Slider

MAKAA YA MAWE KUZALISHA UMEME TANZANIA
Local News

  SERIKALI imesema  itahakikisha  inafanya Makaa ya Mawe yanakuwa chanzo kingine kikubwa cha uzalishaji umeme Nchini.   Hayo yameelezwa na Waziri wa Nishati na Madini, Prof. Sospeter Muhongo alipotembelea  Mgodi wa Makaa ya Mawe wa Ngaka unaomilikiwa kwa ubia Kati ya Kampuni ya  TANCOAL na Serikali kupitia shirika la NDC.   Mgodi huo  upo katika Wilaya ya  Mbinga mkoani...

Like
255
0
Wednesday, 13 January 2016
GARISSA: WANAFUNZI WAREJEA CHUONI
Local News

WANAFUNZI wamerejea tena katika Chuo Kikuu cha Garissa na kuanza masomo miezi tisa baada ya chuo hicho kufungwa kutokana na shambulio la al-Shabab, Nchini Kenya. Serikali imesema imeweka usalama wa kutosha kuhakikisha kundi hilo kutoka Somalia haliwezi likashambulia tena, lakini licha ya hakikisho kutoka kwa maafisa wa usalama, ni wanafunzi wachache pekee waliorejea chuoni. Takriban wanafunzi 800 wa kufadhiliwa na serikali, waliokuwa wakisomea katika chuo hicho kabla ya shambulio kutokea, walihamishiwa chuo kikuu cha Moi mjini...

Like
176
0
Monday, 11 January 2016
CUF YAGOMA KURUDIA UCHAGUZI ZANZIBAR
Local News

WAKATI kesho ni maadhimisho ya miaka 52 ya Mapinduzi, Chama cha Wananchi –CUF, kimesema hakitakubali marudio ya uchaguzi wa urais visiwani Zanzibar. Taarifa ya chama hicho ambayo imesomwa leo na aliyekuwa mgombea wa urais wa CUF katika uchaguzi wa 25 Oktoba mwaka jana,  Maalim Seif  imeeleza kuwa hakuna hoja wala msingi wa kikatiba na kisheria wa uchaguzi  huo kurudiwa. Taarifa hiyo imeonyesha kutoa mapendekezo ya kuondolewa kwa mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi Zanzibar (ZEC) Jecha Salim...

Like
210
0
Monday, 11 January 2016
13,491 WAGUNDULIKA KUWA NA KIPINDUPINDU
Local News

JUMLA ya Watu elfu 13,491 wamegundulika kuwa na ugonjwa wa Kipindupindu tokea kuanza kwa ugonjwa huo Agosti 15 Mwaka jana na kuwa kati yao jumla ya watu 205 wameshafariki kwa ugonjwa huo.   Kwa mujibu wa Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mheshimiwa Ahmis Kigwangala, wiki iliyoaanza tarehe 4 hadi leo 11 Januari,  kumekuwa na jumla ya Wagonjwa 615 walioripotiwa nchini na vifo 3 hali inayoonyesha kuwa hali ya kipindupindu nchini bado sio nzuri....

Like
208
0
Monday, 11 January 2016
RAIS MAGUFULI AMTEMBELEA SUMAYE HOSPITALI
Local News

RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dokta. John Pombe Magufuli, amemtembelea na kumpa pole Waziri Mkuu Mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Frederick Sumaye leo, ambaye amelazwa katika Taasisi ya Jakaya Kikwete iliyopo katika Hospitali ya Taifa Muhimbili Jijini Dar es Salaam.   Mheshimiwa Frederick Sumaye alilazwa katika Taasisi hiyo siku nne zilizopita kwa matibabu ya moyo na madaktari wanaomtibu wamemhakikishia Rais Magufuli kuwa anaendelea vizuri ikilinganishwa na wakati alipofikishwa katika Taasisi hiyo.  ...

Like
336
0
Monday, 11 January 2016
UFARANSA YAWAKUMBUKA WALIOUAWA KIGAIDI PARIS
Global News

RAIS wa Ufaransa Francois Hollande na Meya wa mji wa Paris Anne Hidalgo waliweka bango la taarifa katika eneo la Place de la Republique kuwakumbuka watu 147 waliouawa katika mashambulizi ya kigaidi katika mji mkuu wa Ufaransa, Paris mnamo mwezi Novemba mwaka jana.   Rais Hollande aliungana na viongozi wengine na maelfu ya raia kuwakumbuka wahanga hao wa mashambulizi ya kigaidi ambayo kundi la wanamgambo wenye itikadi kali wa Dola la Kiislamu IS lilidai kuhusika.   Wiki nzima iliyopita, Ufaransa...

Like
168
0
Monday, 11 January 2016
MAKONDA AWEKA MAWE YA MSINGI YA UJENZI WA SHULE 2 ZA SEKONDARI KINONDONI
Local News

KATIKA kupunguza tatizo la watoto wengi wanaomaliza darasa la saba kushindwa kuendelea na elimu ya Sekondari kutokana na uhaba wa Madarasa wilayani Kinondoni , Mkuu wa Wilaya hiyo,  Paul Makonda leo ameweka mawe ya msingi ya ujenzi wa shule za Sekondari Mbezi Juu na shule ya Sekondari Mzimuni zinazojengwa katika manispaa ya Kinondoni.   Akizungumza na Waandishi wa habari pamoja na wananchi wakati akiweka mawe hayo ya msingi Makonda amesema hii ni sehemu yamkakati wa Manispaa hiyo kujenga shule za...

Like
633
0
Monday, 11 January 2016
SERIKALI KUWALINDA WANANCHI DHIDI YA MATUMIZI YA CHAKULA KISICHO SALAMA
Local News

SERIKALI imesema imejidhatiti kuwalinda wananchi kwa kuzuia athari za kiafya zinazoweza kujitokeza kutokana na matumizi ya chakula kisicho salama kote nchini.   Meneja Mawasiliano na Uhusiano wa Umma wa mamlaka ya chakula na Dawa (TFDA)  Gaudensia Simwanza ameyasema hayo  na kufafanua kuwa uchafuzi wa chakula hufanya chakula kisiwe salama na hivyo kusababisha madhara ya kiafya ya muda mfupi na muda mrefu na hata vifo kwa mlaji pamoja na athari za...

Like
287
0
Monday, 11 January 2016
NEW MUSIC: DREAM – NIMESHAZAMA
Entertanment

Baada ya kufnya vizuri na track yake ya kwanza kama  solo artist, Dream ameachia wimbo mpya unaweza kuusikiliza na kuupakua hapa Wimbo umetayarishwa na Abbah katika studio za Vipaji TZ pakua...

Like
532
0
Friday, 08 January 2016
WAPALESTINA WANNE WAUAWA UKINGO WA MAGHARIBI
Global News

JESHI la Israel limesema kwa Wapalestina wanne wameuawa kwa kupigwa risasi baada ya kujaribu kuwachoma visu wanajeshi wa Israel katika matukio mawili tofauti eneo la Ukingo wa Magharibi.   Watatu waliuawa katika makutano ya barabara ya Gush Etzion, ambako visa kama hivyo vimewahi kutokea awali na mwingine aliuawa karibu na Hebron lakini hakuna mwanajeshi aliyejeruhiwa.   Maafisa wa afya wa Palestina wamethibitisha vifo...

Like
166
0
Friday, 08 January 2016
SUDANI KUSINI: SALVA KIIR AOMBA RADHI RAIA
Global News

RAIS wa Sudan Kusini Salva Kiir kwa mara ya kwanza amewaomba radhi raia wa nchi hiyo kutokana na mateso na dhiki ambayo wamepitia wakati wa mzozo wa kisiasa uliodumu miaka miwili.   Rais  Kiir amesema kuomba msamaha ndiyo hatua ya kwanza katika kufanikisha maridhiano nchini humo.   Amechukua hatua hiyo wakati wa kufungua rasmi mkutano mkuu wa chama tawala cha SPLM. Jana, pande zilizohusika katika mzozo huo ziliafikiana kuhusu kugawana nyadhifa za uwaziri katika baraza la mawaziri la serikali ya...

Like
182
0
Friday, 08 January 2016