WANAJESHI wa Marekani wakishirikiana na wanajeshi wa Iraq wamefanikiwa kuwakomboa mateka 70 waliokuwa wakizuiliwa na wapiganaji wa Islamic State (IS) nchini Iraq. Idara ya ulinzi ya Marekani imesema operesheni ya kuwakomboa mateka hao ilitekelezwa baada ya kubainika kwamba walikuwa karibu kuuawa. Lakini mwanajeshi wa Marekani aliyejeruhiwa kwenye operesheni hiyo amefariki na ndiye mwanajeshi wa kwanza kufariki tangu kuanza kwa operesheni ya wanajeshi wa Marekani dhidi ya IS mwaka jana. ...
RAIS wa Afrika Kusini Jacob Zuma amepangiwa kukutana na viongozi wa wanafunzi wa vyuo leo kujadili maandamano ya wanafunzi yaliyosababishwa na kuongezwa kwa ada ya masomo. Wanafunzi wamekuwa wakiandamana wiki moja sasa, hasira nyingi zikielekezwa kwa chama tawala African National Congress (ANC). Jana, maelfu ya wanafunzi walikusanyika nje ya makao makuu ya ANC mjini Johannesburg wakitaka elimu itolewe kwa wote bila malipo...
MAJADILIANO kuhusiana na hatua zinazoweza kuchukuliwa kimataifa kupambana na mabadiliko ya tabia nchi yamelalamikiwa kuwa yanaendelea kwa kasi ndogo . Mazungumzo hayo yanayofanyika mjini Bonn yana lengo la kupata msimamo wa pamoja kabla ya mkutano wa mwezi Desemba wa Umoja wa Mataifa mjini Paris wakati viongozi wa dunia wataamua kuhusu makubaliano yatakayofuatwa kisheria na kila taifa duniani kote. Kundi la mataifa yanayojulikana kama G77, ...
RAIS wa Afrika kusini Jacob Zuma amesema atakutana na viongozi wa wanafunzi na maafisa wa vyuo vikuu kesho Ijumaa kujadili mpango wa kupandisha ada ambao umezusha maandamano ya wiki nzima katika taifa hilo. Wakosoaji wanasema ongezeko hilo litaleta athari kwa wanafunzi Waafrika , ambao tayari ni wachache. Akizungumza leo, rais Zuma hajaweka wazi juu ya maandamano hayo hapo kabla , na jana wanafunzi walivamia viwanja vya bunge mjini Cape...
MAKAMU wa Rais wa Marekani Joe Biden ametangaza kwamba hatawania urais mwaka ujao. Ni wazi sasa kuwa Bernie Sanders ndiye mpinzani mkuu wa Mama Hillary Clinton kwa uwaniaji wa Urais wa Marekani kupitia chama cha Democrat, baada ya Makamu wa Rais Joe Biden kutangaza kuwa hatagombea Urais wa Marekani. Akiongea katika mji mkuu wa New York, Bwana Sanders alimpongeza Makamu wa Rais kwa kutoa huduma muhimu kwa jamii kwa muda...
MAREKANI imeshutumu Urusi kwa kumpa mapokezi ya heshima Rais wa Syria Bashar al-Assad mjini Moscow. Afisa wa wizara ya masuala ya ndani ya Marekani amesema taifa hilo halijashangazwa na ziara hiyo, lakini wasiwasi mkubwa kwa Marekani ni Urusi kuendelea kumsaidia kivita Assad kitendo ambacho inaamini kuwa litaipa nguvu zaidi serikali ya Assad na hivyo kuendeleza mapigano ya wenyewe kwa wenyewe nchini humo. Ziara hiyo ya kiongozi wa Syria ilifanyika wiki tatu baada ya Urusi kuanza kushambulia kwa ndege ngome za...
POLISI nchini Congo Brazaville wamefyatua risasi na mabomu ya kutoa machozi kwa waandamanaji walioitikia mwito wa upinzani wa kuendelea na siku ya pili ya maandamano ya kupinga nia ya rais aliyeko madarakani Denis Sassou Nguesso kuwania muhula wake wa tatu. Waandamanaji wameweka vizuizi barabarani huku wakipigana na maafisa wa usalama. Maeneo ya Kusini mwa jiji hilo la Brazzaville ndio lililoathirika zaidi na makabiliano hayo baina ya waandamanaji na...
URUSI na Marekani zimetia saini makubaliano yanayotarajiwa kuzuia ndege za kijeshi za nchi hizo kushambuliana nchini Syria. Habari za kutiwa saini kwa mkataba huo zimethibitishwa na maafisa kutoka nchi zote mbili. Urusi ilianza kushambulia kwa ndege maeneo ya Syria Septemba 30, ikisema ilikuwa ikiwalenga wapiganaji wa kundi la Islamic State –IS, Nna wiki iliyopita, Marekani ilisema ndege za mataifa hayo zilikuwa zimeingia eneo moja la mapigano na zilikuwa karibu sana...
KATIBU MKUU wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-Moon ataliarifu baraza la usalama la Umoja wa Mataifa leo, kuhusu ziara yake ya Mashariki ya Kati, iliyolenga kutuliza ghasia zilizodumu kwa wiki kadhaa sasa. Ban Ki-Moon alitoa ombi la kuzungumza na baraza hilo haraka kupitia njia ya video, kutokea mji wa Ramallah, uliyoko katika Ukingo wa Magharibi wa Palestina. Katibu mkuu huyo wa Umoja wa Mataifa alifanya ziara ya kustukiza katika eneo hilo jana, ili kutoa onyo kwa pande mbili...
CHAMA cha upinzani nchini Canada cha Liberal kimeshinda uchaguzi mkuu na kufikisha kikomo uongozi wa karibu mwongo mmoja wa chama cha Conservative. Chama hicho kinachoegemea siasa za mrengo wa kati, chini ya uongozi wa Justin Trudeau, kilianza kampeni kikishikilia nafasi ya tatu kwa mujibu wa kura za maoni lakini sasa kimeongoza kwa kura. Trudeau, mwenye umri wa miaka 43, ambaye ni mtoto wa aliyekuwa waziri mkuu Pierre Trudeau, amesema raia wa Canada walipigia kura mabadiliko halisi ambapo pia Waziri Mkuu...
Milipuko imesikika katika mji mkuu wa Congo, Brazzaville kufuatia maandamano makubwa yaliyoitishwa na vyama vya upinzani kupinga hatua ya rais aliyeko madarakani Denis Sassou Nguesso kutaka kubadilisha katiba ili kumruhusu kuwania muhula wa tatu. Vyama vya upinzani viliitisha maandamano hayo na inasemekana kuwa wanajaribu kuingia katikati mwa jiji hilo la Brazzaville. Serikali ilikuwa imepiga marufuku maandamano yoyote kabla ya kura ya maoni itakayoamua iwapo katiba ya taifa hilo itabadilishwa au...