Global News

MELI YA IRAN YATEKWA NYARA SOMALIA
Global News

MAHARAMIA wa Somalia wameiteka nyara meli moja ya Iran iliyokuwa na wafanyi kazi 15. Taarifa iliyotolewa na maafisa wakuu wa Somalia imeeleza kuwa Meli hiyo imetekwa nyara licha ya tahadhari iliyotolewa awali kuwa kuna uwezekano wa maharamia kuanza tena shughuli za kiharifu katika maeneo ya bahari ya Hindi. Hata hivyo imeelezwa kwamba ingawa matukio ya uharamia yamejitokeza kwenye maeneo ya bahari hiyo karibu na ufuo wa Somalia, imebainika kuwa vitendo hivyo vimepungua kwa kiasi kikubwa katika kipindi cha miaka mitatu...

Like
277
0
Tuesday, 24 November 2015
MAREKANI: KIJANA ALIYEUNDA SAA ADAI FIDIA
Global News

MVULANA mwenye umri wa miaka 14 aliyejipatia umaarufu baada ya kukamatwa kwa kupeleka saa ya kujitengenezea shuleni, anadai fidia ya dola za marekani milioni 15. Ahmed Mohammed alitiwa mbaroni na polisi wa mji wa Irving, jimbo la Texas nchini Marekani baada ya saa yake kudhaniwa kuwa kilipuzi na baadaye akafukuzwa shule. Mawakili wake wanadai dola milioni 10 za marekani kutoka kwa mji wa Irving na dola milioni5 kutoka kwa shule ya Irving Independent, wakisema Ahmed alifedheheshwa na kuathirika...

Like
284
0
Tuesday, 24 November 2015
HALI YA TAHADHARI KUENDELEZWA BRUSSELS
Global News

WAZIRI Mkuu wa Ubelgiji, Charles Michel amesema hali ya tahadhari itaendelea kubaki kwa kiwango cha juu katika mji wa Brussels. Waziri huyo amesema wasiwasi wa tishio la ushambulizi kama lililowahi kutokea siku kumi zilizopita mjini Paris bado ni mkubwa ingawa kuanzia Jumatano shule zitafunguliwa na usafiri wa treni katika mji mkuu utakuwepo. Mamlaka ya Ubelgiji imesema hadi sasa inawashitaki watuhumiwa wanne kwa kujihusisha katika shughuli zinazohusiana na...

Like
255
0
Tuesday, 24 November 2015
TISHIO LA UGAIDI: MAREKANI YATOA TAHADHARI KWA RAIA WAKE
Global News

SERIKALI ya Marekani imetoa tahadhari ya kusafiri duniani kote kwa raia wake, ikiwaonya kuwepo kwa ongezeko la tishio la kigaidi. Tahadhari hiyo imeeleza kuwa taarifa zilizopo kwa sasa zinaashiria kwamba makundi ya kigaidi ikiwemo Islamic State, Al-Qaeda na Boko Haram wanaendelea kupanga mashambulio katika maeneo tofauti. Hata hivyo, Afisa kutoka Wizara ya Mambo ya Nje ya Marekani amesema kwamba hakuna sababu ya kuamini kwamba raia wa Marekani ndio walengwa wa mashambulio...

Like
279
0
Tuesday, 24 November 2015
ARGENTINA: MAURICIO MACRI ATHIBITISHWA KUWA MSHINDI WA UCHAGUZI
Global News

MGOMBEA Urais kupitia chama cha upinzani cha Conservative Mauricio Macri amethibitishwa kuwa mshindi wa uchaguzi wa urais nchini Argentina huku mgombea wa chama tawala akikubali kushindwa. Matokeo yaliyotangazwa yameonesha Macri amepata asilimia 52 ya kura zote zilizopigwa huku mgombea wa chama Tawala Daniel Scioli akipata asilimia 48. Hata hivyo katika Uchaguzi wa awamu ya kwanza uliofanyika mwezi Oktoba Macri ambaye ni meya wa zamani wa Buenos Aires, alikuwa ameshindwa na Scioli ambaye ni gavana wa mkoa wa Buenos Aires....

Like
270
0
Monday, 23 November 2015
16 WATIWA NGUVUNI BRUSSELS
Global News

UBELGIJI imesema kuwa imewakamata watu 16 katika operesheni ya polisi ya kupambana na ugaidi mjini Brussels. Katika msako huo, nyumba kumi na tisa zimekaguliwa, ingawa hakuna silaha zilizokamatwa. huku mtuhumiwa mkuu wa shambulio lililotokea mjini Paris, Salah Abdeslam, bado hajakamatwa. Operesheni hiyo ya polisi kuhusiana na tishio la ugaidi mjini Brussels imemalizika bila kupatikana kwa vithibitisho vya kutosha kwa wahusika hali iliyosababisha mamlaka ya mji huo kuongeza muda ili kufanya uchunguzi Zaidi wa tukio...

Like
254
0
Monday, 23 November 2015
PARIS: MWILI WA MSHUKIWA WA 3 WA UGAIDI WAPATIKANA
Global News

MWILI wa mshukiwa wa 3 wa kosa la kigaidi umepatikana katika nyumba ya Saint-Denis iliovamiwa na maafisa wa polisi kuhusiana na shambulizi la Paris, kulingana na kiongozi wa mashitaka nchini humo. Vilevile amethibitisha kuwa mwanamke mmoja ni miongoni mwa watu watatu waliouawa, huku pasipoti ilio na jina la Hasna Aitboulahcen ilipatikana kwenye begi lake katika eneo hilo. Hata hivyo Mwili mmoja umetambulika kuwa wa kiongozi wa shambulio hilo Abaaoud...

Like
250
0
Friday, 20 November 2015
MALI: WATU WENYE SILAHA WASHAMBULIA HOTELI
Global News

WATU wenye silaha wameshambulia hoteli ya Radisson Blu katika mji mkuu wa Mali, Bamako. Ripoti zinaeleza kwamba Kuna dalili kwamba hilo ni jaribio la kuwachukua watu mateka ambapo Milio ya risasi imesikika kutoka nje ya hoteli hiyo. Hata hivyo Maafisa wa usalama wa serikali ili kupata usaidizi kurejesha usalama na hali ya kawaida hotelini hapo pamoja na wananchi wote walio karibu na maeneo hayo. sehemu ya...

Like
256
0
Friday, 20 November 2015
ANGELA MERKEL: SULUHU YA MZOZO WA WAHAMIAJI ITAPATIKANA NJE YA ULAYA
Global News

KANSELA wa Ujerumani Angela Merkel amesema mzozo wa wahamiaji unaolikumba bara la Ulaya utasuluhishwa katika mipaka ya nje ya Umoja wa Ulaya na mbali ya mipaka hiyo. Akizungumza akiwa na Kansela wa Austria Werner Faymann, Merkel amesema Ulaya inahitaji uimara na kasi zaidi kuhusu kushughulikia maeneo yaliyo na utata ikiwemo Ugiriki ambako wakimbizi na wahamiaji wanaweza kusajiliwa. Ujerumani imeshuhudia ongezeko la wahamiaji huku ikiwapokea zaidi ya wahamiaji laki saba hadi kufikia mwezi...

Like
212
0
Friday, 20 November 2015
NEW ZEALAND WAPIGA KURA KUCHAGUA BENDERA YA TAIFA
Global News

RAIA nchini New Zealand leo wanapiga kura kuchagua bendera ya Taifa ambayo huenda ikachukua nafasi ya bendera ya sasa. Kura hiyo ya maamuzi inapigwa kuanzia leo hadi Desemba 11 kupitia posta kuamua bendera moja kati ya tano zilizopendekezwa ambayo ni bora zaidi. Waziri Mkuu wa nchi hiyo John Key amesema bendera ya sasa haiakisi hali halisi ya New Zealand na kuamini kuwa bendera hiyo inafanana na bendera ya...

Like
238
0
Friday, 20 November 2015
MISIKITI YA US NA CANADA YAKABILIWA NA TISHIO
Global News

MISIKITI iliyopo nchini Marekani na Canada inakabiliwa na ongezeko la uharibifu na vitisho vya kigaidi tangu kutokea kwa shambulio kali mjini Paris. Vituo vya kiislamu vimekuwa vikipokea ujumbe wa chuki katika simu huku baadhi ya misikiti ikichapishwa michoro ya moto na jumbe za kulipiza kisasi. Hata hivyo Nchini Canada, mtu mmoja aliyekuwa amejifunika uso wake amekamatwa na maafisa wa polisi baada ya kutishia kuwaua waislamu huko Quebec na kutishia kumuua mwarabu mmoja kila...

Like
220
0
Thursday, 19 November 2015