SHIRIKA la Umoja wa Mataifa linaloshughulkia wakimbizi limehofu kuwa huenda wakimbizi 500 wamefariki kwenye bahari ya Mediterania walipokuwa njiani kuelekea Italia. Hata hivyo msemaji wa shirika hilo amewaambia waandishi wa habari kwamba haijulikani ni lini wakimbizi hao wamefariki lakini amesema wachunguzi wanawahoji wakimbizi 41 walionusurika. Umoja wa Mataifa umebaisha kwamba miongoni mwa watu waliookolewa walikuwa wakimbizi kutoka Somalia, Ethiopia, Misri na...
POLISI nchini Zambia wamesema watu wawili wamechomwa moto mjini Lusaka katika vurugu ya ubaguzi wa wenyeji dhidi ya wageni. Watu Zaidi ya 250 wamekamatwa baada ya maduka mengi yanayomilikiwa na wanyarwanda kuvamiwa. Uvamizi huo umetokea baada ya wanyarwanda hao kushutumiwa kuua watu na kutumia viungo vyao kuvutia wateja....
MANISPAA ya Ilala Jijini Dar es salaam imemvua madaraka mkuu wa Idara ya ujenzi mhandisi Japhery Bwigane na wasaidizi wake wawili kwa tuhuma za kusimamia ujenzi wa barabara za manispaa hiyo kujengwa chini ya kiwango. Akizungumza na waandishi wa Habari wakati akitoa taarifa hiyo, Mstahiki Meya wa Manispaa ya Ilala Charles Kuyeko amewataja maofisa wengine wa idara hiyo waliosimamishwa kuwa ni Siajali Mahili na Daniel Kirigiti ambao wamehamishwa idara hiyo ili kupisha uchunguzi. Kuyeko amesema baraza la madiwani...
MADAKTARI Bingwa wa Upasuaji kutoka Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) kwa kushirikiana na timu ya Madaktari wanne kutoka nchini Hispania wameendesha zoezi la upasuaji wa masikio, pua, pamoja na upasuaji wa shingo na kichwa. Akizungumzia kuhusu zoezi hilo Daktari Bingwa wa magonjwa ya masikio, Pua na koo Martin Mushi amesema katika upasuaji huo madaktari hao wanatumia teknolojia kubwa na ya kisasa zaidi ambapo pamoja na mambo mengine ujio wao utawawezesha madaktari wa Muhimbili kujifunza zaidi matumizi ya teknolojia mpya ya upasuaji....
Ligi kuu ya England inatarajiwa kuendelea tena wikiendi hii kwa michezo kadhaa, Jumamosi Norwich itaikaribisha Sunderland, Everton wao watakuwa wenyeji wa Southampton, Man Utd watakuwa wenyeji wa Aston Villa katika dimba la Old Traford , Newcastlle itamenyana na Swansea city, West Brom watawaalika Watford na Chelsea watakuwa darajani Stamford dhidi ya Manchester City. Jumapili Vinara wa ligi Leicester city watakuwa nyumbani na West Ham,Bournemouthwatawaalika Liverpool na Arsenal itamenyana na Crystal...
MAHAKAMA ya juu zaidi nchini Brazil imekataa ombi la serikali la kutaka kutupiliwa mbali kura ya bunge kuamua ikiwa rais Dilma Rousseff ataondolewa madarakani. Mahakama imekataa kufuta amri ya kupiga kura iliyoamuliwa na spika wa bunge la chini, ambayo itaamua siku ya Jumapili ikiwa Rousseff ataondolewa madarakani au la. Wafuasi wa rais huyo, walikuwa wamedai kuwa zoezi hilo litavurugwa kwa sababu wabunge kutoka majimbo yanayompinga Rousseff huenda wakapiga kura kwanza. Bi Rousseff amelaumiwa kwa kuvuruga bajeti kabla ya uchaguzi wa...
KOREA Kaskazini imefanya jaribio la kufyatua kombora katika pwani yake ya mashariki, lakini dalili zinaonesha jaribio hilo halikufanikiwa, kwa mujibu wa maafisa wa Marekani na Korea Kusini. Bado haijabainika roketi iliyotumiwa ilikuwa ya aina gani lakini inadhaniwa majaribio hayo yalikuwa ya kombora la masafa ya wastani kwa jina “Musudan” ambalo taifa hilo lilikuwa halijalifanyia majaribio. Shughuli hiyo ilikuwa ikifanyika siku ambayo ni ya kuadhimisha siku ya kuzaliwa kwa mwanzilishi wa taifa la Korea Kaskazini Kim...
IMEELEZWA kuwa endapo sekta ya viwanda itasimamiwa na kuwekewa mazingira bora, ina nafasi kubwa ya kuleta mabadaliko na kuweza kuharakisha ukuaji wa uchumi na kuliwezesha Taifa kufika pale linapokusudia kufika kama inavyoainishwa na dira ya Taifa ya maendeleo ya mwaka 2025. Hayo yamesemwa na Mkurugenzi wa REPOA Dokta Donald Mmari katika mahojiano maalum na Efm juu ya namna sekta ya viwanda inavyoweza kutumika kuleta mageuzi ya kiuchumi yanayoenda sanjari na mabadiliko ya mtu mmoja mmoja. Dokta Mmari amesema kuwa licha...
RAIS wa Sudan Kusini Salva Kiir ambaye amewasili nchini leo, anatarajiwa kutia saini mkataba wa kuiingiza rasmi nchi hiyo kwenye Jumuiya ya Afrika Mashariki. Rais Kiir atatia saini mkataba huo jijini Dar es Salaam mbele ya mwenyeji wake, Rais wa Tanzania John Magufuli, ambaye kwa sasa ndiye mwenyekiti wa jumuiya hiyo. Sudan Kusini itakuwa nchi ya sita kujiunga na jumuiya hiyo iliyoanza kwa nchi tatu Tanzania, Kenya na Uganda. Rwanda na Burundi zilijiunga na jumuiya hiyo...
Gwiji la soka toka Ivory Coast na nyota wa zamani wa klabu ya Chelsea Didier Drogba amesema atachukua hatua za kisheria dhidi ya gazeti la Daily Mail. Hii ni baada ya gazeti hilo kuchapisha habari zinazodai kuwa kati ya pesa anazokusanya kupitia wakfu wake wa kusaidia jamii, ni chini ya asilimia moja ndizo zinazotumika kusaidia jamii. Gazeti hilo limesema ni £14,115 pekee kati ya £1.7m zinazotolewa na wachezaji nyota na wafanyabiashara ambazo husaidia watoto Afrika. Drogba, 38, ametoa taarifa...
Mmoja wa nyota wa mpira wa vikapu duniani Kobe Bryant, amecheza mechi yake ya mwisho ya kulipwa nchini Marekani. Mchezo huo utafikisha kikomo uchezaji wake wa zaidi ya miongo miwili ambapo Bryant amekuwa wa tatu kwa kuandikisha alama nyingi zaidi katika historia ya mchezo huo. Alishinda mataji matano ya NBA akiwa na LA Lakers ambao amewachezea muda wote huo. Lakini mwandishi mmoja wa BBC anasema Bryant hajaenziwa kwa njia sawa na mashabiki. Wakati mwingine alikuwa hachezaji vyema na mara kwa...