Global News

LIBYA: BUNGE LAKATAA SERIKALI YA UMOJA WA KITAIFA
Global News

BUNGE la Libya linalotambulika na Jumuiya ya kimataifa limeyakataa mapendekezo ya Umoja wa Mataifa ya kuunda serikali ya umoja wa kitaifa. Mbali na hayo Baraza hilo la wawakilishi limesema kuwa litashiriki mazungumzo ya Amani ya Umoja wa Mataifa pamoja na mahasimu wao wanaoendesha serikali nyingine kutokea mji mkuu wa Tripoli. Hata hivyo Mataifa ya Magharibi yanazishinikiza pande mbili kuyaafiki makubaliano ya Umoja wa Mataifa, miaka minne tangu kuangushwa na kuuawa kwa kiongozi wa muda mrefu wa Taifa hilo Muammar Ghadhafi....

Like
218
0
Tuesday, 20 October 2015
MAANDAMANO YAFANYIKA DRESDEN
Global News

WATU wasiopungua Elfu 15 wameandamana katika mitaa ya mji wa Dresden jana jioni, kuadhimisha mwaka mmoja tangu yalipofanyika maandamano ya kwanza ya vuguvugu la PEGIDA. Kauli zilizokuwa zinatumiwa na miongoni mwa waandamanaji hao zilikuwa za hisia kali dhidi ya Kansela wa Ujerumani Angela Merkel kuhusiana na msimamo wake wa kuwaunga mkono wakimbizi. Polisi mjini Dresden imeripoti kuwa makabiliano kati ya waandamanaji wa PEGIDA ikimaanisha Wazalendo wa Ulaya dhidi ya Kusilimishwa kwa mataifa ya Magharibi,” walifanya maandamano yake ya...

Like
200
0
Tuesday, 20 October 2015
SHAMBULIO LAUA 3 BERSHEBA
Global News

WATU watatu wameuwawa kufuatia shambulio katika kituo cha  mabasi mjini Bersheba. Waliouawa ni pamoja na kijana wa kipalastina aliyefanya shambulio hilo,mwanajeshi mmoja wa Israel na mtu mwingine aliyepigwa risasi akidhaniwa kuwa gaidi. Polisi inasema kijana huyo wa kipalastina alianza kwa kumpiga risasi mwanajeshi wa Israel,kabla ya kumpokonya bunduki yake na baadae...

Like
283
0
Monday, 19 October 2015
MSHAMBULIAJI AUAWA ISRAEL
Global News

RAIA mmoja wa Israel ameuawa katika mapambano ya kurushiana risasi na kuchomana visu yaliyozuka katika kituo cha Basi kusini mwa mji wa Beersheva. Hata hivyo katika mapambano hayo watu wengine kumi walijeruhiwa wanne kati yao wakiwa ni Polisi. Mtu aliyetekeleza shambulio hilo anadhaniwa kuwa ni raia wa Palestina ambaye alipigwa risasi na Polisi na...

Like
248
0
Monday, 19 October 2015
MAMIA YA WAHAMIAJI WAINGIA SLOVENIA
Global News

MAMIA ya wahamiaji wamevuka na kuingia Slovenia kutoka Croatia leo, baada ya Serikali ya Hungari kufunga mpaka wao ambapo Siku ya Jumamosi Wahamiaji 2,500 waliruhusiwa kuingia Slovena.   Serikali ya Slovenia imesema inaweza kuhudumia idadi kama hiyo tu kwa siku na Hungary ilisema kuwa ilifunga mpaka wake na Croatia usiku wa Kuamkia Jumamosi kwa sababu viongozi wa Muungano wa Ulaya walishindwa kukubaliana juu ya mpango wa kupunguza idadi ya watu wanaotafuta hifadhi.   Msemaji wa UNHCR, Babar Baloch, amesema kuwa...

Like
211
0
Monday, 19 October 2015
UMOJA WA ULAYA NA UTURUKI KUKABILIANA NA ONGEZEKO LA WAHAMIAJI
Global News

UMOJA wa Ulaya na Uturuki zimekubaliana kushirikiana pamoja kukabiliana na ongezeko la wahamiaji wanaoingia barani Ulaya.   Viongozi wa nchi za Umoja wa Ulaya na Uturuki walifanya mkutano wa kilele hapo jana mjini Brussels na kukubaliana kuwa na mpango wa pamoja wa kushughulikia mzozo huo licha ya kuwa bado baadhi ya masuala hayajafikiwa kikamilifu.   Uturuki kwa hivi sasa inawahifadhi zaidi ya wakimbizi milioni mbili wengi wao kutoka Syria na ni mojawapo ya kituo kinachotumika na wahamiaji kuingia barani...

Like
206
0
Friday, 16 October 2015
AFRIKA KUSINI YAPEWA MUDA KUTOA MAELEZO YA KUSHINDWA KUMKAMATA RAIS OMAR AL BASHIR
Global News

MAHAKAMA ya kimataifa inayoshughulikia kesi za uhalifu ICC imeipa Afrika Kusini muda zaidi kutoa maelezo ni kwanini ilishindwa kumkamata Rais wa Sudan Omar al Bashir anayetakiwa na mahakama hiyo kujibu mashitaka ya uhalifu wa kivita wakati alipoizuru nchi hiyo mwezi Juni mwaka huu. Nchi hiyo ambayo ni mwanachama wa mkataba wa Roma, ina wajibu wa kuheshimu na kutekeleza maagizo ya mahakama ya ICC lakini serikali ya Afrika Kusini ilikataa kumkamata Bashir na kumruhusu kuondoka nchini humo kinyume na agizo la...

Like
303
0
Friday, 16 October 2015
MAJESHI YA MAREKANI KUSALIA AFGHANISTAN
Global News

RAIS wa Marekani,Barack Obama ametangaza kuongeza muda wa majeshi ya Marekani kuwepo nchini Afghanistan. Takriban wanajeshi 10,000 wataendelea kubaki nchini humo kwa kipindi hasa cha mwaka ujao. Obama amesema vikosi vya Afghanistan havina nguvu bado ya kupambana na tishio linaloongezeka kutoka kwa wanamgambo wa Taliban....

Like
283
0
Friday, 16 October 2015
NIGERIA: SHAMBULIO LA KUJITOA MHANGA LAUA 26 MSIKITINI
Global News

WATU  kadhaa  wameuawa baada ya bomu kuripuka ndani  ya msikiti  katika mji  wa Maiduguri  kaskazini  mashariki  mwa  Nigeria. Idadi  kamili  ya  watu waliouawa bado  haijajulikana lakini  gazeti  la Nigeria, Vanguard  limearifu kwamba  watu  26 wamekufa. Kwa mujibu  wa waliolishuhudia  tukio  hilo, washambuliaji  wawili  wa  kujitoa mhanga walijichanganya na watu  waliokuwamo msikitini,  Wameeleza  kuwa mmoja wa washumbuliaji  aliingia ndani  ya msikiti na...

Like
224
0
Friday, 16 October 2015
MAREKANI YAPELEKA MAJESHI CAMEROON KUPAMBANA NA BOKO HARAM
Global News

RAIS wa Marekani, Barack Obama ametangaza kuwa vikosi vya marekani vyenye silaha vimepelekwa Cameroon kusaidia mapambano dhidi ya wanamgambo wa Boko Haram. Kikosi cha wanajeshi 300, kitafanya operesheni za upelelezi, kijasusi na operesheni za kipelelezi katika ukanda mzima. Cameroon na Chad zimekuwa zikilengwa na wanamgambo hao kutoka kaskazini mwa Nigeria na Obama amesema vikosi hivyo vitaendelea kubaki Cameroon mpaka watakapokuwa hawahitajiki...

Like
190
0
Thursday, 15 October 2015
GHASIA KENYA: CHUO CHAFUNGWA
Global News

CHUO kikuu kimoja nchini Kenya kimefungwa baada ya mwanafunzi mmoja kufariki wakati wa makabiliano kati ya wanafunzi na polisi usiku wa jana. Kaimu Naibu Chansela wa chuo kikuu hicho cha Maseno Bi Catherine Muhoma, ameagiza chuo hicho kufungwa haraka kutokana na vurugu kuzidi. Ghasia zilianza baada ya polisi kudaiwa kulifyatulia risasi gari lililokuwa likitumiwa na wanafunzi kupigia debe mmoja wa wagombea katika kampeni za uchaguzi wa viongozi wa wanafunzi...

Like
206
0
Tuesday, 13 October 2015