Slider

NETANYAHU AMTUHUMU BAN KI-MOON KUUNGA MKONO UGAIDI
Global News

WAZIRI mkuu wa Israel, Benjamin Netanyau amemshutumu katibu mkuu wa umoja wa mataifa, Ban Ki-Moon kwa kuunga mkono ugaidi, baada ya kusema kuwa ni jambo la kawaida kwa watu wanaotawaliwa au kukandamizwa, kukabiliana na walowezi. Hayo yamejiri kufuatia Zaidi ya Wapalestina 155, Waisraeli 28, Mmarekani na Raia wa Eritrea kuuawa kwa kushambuliwa kwa risasi na visu tangu mwezi Oktoba mwaka jana. Akihutubia Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa, Ban amesema visa hivyo vimeongezeka kutokana na sababu mbalimbali zilizojitokeza miongoni...

Like
173
0
Wednesday, 27 January 2016
WATANZANIA WATAKIWA KUJENGA UTAMADUNI WA KUSOMA VITABU
Local News

WATANZANIA wametakiwa kujenga utamaduni wa kusoma vitabu ili kukuza uwezo wa ufahamu na kuongeza ujuzi katika utendaji kazi wao wa kila siku. Wito huo umetolewa jana na Waziri wa Elimu, Sayansi,Teknolojia na Ufundi Profesa Joice Ndalichako kwa niaba ya Rais dokta John Pombe Magufuli katika ufunguzi wa Maonesho ya vitabu yanayofanyika katika meli ya Logos Hope inayozunguka katika maeneo mbali mbali duniani kuhamasisha usomaji wa vitabu. Profesa Ndalichako amewataka Walimu na wakufunzi wa shule na vyuo nchini kutembelea katika meli...

Like
250
0
Wednesday, 27 January 2016
SERIKALI YASISITIZA KUTENDA HAKI KWA VIONGOZI WANAORUHUSIWA KUJIHUSISHA NA SIASA
Local News

SERIKALI imesisitiza kuwa ipo makini kuhakikisha kuwa kila kiongozi anayeruhusiwa kujihusisha na masuala ya kisiasa anapata haki yake bila usumbufu wowote. Hayo yamesemwa leo Bungeni mjini Dodoma na Waziri wa nchi Ofisi ya rais, Utumishi na Utawala bora Mheshimiwa Angela Kairuki wakati akijibu swali la mheshimiwa Hafidhi Ali Tahir Mbunge aliyetaka kufahamu utaratibu wa serikali juu ya watumishi hao. Mheshimiwa Kairuki amesema kuwa watumishi ambao hawaruhusiwi kujihusisha na masuala ya kisiasa ni pamoja na Wanajeshi wa Jeshi la wananchi wa...

Like
178
0
Wednesday, 27 January 2016
MAHAKAMA AFRIKA YA KATI YAFUTA MATOKEO YA UBUNGE
Global News

MAHAKAMA ya kikatiba nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati imefuta matokeo yote ya uchaguzi wa ubunge kutokana na kasoro nyingi zilizojitokeza wakati wa uchaguzi. Mbali na hayo Mahakama hiyo pia imeidhinisha matokeo ya uchaguzi wa urais, ambao ulifanyika katika kipindi cha mwezi mmoja uliopita.   Hata hivyo imethibitisha kwamba mawaziri wakuu wa zamani Anicet- Dologuele na Faustin Touadere watakutana kwenye duru ya pili ya uchaguzi Februari 7 mwaka...

Like
166
0
Tuesday, 26 January 2016
PAPA FRANCIS AOMBA RADHI WAUMINI WA KIPROTESTANTI
Global News

IKIWA ni hatua ya kujumuisha umoja wa kikristo duniani, Kiongozi mkuu wa Kanisa katoliki Ulimwenguni, Papa Francis amewaomba radhi waumini wa Kiprotestanti kutokana na unyanyasaji walioupata kutoka kanisa Katoliki miaka iliyopita. Papa Francis amewataka waumini wa kanisa Katoliki pia kuwasamehe wale ambao waliwakosea ili wasiruhusu makosa yaliyotendeka kuwa sumu ya mahusiano ya sasa. Kufuatia tamko hilo msemaji wa Vatcan ametangaza kuwa Papa Francis atazuru mji wa Lund uliopo Swedish eneo ambalo jumuiya ya Kilutheri ilianzishwa na kuanzisha...

Like
233
0
Tuesday, 26 January 2016
HALMASHAURI YA MANISPAA YA ILALA YAPEWA MWEZI MMOJA KUBOMOA JENGO REFU KATIKA MTAA WA INDIRAGHANDI
Local News

WAZIRI wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi mheshimiwa William Lukuvi amewaagiza watendaji wa Halmashauri ya Manispaa ya Ilala na shirika la Nyumba la Taifa kubomoa jengo refu lililojengwa chini ya kiwango katika mtaa wa Indiraghandi ndani ya kipindi cha mwezi mmoja kuanzia jana. Lukuvi ametoa kauli hiyo Jijini Dar es salaam kabla ya kuelekea kwenye ziara fupi ya kikazi wilayani Bagamoyo mkoani Pwani ambapo huko pia amebaini matatizo mbalimbali katika sekta ya Ardhi. Miongoni mwa changamoto alizozikuta ni pamoja...

Like
312
0
Tuesday, 26 January 2016
BUNGE LA 11 LAANZA KUJADILI HOTUBA YA RAIS
Local News

MKUTANO wa pili wa Bunge la 11 umeanza leo mjini Dodoma ambapo Bunge la Jamhuri ya Muungano linajadili hotuba ya Rais kwa muda wa siku tatu aliyoitoa wakati wa ufunguzi wa Bunge hilo. Kikao cha kwanza cha Bunge hilo kimeanza kwa kipindi cha maswali na majibu ambapo baadhi ya wabunge wamepata nafasi ya kuiuliza maswali serikali na kuhoji mikakati mbalimbali inayotarajiwa kufanywa kwa manufaa ya Taifa. Awali kabla ya kipindi cha maswali na majibu kuanza, Spika wa Bunge mheshimiwa Job...

Like
244
0
Tuesday, 26 January 2016
TEMEKE: SEKTA YA UHANDISI IMETAKIWA KUANDAA MIRADI INAYOTEKELEZEKA
Local News

MSTAHIKI MEYA wa Manispaa ya Temeke Abdallah Chaurembo ameitaka sekta ya uhandisi pamoja na Watendaji wa Manispaa hiyo kuandaa miradi michache inayotekelezeka na kuwasilisha katika kamati ya maendeleo ya manispaa hiyo badala ya kuwa na miradi mingi isiyotekelezeka. Chaurembo ameyasema hayo alipokuwa akizungumza na Waandishi wa habari baada ya kufanya ziara ya ukaguzi wa miradi ya maendeleo na kubaini kuwa miradi mingi haijakamilika kutokana na sababu mbali mbali ikiwemo ufinyu wa bajeti. Aidha Chaurembo amewataka Wahandisi na Watendaji hao...

Like
226
0
Monday, 25 January 2016
WAUMINI NCHINI WAASWA KULINDA AMANI
Local News

WAUMINI wa dini zote nchini wameaswa kutojihusisha na vitendo vya kupeana majina mabaya yanayo hamasisha vurugu au uvunjifu wa amani. Wito huo umetolewa Jijini Dar es salaam na Mmoja wa Viongozi wa Kuu wa kiroho wa Waislamu Dhehebu la Shia Ithina Sheria Tanznia Sheikh Hemed Jalala alipokuwa akizungumza kwenye semina ya kujadili changamoto zinazo wakabili umma wa kiislamu nchini na duniani kwa ujumla. Sheikh JALALA amebainisha kuwa kuitana majina hayo ndio chanzo kikubwa cha kuibuka kwa vitendo vya kigaidi vinavyo...

Like
204
0
Monday, 25 January 2016
RAIS WA MYNAMAR AAMURU WAFUNGWA 101 KUACHIWA HURU
Global News

RAIS wa Myanmar anayemaliza muda wake, Thein Sein, ameamuru kuachiwa huru kwa wafungwa 101 wakiwemo takribani 25 waliohukumiwa kwa makosa ya kisiasa.   Maafisa nchini humo wamesema msamaha huo unawahusu pia wafungwa 77 waliokuwa wamehukumiwa kifo na adhabu yao kubadilishwa kuwa kifungo cha maisha.   Kwa mujibu wa chama cha wafungwa wa kisiasa  nchini humo, miongoni mwa wafungwa 25 wa kisiasa, yumo raia wa New Zealand, Philip Blackwood, ambaye alihukumiwa mwezi Machi kwa kosa la kwenda kinyume na misingi ya...

Like
176
0
Friday, 22 January 2016
SOMALIA: WANAJESHI WA KENYA WALIPEWA TAHADHARI
Global News

IMEELEZWA kuwa Wanajeshi wa Kenya nchini Somalia walionywa kuhusu shambulizi la kundi la Alshabaab siku 45 kabla ya kundi hilo kuvamia mojawapo ya kambi zao. Jenerali Abas Ibrahim Guery ameiambia BBC kuwa , Kenya ilipewa ripoti ya kiintelijensia kuhusu tishio la uvamizi huo ambapo Wapiganaji hao wa kiislamu wanasema kuwa waliwaua zaidi ya wanajeshi 100 katika shambulio hilo likiwa ni baya zaidi kuwahi kufanyika kwa jeshi la Kenya. Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta amewatambelea baadhi ya wanajeshi waliojeruhiwa katika hospitali...

Like
229
0
Friday, 22 January 2016