Slider

EFM YAKABIDHIWA MICHORO YA MADARASA KUTOKA KWA AFISA ELIMU, KINONDONI
Local News

Efm Radio,katika harakati zakufanikisha ahadi ya kujenga madarasa, imekabidhiwa michoro ya ramani ya madarasa ya sekondari wilaya ya Kinondoni kata ya Kimara, Makabidhiano yaliyofanyika  katika ofisi za Kituo hicho cha Utangazaji kupitia masafa ya 93.7 leo asubuhi. Mkurugenzi Mkuu wa Efm Radio, Francis Siza akipokea ramani ya michoro ya madarasa kutoka kwa Afisa elimu wa wilaya ya Kinondoni Bwana Rogers J. Shemwelekwa. Afisa elimu wa wilaya ya Kinondoni Bw. Rogers J. Shemwelekwa katika picha ya pamoja na uongozi wa Efm...

Like
716
0
Monday, 01 February 2016
70 WAUAWA KWA MABOMU SYRIA
Global News

WATU zaidi ya  70 wameuawa kutokana na mashambulio  ya mabomu ambayo kundi la magaidi wanaoitwa Dola  la  Kiislamu limedai kuyafanya karibu  na sehemu takatifu ya Washia nje ya mji mkuu wa Syria, Damascus.   Kwa mujibu  wa  taarifa  iliyotolewa  na kituo kilichopo mjini London, kinachofuatilia haki za binadamu nchini  Syria, watu  hao waliuawa kutokana  na miripuko miwili ya mabomu karibu na  sehemu hiyo takatifu, Sayyida Zeinab.   Watoto kadhaa walikuwamo miongoni mwa walioangamizwa huku Watu wengine zaidi ya 100...

Like
355
0
Monday, 01 February 2016
NIGERIA YAOMBA MKOPO WA DHARURA
Global News

NIGERIA imeomba mkopo wa dharura wa jumla ya dola bilioni tatu na nusu kutoka Benki ya Dunia ili kujaribu kuziba pengo kwenye bajeti yake. Uchumi wa Nigeria umeathiriwa sana na kushuka kwa bei ya mafuta duniani. Waziri wa fedha nchini humo Kemi Adeosun amesema amekuwa akifanya mazungumzo na maafisa wa Benki ya Dunia. Hata hivyo, hatua ya Nigeria kuomba mkopo wa dharura inashangaza ikizingatiwa kwamba siku chache zilizopita Shirika la Fedha Duniani (IMF) lilisema haihitaji usaidizi wa...

Like
254
0
Monday, 01 February 2016
MACHAFUKO BURUNDI: RAIA 126000 WAKIMBILIA TANZANIA
Local News

IMEELEZWA kuwa zaidi ya raia laki 126,000 wa Burundi wamekimbilia nchini Tanzania tangu mwezi Aprili, 2015, kufuatia machafuko ya kisiasa nchini humo. Huku tayari wakimbizi  elfu 64,000 kutoka Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo (DRC) wakiwa tayari nchini. Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon  ametoa dola za Marekani milioni 100, sawa na shilingi za Tanzania bilioni 220 kutoka katika Mfuko Mkuu wa Kushughulikia Dharura wa Umoja wa Mataifa -CERF kwa shughuli za misaada katika maeneo tisa yenye dharura duniani...

Like
223
0
Monday, 01 February 2016
RAIS MAGUFULI ASIKITISHWA NA KIFO CHA RUBANI MUINGEREZA ALIYEUAWA NA MAJANGILI
Local News

RAIS wa Jamhuri ya Mmuungano wa Tanzania Dokta  John Pombe Magufuli amesema amesikitishwa na kitendo cha kuuawa kwa rubani Mwingereza aliyekuwa akisaidiana na maafisa wa Tanzania kupambana na ujangili. Rubani wa helkopta Kapteni Roger Gower, alifariki baada ya majangili kuifyatulia risasi na kuidondosha helkopta aliyokuwa akiiendesha wakati alipoungana na askari wanyamapori waliokuwa wakikabiliana na majangili katika pori la akiba lililopo katika wilaya ya Meatu Mkoani Simiyu. Askari mmoja wa Tanzania alijeruhiwa wakati wa tukio hilo ambapo...

Like
275
0
Monday, 01 February 2016
MAKABURI YA WATU WENGI YAGUNDULIKA BURUNDI
Global News

SHIRIKA la Kimataifa la kutetea haki za binadamu la Amnesty International limesema limeona picha za setilite zinazoonyesha mamia ya raia wa Burundi kuuawa na baadae kuzikwa katika kaburi la watu wengi. Amnesty limesema sehemu za picha hizo zinaonyesha makaburi ya watu wengi yapatayo matano katika eneo la Buringa viungani mwa mji mkuu wa Bujumbura. Shirika hilo limeongeza kuwa uchunguzi wao wa kitaalamu unafanana na ule ambao wameupata kutoka kwa mashahidi kuwa kuna makaburi mengine ya pamoja ya watu waliouwawa siku...

Like
181
0
Friday, 29 January 2016
MAOMBI YA RUHUSA YA KUTOA MIMBA KWA WENYE ZIKA YATUMWA BRAZIL
Global News

KUNDI la mawakili, wanaharakati na wanasayansi nchini Brazil limewasilisha ombi kwa mahakama ya juu nchini humo likitaka wanawake wenye virusi vya Zika waruhusiwe kutoa mimba. Virusi vya Zika vinaaminika kusababisha watoto kuzaliwa wakiwa na vichwa vidogo, na kudumaza ubongo. Utoaji mimba nchini Brazil hauruhusiwi kisheria, ila tu wakati wa dharura ya kiafya au iwapo mimba imetokana na ubakaji hali ambayo kwa Kiingereza inajulikana kama...

Like
211
0
Friday, 29 January 2016
KIWANDA CHA KUZALISHA MBOLEA KUNZISHWA LINDI
Local News

SHIRILA la maendeleo ya mafuta na petrol Tanzania (TPDC) kwa kushrikiana na kampuni tatu wanatarajia kuanzisha kiwanda cha kuzalisha mbolea katika wilaya ya kilwa mkoani lindi. Akizungunza wakati wa semina ya siku mbili ya kuwajengea uwezo waandishi wa habari kuhusu uelewa wa sekta ndogo ya mafuta na gesi mkurugenzi wa mkondo wa chini kutoka TPDC dokta Wellington Hudson amezitaja baadhi ya kampuni watakazoshirikiana nazo katika ujenzi wa kiwanda hicho kuwa ni pamoja na kampuni ya ferostar ya Ujerumani na haldo...

Like
345
0
Friday, 29 January 2016
SERIKALI YAAHIDI KUWAWEZESHA WAVUVI WADOGO
Local News

SERIKALI imewahakikishia wananchi hususani wavuvi wadogo kuwa itahakikisha inawawezesha wavuvi hao kufanya shughuli zao za uvuvi kwa manufaa ili kujiletea maendeleo yao pamoja na Taifa kwa ujumla. Hayo yamebainishwa leo Bungeni Mjini Dodoma na Waziri wa Kilimo, Mifugo na Uvuvi mheshimiwa Mwigulu Nchemba wakati akijibu swali la mbunge wa Jimbo la Mwibara mheshimiwa Kangi Lugola aliyetaka kufahamu jitihada za serikali katika kuwanufaisha wavuvi. Katika majibu ya swali hilo pia mheshimiwa Nchemba amewataka watu wenye dhamana ya kusimamia shughuli...

Like
159
0
Friday, 29 January 2016
KENYA: WAWILI WAPANDISHWA KIZIMBANI KUJIBU MASHTAKA YA MAUAJI
Global News

MAHAKAMA Kuu mjini Mombasa imeamua kwamba washukiwa wawili walioshitakiwa kwa mauaji ya watu 60 eneo la Mpeketoni miaka miwili iliyopita wana kesi ya kujibu. Jaji Martin Muya amesema upande wa mashitaka uliwasilisha ushahidi wa kutosha kuwafungulia mashitaka wawili hao. Diana Salim Suleiman na Mahadi Suleiman Mahadi ajulikanaye kama Jesus wanadaiwa kuhusika katika uvamizi uliopelekea kuuawa kwa watu 60 mwezi Juni mwaka 2014 katika vijiji vya Mpeketoni na Kaisairi, Kaunti ya Lamu.nchini Kenya....

Like
167
0
Thursday, 28 January 2016
UFISADI: WAZIRI WA UCHUMI JAPAN AJIUZULU
Global News

WAZIRI wa uchumi nchini Japan Akira Amari amejiuzulu kutokana na madai ya ufisadi yaliyokuwa yakimkabili. Bwana Amari ametoa tangazo hilo ghafla katika mkutano na waandishi wa habari jana ambapo mbali na hayo amekanusha kupokea hongo kutoka kwa kampuni moja ya ujenzi kama ilivyodaiwa na jarida moja la Japan. Hatua hiyo imechukuliwa kama pigo kubwa kwa waziri mkuu Shinzo Abe kwani Amari alitarajiwa kusafiri hadi New Zealand wiki ijayo kusaini mkataba wa ushirikiano kati ya mataifa ya ng’ambo ya pili ya...

Like
195
0
Thursday, 28 January 2016