WAKAZI na wafanyabiashara wa eneo la banana jijini Dar es Salaam wameiomba halmashauri ya manispaa ya Ilala kuondoa dampo la taka ambalo siyo rasmi ambazo zinatupwa kandokando ya barabara ili kuweza kuzuia magonjwa ya mlipuko. Takataka hizo ambazo zimewekwa katika eneo ambalo siyo rasmi zimekaa kwa muda mrefu bila kuondolewa hali inayosababisha eneo hilo kuwa na harufu mbaya kwa wakazi hao. Hayo yamesemwa leo jijini Dar es Salaam na baadhi ya...
UCHAGUZI wa Serikali za Mitaa katika sehemu kubwa nchini umeshindwa kufanyika kwa sababu mbalimbali,zikiwemo za kutofikishwa kwa Vifaa vya kupigia kura Vituoni. Wakati maeneo mengine uchaguzi huo licha ya kufanyika ,umetawaliwa na Vurugu ambazo baadhi ya vurugu hizo zimetokana na utaratibu mbovu uliopo katika kituo husika. Pamoja na hayo Wananchi walio wengi wameilalamikia Serikali kwa kushindwa kuweka utaratibu mzuri wa kupiga kura hivyo wananchi wanaamini kutakuwa na hujma ndani...
MUDA wowote kuanzia leo Rais JAKAYA KIKWETE atatoa na kutangaza uamuzi wake kuhusiana na baadhi ya Watendaji wakiwemo Mawaziri kuhusishwa katika kashfa ya Akaunti ya Tegeta ESCROW. Wiki iliyopita Rais KIKWETE alipokea na kuanza kuipitia Ripoti,Nyaraka na Ushauri uliotolewa katika maazimio ya Bunge kuhusu Akaunti ya Tegeta ESCROW. Rais KIKWETE ambaye ameanza kazi rasmi Desember 8 mwaka huu, baada ya mapumziko kutokana na upasuaji aliofanyiwa mwezi uliopita amesema atatoa uamuzi wake ndani ya wiki hii....
MJUMBE wa Halmashauri Kuu ya Taifa –NEC, ya Chama Cha Mapinduzi –CCM, kupitia wilaya ya Lindi mjini Mama Salma Kikwete amewataka wanachama wa chama hicho pamoja na wananchi kujitokeza kwa wingi kupiga kura katika uchaguzi wa Serikali za mitaa unaotarajia kufanyika mwishoni mwa wiki hii. Mama Kikwete ambaye ni Mke wa Rais Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete ametoa rai hiyo wakati akiongea na wanachama pamoja na wagombea wa nafasi za Uenyeviti na Wajumbe wa Serikali za mitaa katika kata za Ndoro...
HALMASHAURI ya Manispaa ya Kinondoni imefanikiwa kujenga maabara 138 ikiwa ni agizo la Rais JAKAYA KIKWETE la kutaka kila shule za Kata ziwe na Maabara. Hayo yamebainishwa jijini Dar es salaam na Mkurugenzi wa Manispaa hiyo Mhandisi MUSA NATTY wakati wa hafla ya kukabidhi vyeti kwa wafanyakazi waliofanya vizuri wakiwamo wasimamizi wa Maabara hizo. Mhandisi NATTY ameeleza kuwa kwa kiasi kikubwa wametimiza agizo la rais kwani awali walikuwa na maabara 12 na vyumba 126 hivyo kufanya idadi ya maabara...
Vijana wa TANZANIA wameaswa kujitokeza kwa wingi kushiriki Chaguzi mbalimbali hususani huu wa Serikali za Mitaa unaotarajiwa kufanyika Desember 14 mwaka huu ili kupata viongozi bora kwa manufaa ya Taifa. Wito huo umetolewa leo na Mkurugenzi Mtendaji wa EFM Radio FRANCIS SIZA wakati wa mahojiano katika kipindi cha Joto la Asubuhi ambapo amesema kuwa ni wakati muafaka kwa vijana kutumia fursa hiyo kuchagua viongozi watakaosaidia nchi kufikia katika malengo ya kuwa na maendeleo pamoja na uchumi Imara. Amewaomba watanzania...
RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete amemteua Bwana Laurence Nyasebwa Mafuru kuwa Msajili wa Hazina kuanzia tarehe 5 Novemba, 2014. Taarifa iliyotolewa na Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi Ombeni Sefue imeeleza kuwa kabla ya uteuzi wake, Bwana Mafuru alikuwa Mkuu wa Idara ya Rasilimali Fedha katika Ofisi ya Rais inayohusika na ufuatiliaji Miradi ya Matokeo Makubwa Sasa -PDB. Aidha Bwana Mafuru pia alikuwa Kaimu Mtendaji Mkuu wa Benki ya FBME iliyowekwa chini ya uangalizi wa...
MBUNGE WA MONDULI na waziri Mkuu wa zamani Mheshimiwa EDWARD LOWASSA amesema Serikali ya Awamu ya Nne inayoongozwa na Rais JAKAYA KIKWETE imefanya makubwa ikiwa ni pamoja na usambazaji Umeme na Maji Vijijini. Mheshimiwa LOWASSA ameeleza hayo wakati akizungumza katika Mkutano wa Kampeni za Uchaguzi wa Serikali za Mitaa na Viongoji huko Bwawani Mto wa Mbu Wilayani Monduli. Amebainisha kuwa haijawahi kutokea Serikali ya Rais KIKWETE imefanya makubwa katika Umeme, Barabara na Maji na kwamba wakati akiwa Waziri wa Maji...
UMOJA WA AFRICA na nchi zake 13 ikiwemo Tanzania zimekutana leo nchini kujadili mpango wa muda mfupi wa kukabiliana kwa haraka na migogoro na majanga yanayojitokeza wakati wowote Africa ACIRC. Mpango huo wa ACIRC uliounda jeshi la Afrika la kukabiliana kwa haraka na migogoro na majanga yanayojitokeza wakati wowote kupitia zoezi la utulivu, Africa imelenga kutimiza malengo ya nchi za umoja huo kwa kupima uwezo wa kutatua matatizo yake yenyewe ambapo kwa mwaka huu Tanzania imekuwa mwenyeji wa hafla hiyo....
WAZIRI WA NISHATI na Madini Profesa SOSPITER MUHONGO amewasilisha hoja yenye maelezo juu ya mkataba uliowekwa kati ya kampuni ya –IPTL-na shirika la umeme nchini Tanesco ambapo amesema kuwa taarifa iliyotolewa na kamati ya hesabu za serikali na mashirika ya umma- PAC- haina ukweli wowote kwa kuwa fedha za –ESCROW– siyo fedha za umma. Akiwasilisha hoja hiyo leo Bungeni mjini Dodoma Profesa MUHONGO amesema kuwa ingawa kiasi hicho cha fedha za –ESCROW- siyo za umma pia hakuna ukweli wowote juu...
WAZAZI nchini wameshauriwa kuwekeza katika sekta ya elimu ili kuweza kusaidia kutatua changamoto mbalimbali zinazoikabili sekta hiyo hasa kwa baadhi ya shule za msingi nchini. Hayo yamebainishwa leo jijini Dar es Salaam na mtabibu wa tiba mbadala Abdalah Mandai wakati akizungumza na kituo hiki juu ya changamoto mbalimbali za sekta ya elimu nchini. Amesema kuwa baadhi ya shule za msingi zinakabiliwa na upungufu mkubwa wa madawati pamoja na vyumba vya madasara kitendo kinachochangia wanafunzi kusoma huku wakiwa wamekaa chini na...