Sports

MAYWEATHER KUTUMIA DOLA ELFU ISHIRINI NA TANO ZA KIMAREKANI KULINDA MENO YAKE
Slider

Ikiwa zinahesabika siku na masaa kuelekea kwenye pambano linalosuriwa kwa hamu ulimwenguni kati mmarekani Floyd Mayweather na mfilipino Manny Pacquiao, Mayweather ameendelea kutamba na kumfanya azidi kuzungumziwa na vyombo vya habari duniani Taarifa kutoka jarida la Forbes la nchini Marekani zinasema Mayweather atatumia kifaa cha kulinda meno (mouth Guard) chenye gharama ya dola za kimarekani elfu ishirini na tano....

Like
278
0
Thursday, 16 April 2015
USIKU WA ULAYA: BARCELONA YAITIKISA PSG NYUMBANI
Slider

Kwenye usiku wa Ulaya jana michezo miwili ilichezwa katika hatua ya robo fainali ambapo FC Porto ya Ureno waliwakaribisha Bayern Munich ambapo mchezo huo ulimalizika kwa Bayern Munich kukubali kichapo cha 3-1. Huko nchini Ufaransa pia Paris Saint German ilikuwa mwenyeji wa miamba ya soka ya Hispania Barcelona ambapo mchezo huo ulimalizika kwa PSG kukubali kichapo cha 3-1 katika uwanja wa nyumbani. Magoli ya Barcelona yalitiwa nyavuni na Neymar Jr huku Luis Suárez akiziona nyavu za PSG mara mbili magoli...

Like
229
0
Thursday, 16 April 2015
MASWALI YA DK. PANJUAN KWA HANS POPE
Slider

...

Like
483
0
Wednesday, 15 April 2015
MARIA SHARAPOVA KUIKOSA FED CUP
Slider

  Maria Sharapova mchezaji nambari mbili duniani katika mchezo wa tennis hatocheza mchezo wa nusu fainali mwishoni mwa wiki hii dhidi ya mjerumani kwenye mashindano ya Fed Cup yanayofanyika huko Sochi nchini Urusi. Maamuzi hayo yakumuondoa Sharapova yamekuja kufuatia kusumbuliwa na jeraha la mguu Akizungumza na waandishi wa habari, Sharapova ameonesha masikitiko yake kutokana na namna alivyokuwa na hamasa ya kufanya vizuri katika mashindano hayo. “ mimi na timu yangu tulibadilisha ratiba ya mazoezi ili kuweza kuiwakilisha nchi yangu...

Like
167
0
Wednesday, 15 April 2015
UEFA: WABABE WA JIJI LA MADRID WATOANA JASHO
Slider

Wababe wa jiji la Madrid nchini Hispania jana wameshindwa kutambina katika mchezo wa kwanza wa Kombe la Mabingwa barani Ulaya,UEFA, hatua ya robo fainali baada ya kutoka sare ya bila kufungana 0-0. Katika mchezo huo uliochezwa katika dimba la Vicente Calderon Athletico Madrid walikuwa wenyeji wa Real Madrid ambapo timu hizo zitarudiana katika uwanja wa Bernabeu tarehe 22 Aprili. Nyota ya mshambuliaji wa real Madrid Gareth Bale ilishindwa kung’aa jana baada ya kukosa nafasi ya wazi mnamo dakika ya tatu...

Like
671
0
Wednesday, 15 April 2015
LIVERPOOL KUMCHUNGUZA RAHEEM STERLING
Slider

Raheem Sterling arejesha matumaini kwa klabu ya soka ya Liverpool kuingia kwenye top four kwenye ligi ya Uingereza lakini pia kujihakikishia nafasi kwenye msimu ujao wa ligi ya mabingwa baada ya kuichabanga 2-0 klabu ya Newcastle United katika uwanja wa Anfield hapo jana. Kikosi cha Newcastle United kilimpoteza nahodha wa timu hiyo Moussa Sissoko alietolewa nje ya mchezo kwa kadi kwenye dakika ya saba Sterling mwenye umri  wa miaka 20 ameingia kwenye wakati mgumu kufuatia kunaswa kwa video inayomuonesha akivuta...

Like
188
0
Tuesday, 14 April 2015
PHILL NEVILLE AMTETEA YAYA TOURE NA KUMMWAGIA LAWAMA MANUEL PELLEGRINI
Slider

Kufuatia matokeo mabaya iliyoyapata klabu ya Manchester City kwenye mchezo wake na klabu ya Manchester United siku ya jumapili ambapo mchezo huo ulimalizika kwa Manchester United kuichabanga Man City bao 4-2, ikiwa ni mchezo wa sita kwa klabu ya man City kuupoteza kati ya michezo nane. Akizungumza na kituo cha Bbc mchezaji wa zamani wa timu ya taifa ya England na Manchester Utd, Phil Neville ametoa utetezi wake kwa Yaya Toure wa Manchester City kwa kusema kuwa mwanandinga huyo si...

Like
180
0
Tuesday, 14 April 2015
TANZANIA KUSHIRIKI KIGALI MARATHON
Slider

Tanzania yaingia kwenye orodha ya nchi zinazotarajiwa kushiriki kwenye mbio za Kigali Marathon May 23-24 huko Rwanda, huku nchi kadhaa zikialikwa. Chama cha riadha nchini Rwanda (RAF) kimeeleza kuwa mbio hizo ni na msisitizo wa kudumisha amani kupitia michezo.wakimbiaji watashindana katika mbio ndefu (kilometa 42) na half marathon (kilometa 21) kwa upande wa wanawake na wanaume. Mbio hizo zitaanza uwanja wa Amahoro. Wanariadha wengi kwa sasa wapo katika matayarisho na mashindano mbalimbali yakiwemo ya Olimpiki yatakayofanyika Rio de Janeiro,...

Like
176
0
Monday, 13 April 2015
PELLEGRINI KUTETEA KIBARUA CHAKE LEO
Slider

Mwalimu wa klabu ya Manchester City Manuel Pellegrini amesisitiza kuwa klabu yake hiyo haina mgogoro. Pellegrini ambae ni raia wa Chile atakuwa na kibarua kikgumu leo kutetea kibarua chake kisiote nyasi pindi klabu hiyo itakaposhuka dimbani kuchuana vikali na Manchester United kwenye uwanja wa Old Trafford Manchester City imeshuka hadi nafasi ya nne kufuatia msururu mbaya wa matokeo baada ya kushinda mara mbili pekee kati ya mechi saba. Pellegrini Kocha Pellegrini amewaona wapinzani wake Arsenal na Manchester United wakipanda katika...

Like
211
0
Sunday, 12 April 2015
CRICKET: RICHIE BENAUD AFARIKI DUNIA
Slider

Aliekuwa nahodha wa timu ya cricket ya Australia Richie Benaud amefariki dunia akiwa na umri wa miaka 84. Benaud alistaafu mchezo huo mwaka 1964 na kuingia kwenye taaluma ya habari ambapo kazi yake ya mwisho kama mchambuzi aliifanya nchini Uingereza mwaka 2005 kwenye michuano ya Ashes Series na baadae alikwenda kukitumikia kituo cha Channel Nine huko Australia mpaka mwaka 2013. Mwezi November aligundulika kuwa na ugonjwa wa saratani ya ngozi Kufuatia heshima aliyojiwekea kwenye mchezo huo duniani wadau mbalimbali wametoa...

Like
198
0
Friday, 10 April 2015
TANZANIA YAPOROMOKA KWENYE VIWANGO VYA FIFA
Slider

Shirikisho la mpira wa miguu duniani FIFA limetangaza viwango vipya ambapo kushuka na kupanda kwa viwango kunatokana na mechi za kirafiki za kimataifa za Fifa zilizofanyika mwezi Machi , ambazo matokeo yake ni sehemu ya kigezo. Tanzania, baada ya kutoka droo ya 1-1 na timu ya Malawi katika moja ya mechi hizo za kirafiki, imeshuka kutoka nafasi ya 100 mpaka ya 107. Nchi 10 bora katika viwango vya fifa ni 1. Ujerumani 2. Argentina 3. Belgium 4. Colombia 5. Brazil...

Like
412
0
Friday, 10 April 2015