Local News

PRO. TIBAIJUKA: KAMWE SITAJIUZULU
Local News

WAZIRI wa Ardhi nyumba na maendeleo ya Makazi Mhe Profesa Anna Tibaijuka amesema kamwe hawezi kujiuzulu kutokana na kashfa ya Escrow kwa kuwa hausiki na wizi wa fedha hizo na kusema kuwa kama akijiuzulu atakuwa hatendei haki dhana ya kuchakalika ili kuleta maendeleo. Akizungumza na Waandishi wa habari jijini dare s salaam Tibaijuka amesema kuwa fedha aliyoipokea ni mchango wa shule katika taasisi ya Shirika la JOHA TRUST wa shilingi Bilioni moja milioni mia 6 kumi na saba na laki...

Like
369
0
Thursday, 18 December 2014
SERIKALI YAPITISHA AZIMIO LA KINGA YA JAMII
Local News

SERIKALI ya Tanzania imepitisha Azimio linalohusu Kinga ya Jamii lenye msingi imara wa kusimamia masuala hayo nchini na Afrika kwa ujumla ili kuwa na maendeleo halisi kwa watu wake.   Azimio hilo limepitishwa na kusainiwa na Waziri wa Fedha Saada Mkuya Salum kwa niaba ya Serikali jijini Arusha wakati wa kufunga kongamano la kimataifa la siku tatu kuhusu Kinga ya Jamii ambalo limeshirikisha wajumbe kutoka nchi mbalimbali za Afrika na nje ya Afrika.   Akitoa hotuba ya kufunga kongamano hilo...

Like
256
0
Thursday, 18 December 2014
MAONYESHO YA KITAIFA YA ELIMU YAFUNGULIWA RASMI
Local News

WAZIRI wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi Dokta Shukuru Kawambwa amesema kuwa Maonyesho ya Kitaifa ya Elimu –TIEE yatasaidia kuangalia namna ya kuisukuma ajenda ya elimu nchini.   Dokta Kawambwa ameyasema hayo leo wakati akifunguwa rasmi Maonyesho ya siku saba ya Elimu kwenye Viwanja vya Mwalimu Nyerere jijini Dar es salaam.   Maonyesho hayo ya siku saba yanayohusisha zaidi ya kampuni 80 za Elimu, Wadau, Taasisi na Walimu yamelenga kutengeneza jukwaa moja la kutoa taarifa za Elimu na Taasisi zake...

Like
249
0
Thursday, 18 December 2014
RAIS AMTEUA DK. MATARAGIO KUWA MKURUGENZI MTENDAJI WA TPDC
Local News

RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete, amemteua Dokta James Mataragio kuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania -TPDC.   Kulingana na, Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi Ombeni Sefue uteuzi huo ulianza tarehe 15 Desemba, 2014.   Dokta Mataragio ni Mtanzania ambaye hivi sasa anaishi na kufanya kazi nchini Marekani akiwa Senior Geoscientist wa Kampuni ya Bell Geospace, Houston, Marekani.   Aidha, Dokta Mataragio pia ni mmoja wa wataalam wa sekta ya madini, mafuta...

Like
310
0
Thursday, 18 December 2014
KINANA: WAMASAI NI WATANZANIA HALALI
Local News

KATIBU MKUU wa Chama Cha Mapinduzi-CCM ABDULRAHMAN KINANA amesema kuwa watu wa Kabila la Wamasai ni watanzania halali na kwamba hawana sababu ya kutafuta Uraia kwenye Maeneo mengine. Kinana ameeleza kuwa tatizo la migogoro ya ardhi ikiwa ni pamoja na Wafugaji kuingia kwenye mapori ya Akiba na Hifadhi za Taifa haliwahusu Wamasai pekee bali ni la nchi nzima. Kiongozi huyo wa chama cha Mapinduzi, ametoa kauli hiyo wakati akijibu Malalamiko yaliyotolewa na viongozi wa Mila wa Kabila la Wamasai katika...

Like
973
0
Thursday, 18 December 2014
WALIOFAULU MTIHANI WA DARASA LA SABA KUPANGIWA SHULE
Local News

WANAFUNZI waliofaulu mtihani wa darasa la Saba wanatarajiwa kupangiwa shule kuendelea na Elimu ya Sekondary muda wowote kuanzia leo. Habari za kuaminika zimeeleza kuwa majina ya Wanafunzi na shule walizopangiwa yatatangazwa leo ikiwa ni maandalizi ya kuanza kidato cha kwanza mwakani. Wanafunzi laki nane na elfu nane mia moja kumi na moja wa shule za msingi nchini wamefanya mtihani wa kumaliza darasa la Saba September 9 mwaka huu idadi ambayo ni pungufu kulinganisha na waliomaliza mwaka jana ambao walikuwa 844,938....

29
11719
0
Thursday, 18 December 2014
VODACOM YATANGAZA KUMPATA MSHINDI WA APPSTAR
Local News

KAMPUNI ya simu za Mkononi ya Vodacom, imetangaza kumpata mshindi bora wa ubunifu wa program za simu kupitia shindano la AppStar linaloendeshwa na Kampuni hiyo. Kwa Mujibu wa Meneja Uhusiano wa Nje wa Vodacom Tanzania, Abigail Ambweni, kupitia program hiyo Mshindi wa kwanza atakwenda India kushiriki katika ngazi ya kimataifa.  Mshindi kuyo ni Roman Mbwasi ambaye ameibuka kidedea katika shindano la kutafuta vipaji vya ugunduzi wa program za simu la AppyStar lililoandaliwa na kampuni ya mawasiliano ya Vodacom Tanzania likiwa...

Like
283
0
Wednesday, 17 December 2014
JUNIOR ARCHIEVEMENT NA CITI BENKI WAKABIDHI ZAWADI KWA WASHINDI WA BIDHAA BORA
Local News

SHIRIKA la Junior Archvment kwa kushirikiana na   Citi Benki wamewapongeza vijana wajasiriamali walioshinda katika shindano la bidhaa bora lililofanyika jijini Dar es salaam kwa lengo la kumtafuta mshindi wa bidhaa bora atakayewakilisha katika shindano la Ujasiriamali Afrika. Akizungumza wakati wa kukabidhi zawadi kwa washindi watatu kati ya makundi 13 walioshiriki, mkurugenzi wa   shirika lisilo la serikali la Junior archievement Maria Ngowi amesema shirika hilo limekuwa likidhaminiwa na CITI Benki ili kuweza kutoa mafunzo ya ujasiriamali...

Like
289
0
Wednesday, 17 December 2014
CHADEMA YAMTAKA RAIS KUWAWAJIBISHA WAHUSIKA WA SAKATA LA ESCROW
Local News

KUFUATIA kujiuzulu kwa Mwanasheria Mkuu wa Serikali Jaji Fredrick Werema, Chama cha Demokrasia na Maendeleo – CHADEMA- kimemtaka Rais JAKAYA KIKWETE kuwawajibisha haraka viongozi wengine waliohusika katika sakata la Akaunti ya TEGETA ESCROW. Akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es salaam Naibu katibu mkuu wa chama hicho JOHN MNYIKA amesema Rais alipaswa kumuwajibisha kabla hajachukuwa uamuzi huo wa kujiuzulu hivyo amemtaka kuchukua hatuwa za haraka kuwawajibisha watuhumiwa waliobaki akiwemo Waziri wa Nishati na Madini...

Like
300
0
Wednesday, 17 December 2014
TAMISEMI YAWAFUKUZA KAZI WAKURUGENZI WALIOHARIBU CHAGUZI ZA SERIAKALI ZA MITAA
Local News

OFISI ya waziri mkuu tawala za mikoa na serikali za mitaa -TAMISEMI- imetoa maamuzi ya kutenguwa uteuzi, kuwasimamisha kazi, na kutoa onyo kali kwa wakurugenzi walioshindwa kutekeleza wajibu wao katika uchaguzi wa serikali za mitaa uliofanyika Disemba 14 mwaka huu. Akitangaza maamuzi hayo leo jijini Dar es salaam mbele ya waandishi wa habari waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu –TAMISEMI- HAWA GHASIA amesema wizara yake imetekeleza wajibu wake kwa kutoa mafunzo na kuwezesha kifedha, hivyo kasoro zilizojitokeza ni uzembe...

Like
344
0
Wednesday, 17 December 2014
SERIKALI YAENDELEA NA MPANGO WA KUTOA ELIMU YA MSINGI KWA WATOTO
Local News

SERIKALI INAENENDELEA na mpango wake wa kutoa Elimu ya msingi kwa watoto wote waliofikia umri wa kwenda shule nchini. Hayo yamesemwa na Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi Dokta SHUKURU Kawambwa wakati akiwasilisha mada inayohusu “Namna Tanzania inavyoboresha Usawa wa Kinga ya Jamii katika Sekta ya elimu” katika kongamano la Kimataifa linaloendelea katika siku ya pili jijini Arusha kuhusu Kinga ya Jamii. Dokta KAWAMBWA ameeleza kuwa mpango huo umeanzia Elimu ya Awali, shule ya Msingi na Sekondari ambapo kila...

Like
270
0
Wednesday, 17 December 2014