Slider

TETESI ZA MAGAZETI YA NG’AMBO
Slider

TETESI ZA MAGAZETI: Klabu ya Manchester United ipotayari kuvunja rekodi ya usajili kwa kuweka mezani kitita cha paundi milioni 112 ili kumsajili beki wa kati wa klabu ya PSG MARQUINHOS. (Daily Mirror) Klabu ya Everton ipotayari kumpiga bei mshambuliaji wao KEVIN MIRALLAS katika dirisha hili la usajili. (Metro)  Klabu ya Chealsea ipotayari kumsajili mshambuliaji wa klabu ya Fiorentina JUAN CUADRADO endapo watafanikiwa kuwauza wakina MOHAMED SALAH  na ANDRE SCHURRLE. (Daily Mirror)  Kiungo wa klabu ya Manchester City JAMES MILNER amesema...

Like
322
0
Wednesday, 21 January 2015
VIONGOZI WA KANISA LA BAPTIST WAPIGWA NA KUTEKWA NYARA GUINEA
Global News

VIONGOZI watatu wa kanisa la Baptist nchini Guinea wamepigwa na kisha kutekwa nyara baada ya wenyeji kudhani kwamba  walikuwa  maafisa wanaohamasisha jamii dhidi ya ugonjwa wa Ebola . Viongozi hao walikuwa wametembelea kijiji cha kabac eneo la forecariah wakilenga kufukiza dawa ya wadudu kwenye kuta za vyoo vya umma  ikiwa ni sehemu pia ya kujipatia  huduma ya maji . Taarifa zimesema kuwa wanakijiji hao walipowaona waliwashuku kuwa wanataka kueneza ugonjwa wa ebola  katika eneo hilo ....

Like
242
0
Wednesday, 21 January 2015
11 WAUAWA DRC KUFUATIA MSWADA TATANISHI WA UCHAGUZI
Global News

SERIKALI ya Jamhuri ya kidemokrasi ya Congo, DRC ,imesema  kwamba takriban watu 11 wakiwemo raia wameuawa mjini Kinshasa tangu vurugu zilizosababishwa na mswada tatanishi wa uchaguzi kuanza Jumatatu. Msemaji wa Serikali, Bwna Lambert Mende amesema Mswada huo umetajwa na wanasiasa wa upinzani kama mapinduzi ya kikatiba wakisema utamfanya Kabila kujiongeza muda madarakani kwa miaka mingine mitatu. Mswada huo unajadiliwa na baraza la seneti huku viongozi wa upinzani wakiitisha maandamano mengine hii leo kuupinga mswada huo.    ...

Like
342
0
Wednesday, 21 January 2015
KAMATI KUU YA CHADEMA KUKUTANA KESHO
Local News

CHAMA cha Demokrasia na Maendeleo- CHADEMA, kimeitisha Kikao cha Kamati kuu kitakachofanyika kesho ambacho kitatoa maazimio na maamuzi ya chama kuhusu maswala mbalimbali kwa mustakabali wa wananchi kwa ujumla. Akizungumza na Wandishi wa habari leo Jijini Dar es salaam, Afisa habari wa chama hicho Tumaini Makene, amesema kikao hicho pia kitajadili zoezi la uandikishwaji wa Daftari kudumu la wapiga kura. Hata hivyo Makene amesema swala la Elimu ya Katiba pendekezwa ikiwemo elimu ya kura ya maoni na Taarifa ya Ukawa...

Like
237
0
Wednesday, 21 January 2015
VIJANA NCHINI WAMETAKIWA KUJITAMBUA NA KUACHA KUTUMIWA NA WANASIASA
Local News

VIJANA nchini wametakiwa kujitambua na kuacha kutumiwa na baadhi ya wanasiasa kuwa mtaji wao wa mafanikio katika kuelekea uchaguzi mkuu wa mwaka huu kutokana na kubainika kuwa idadi yao ni kubwa zaidi. Askofu wa Kanisa la Anglikana Jimbo la Dar es Salaam, Dokta Valentino Mokiwa amesema kwa mujibu wa taarifa ya  Mkurugenzi Mkuu wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu, Dokta  Albina Chuwa,  Sensa ya Watu na Makazi ya mwaka 2012, inaonyesha kuwa vijana ni asilimia 34.7 ya watu wote nchini,...

Like
264
0
Wednesday, 21 January 2015
CRISTIANO RONALDO AMWAGANA NA SHAYK
Slider

Mchezaji bora wa dunia Cristiano Ronaldo na mwanamitindo wa Urusi Irina Shayk wameripotiwa kuachana baada ya miaka mitano ya mahusiano yao. Tetesi hizo zilianza kusambaa mara baada ya Shyk kukosa kuhudhuria kwenye sherehe za kutoa tuzo za mchezaji bora duniani wiki iliyopita na utata ulikuja zaidi pale muwakilishi wa mwanamitindo Shayk kuzungumza na waandishi wa habari huko marekani na kuweka wazi kuwa wawili hao hawapo pamoja tena Mwanamitindo huyo mwenye umri wa miaka 29 alijizolea umaarufu zaidi duniani baada ya...

Like
280
0
Wednesday, 21 January 2015
KAMANDA WA KUNDI LA LRA KUFIKISHWA ICC
Global News

KIONGOZI wa ngazi za juu wa kundi la kigaidi la Uganda, Lord’s Resistance  Army, LRA amekabidhiwa kwa wawakilishi wa Mahakama  ya Kimataifa ya ICC, na sasa ameshawasili mjini The Hague ambako atafunguliwa kesi. Kiongozi huyo Dominic Ongwen atakabiliwa na mashtaka ya uhalifu  wa kivita na uhalifu dhidi ya binadamu. Kundi la kigaidi la LRA kwa muda mrefu limekuwa linafanya vitendo vya kinyama katika nchi za  Afrika mashariki na kati. Ongwen alijisalimisha mwenyewe kwa majeshi ya Marekani katika  Jamhuri ya Afrika...

Like
264
0
Wednesday, 21 January 2015
OBAMA ALIHUTUBIA TAIFA LA MAREKANI
Global News

RAIS Barack Obama amesema  harakati za kupambana na magaidi wa dola la Kiislamu zitahitaji muda, lakini zitafanikiwa. Obama ameahidi hayo katika hotuba, juu ya hali ya nchi  inayotolewa na Rais kila mwaka nchini Marekani ambapo katika hotuba  hiyo, Rais Obama amelitaka Bunge la nchi yake lipitishe azimio la kuiruhusu Marekani itumie nguvu za kijeshi dhidi ya dola la kiislamu. Rais huyo ameeleza kuwa uongozi wa Marekani katika harakati za kupambana na dola  la kiislamu umewazuia wapiganaji  wa kundi hilo kusonga...

Like
252
0
Wednesday, 21 January 2015
KAMATI YA BUNGE YA KILIMO, MIFUGO NA MAJI YARIDHISHWA NA MAFANIKIO YA MIRADI YA MAJI RUFIJI MKOANI PWANI
Local News

KAMATI ya Bunge ya Kilimo, Mifugo na Maji imeeleza kuridhishwa na maendeleo ya utekelezaji wa miradi ya maji ya Kibiti na Ikwiriri iliyopo wilayani Rufiji mkoani Pwani kutokana na kuonesha mafanikio makubwa. Hayo yamesemwa na Kiongozi wa Wajumbe wa Kamati hiyo Amina Makilagi, Mbunge, baada ya kukagua miradi hiyo ikiwa ni sehemu ya ziara ya ukaguzi wa miradi ya maji Tanzania Bara inayofanywa na baadhi ya wajumbe wa kamati katika mikoa ya Pwani, Lindi na Mtwara. Mradi wa Kibiti wenye...

Like
482
0
Wednesday, 21 January 2015
WAZIRI WA MAJI AMPA MKANDARASI SIKU 90 KWA MKANDARASI WA MEGHA ENGINEERING INFRASTRUCTURE LIMITED
Local News

WAZIRI wa maji Jumanne Maghembe ametoa siku 90, kwa mkandarasi Megha Engineering Infrastructure Limited anaesambaza bomba la maji mradi wa Mlandizi Kimara kufanikisha mradi huo na kupeleka ripoti ya maradi kwenye Mamlaka ya maji safi na maji taka (Dawasco), kwalengo la kupata tathimini ya mradi. Ametoa agizo hilo jana akiwa mkoani Pwani wakati akikagua miradi minne ya Dawasco, yakusambaza maji Ruvu juu na Ruvu Chini kufikisha Jijini Dar es Salaam. Aidha amemwagiza Mkurugenzi Mkuu wa DAWASA Arcado Mutalemwa kuhakikisha pampu...

Like
509
0
Wednesday, 21 January 2015
KATANGA ATEULIWA KUWA AFISA HABARI WA DRFA
Slider

Chama cha soka mkoa wa Dar es salaam DRFA jana kilimtangaza Mwandishi na mtangazaji wa Habari za michezo kutoka kwenye kituo hiki cha EFM kwenye dawati la michezo la E sport Omary Katanga kuwa msemaji Mpya wa chama hicho. Katanga anachukuwa nafasi iliyokuwa ikishikiliwa na Mohamed Mharizo ambae amekubaliana na uongozi kuachia nafasi hiyo. Katanga maarufu kama mlinda mlango namba moja ulimwenguni anawika katika medali ya utangazaji wa habari za kimichezo katika kipindi cha Esport,kinachoruka kila siku sa moja hadi saa...

Like
399
0
Wednesday, 21 January 2015