kutuma walinda Amani elfu 5,000 wa kulinda raia. Umoja wa Mataifa unakadiria watu 400 wameuawa tangu machafuko kuzuka mwezi Aprili baada ya Rais Pierre Nkurunziza kutangaza kwamba angewania urais kwa muhula wa tatu. AU huenda ikalazimika kutuma walinda amani bila kupewa idhini na taifa mwenyeji, muungano huo utatumia kwa mara ya kwanza kifungu kwenye mkataba wake, kinachouruhusu kuingilia kati...
BARAZA la Usalama la Umoja wa Mataifa limepitisha azimio lenye lengo la kukata mifumo ya fedha kwa kundi la Islamic State. Mkutano wa kwanza wa baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa wa mawaziri wa fedha umeafiki juu ya azimio hilo lililobuniwa kwa ajili ya kuzuia fedha kuwafikia wanamgambo wa Islamic State. Mkutano huo umeyataka mataifa kufanya juhudi za haraka kukata mifumo ya udhamini wa fedha kwa kundi hilo kwa kuzuia wizi wake wa mafuta na raslimali nyingine. ...
VIONGOZI wa muungano wa Ulaya wamesema wako tayari kufikia mapatano ya kuiwezesha Uingereza kusalia katika Muungano huo. Hata hivyo viongozi hao wanaokutana mjini Brassels, wamesisitiza kuwa makubaliano yoyote hayapaswi kuvunja kanuni za muungano wa Ulaya. Waziri mkuu wa Uingereza, David Cameron amesema kumekua na mafanikio, lakini akasema bado kuna kazi ngumu inayowasubiri mbele...
WAZIRI MKUU wa Ethiopia Hailemariam Desalegn amesema serikali yake itakabiliana vikali na makundi yanayohujumu amani baada ya watu kadha kuuawa kwenye maandamano eneo la Oromia. Serikali inasema watu watano wameuawa kwenye makabiliano kati ya waandamanaji na vikosi vya usalama lakini makundi ya upinzani na watetezi wa haki za kibinadamu yanasema idadi ya waliofariki inakaribia 40. Akihutubu kupitia runinga ya taifa ya Ethiopia, Bw Desalegn amesema umma pia una jukumu la kutekeleza katika kukabiliana na makundi hayo. ...
MKUTANO maalum wa Baraza la Haki za Binadamu la Umoja wa Mataifa unaendelea mjini Geneva kujadili hali nchini Burundi. Kabla ya mkutano huo kufanyika mjini Geneva, Uswizi, Katibu Mkuu wa umoja UN Ban Ki-moon alikuwa ameonya kuwa taifa hilo limo hatarini ya kutumbukia kwenye mapigano ya wenyewe kwa wenyewe ambayo yanaweza kuathiri kanda yote. Amesema machafuko yaliyotokea nchini Burundi siku za hivi majuzi yanatisha na kwamba atamtuma mshauri wake maalum kwenda Burundi kwa mashauriano ya dharura na serikali....
KIMBUNGA kilichokuwa na kasi ya kilometa 200 kwa saa kimeukumba mji wa Sydney nchini Australia leo , na kuezuwa mapaa ya nyumba katika kitongoji cha kusini ya pwani ya mji huo na kusababisha mafuriko na mvua ya mawe. Kimbunga hicho , kilichokuwa na upepo mkali kuwahi kuonekana katika mji wa Sydney , kilikuwa sehemu ya kimbunga kikubwa kilicholikumba eneo la pwani ya kusini ya New South Wales na Sydney kabla ya kuelekea upande wa ...
MAHAKAMA ya juu zaidi Korea Kaskazini imemhukumu mhubiri kutoka Canada kifungo cha maisha jela na kazi ngumu. Hyeon Soo Lim, mwenye umri wa maika 60, aliyekamatwa mjini Pyongyang baada ya kuzuru taifa hilo Januari kwa kazi ya kibinadamu amehukumiwa kwa makosa ya “uhalifu dhidi ya dola.” Bw Lim, ambaye ni kiongozi wa Light Korean Presbyterian Church, anadaiwa kukiri kuhusika katika njama ya kupanga kupindua serikali na kuunda taifa la...
WAGOMBEA wa Republican wanaowania nafasi ya urais nchini Marekani wamejibizana kuhusu njia bora zaidi za kudumisha usalama wa taifa na kukabiliana na Islamic State (IS) kwenye mdahalo wa kwanza tangu kutokea kwa mashambulio ya California na Paris. Mgawanyiko mkubwa umetokea kati ya wale wanaotetea kuwepo kwa upeelezi zaidi na wale wanaotetea haki za kiraia. Mgombea anayeongoza, Donald Trump, amelazimika kujitetea kutokana na pendekezo lake kwamba Waislamu wazuiwe kuingia Marekani, huku Mgombea mmoja anayempinga vikali, Jeb Bush, akimwita Trump...
MIILI ya watu wapatao 19 imepatikana katika jimbo la mexico la Guerrero, ambako wanafunzi 43 walitoweka mwaka jana. Polisi wanasema miili hiyo ilitupwa kwenye mto mwembamba, wenye kina cha mita mia tano katikati ya miamba na miti karibu na kijiji cha Chichi-hua-lco. Miili nane kati ya hiyo ilikuwa inaonekana kuchomwa baadhi ya viungo....
SAUDI ARABIA imetangaza kuunda muungano mpya wa kijeshi wa nchi 34 za kiislamu kwa lengo la kukabiliana na vitendo vya ugaidi. Shirika rasmi la habari la Saudi Arabia limesema kazi ya muungano huo itaratibiwa katika kituo cha pamoja mjini Riyadh. Akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari, waziri wa ulinzi wa Saudia, Mwanamfalme Mohammed bin Salman, amesema kuwa muungano huo utaratibu juhudi za mapigano dhidi ya makundi yenye itikadi kali katika mataifa ya Syria, Iraq, Libya, Misri na...