Local News

NANYUMBU WALALAMIKA KUNYANYASWA HOSPITALI MASASI
Local News

WANANCHI wa Wilaya ya Nanyumbu mkoani Mtwara wamemlalamikia Katibu Mkuu wa CCM ABDULRAHMAN KINANA kuwa wagonjwa wanaotoka wilani humo kwenda Hospital ya Wilaya ya Masasi wananyanyaswa. Wananchi hao wameiomba Serikali kutoa kibali cha kupandisha hadhi hospital ya Wilaya ya Nanyumbu ambapo Wizara ya Afya na Ustawi wa jamii imeombwa kibali kwa muda mrefu lakini hadi sasa imeshindwa kutoa na matokeo yake hospital ya Wilaya ya Nanyumbu imebaki kuwa Kituo cha Afya. Wananchi hao wamemwambia Ndugu KINANA kuwa ni vema akawasaidia...

Like
430
0
Thursday, 27 November 2014
PINDA: TANZANIA BILA FOLENI INAWEZEKANA
Local News

WAZIRI MKUU MIZENGO PINDA amesema kuwa serikali imedhamiria kuondoa tatizo la msongamano  wa magari katika miji yote mikubwa ikiwemo Dar es salaam, Mwanza na Arusha kwa kuwashirikisha wananchi pamoja na vyombo husika kupitia sheria na Taratibu zilizowekwa. Waziri PINDA ameyasema hayo leo Bungeni mjini Dodoma wakati akijibu swali la mbunge wa Kilwa mheshimiwa MURTAZA MANGUNGU aliyehoji kutaka kujua mikakati ya serikali katika utekelezaji wa suala hilo nchini. Bunge linaendelea tena leo mjini Dodoma ambapo kutakuwa na Tamko la serikali juu ya...

Like
273
0
Thursday, 27 November 2014
ZIMAMOTO KUANZISHA OPARESHENI YA UKAGUZI WA VIFAA
Local News

JESHI la Zimamoto na Uokoaji mkoani Pwani linatarajia kuanza Oparation maalum kwa ajili ukaguzi wa Vifaa vya kung’amua na kuzima moto kwenye shule za Kawaida zenye Mabweni na Vyuo mkoani humo. Kamanda wa Jeshi hilo mkoani Pwani GOODLUCK ZELOTE ameeleza hayo alipokuwa akizungumza na Waandishi wa Habari Ofisini kwake. Amebainisha kuwa Oparation hiyo inatokana na matukio ya moto kutokea mfululizo mkoani humo ambapo hivi karibuni shule ya Sekondary ya Filbert Bay iliungua moto na kuteketeteza baadhi majengo na maduka sita....

Like
506
0
Wednesday, 26 November 2014
VITUMIAJI VYA UZAZI WA MPANGO NI HATARI
Local News

WANAWAKE  nchini  wametakiwa  kuachana  na  matumizi  ya  njia za kisasa  za uzazi wa  mpango na badala  yake watumie njia  asilia ili kuepuka  madhara yatokanayo na  njia za kisasa. Hayo  yamebainishwa leo jijini Dar es Salaam na  Mkurugenzi  wa shirika  lisilo la kiserikali  la kutetea  uhai  Pro-life wakati   akizungumza  na waandishi wa Habari kuhusiana na masuala ya afya ya uzazi na uzazi salama kwa akina mama. Amesema  kuwa  shirika hilo limeweka  mikakati ili...

Like
372
0
Wednesday, 26 November 2014
ESCROW KUJADILIWA BUNGENI LEO
Local News

BUNGE la Jamhuri ya muungano wa Tanzania leo linaanza mjadala kuhusu sakata la wizi wa fedha katika akaunti ya Tegeta –ESCROW- kutokana na zoezi la kugawa ripoti ya mkaguzi mkuu wa serikali-CAG- na ya Takukuru kwa wabunge wote kukamilika. Taarifa zinaeleza kuwa mjadala huo unaanza kwa wabunge mara baada ya kamati ya –PAC- ikiongozwa na mbunge wa kigoma kaskazini mheshimiwa ZITTO KABWE kuwasilisha ripoti yake ya uchunguzi bungeni. Mbali na hayo suala la muingiliano wa madaraka kati ya bunge na...

Like
336
0
Wednesday, 26 November 2014
CHENGE AISHAURI SERIKALI KUPUNGUZA VAT
Local News

SERIKALI imeshauriwa kuangalia upya suala la marekebisho ya kodi katika baadhi ya vifungu vya sheria ikiwemo kupunguza kiwango cha –VAT– kutoka asilimia 18 hadi kufikia asilimia 16 hususani katika sekta ya utalii ili kuboresha uchumi wa nchi. Ushauri huo umetolewa leo Bungeni mjini Dodoma na Mwenyekiti wa kamati ya kudumu ya hesabu za bunge mheshimiwa ANDREW CHENGE wakati akitoa maoni ya kamati hiyo mara baada ya kusomwa kwa mara ya pili muswada waongezeko la thamani ya kodi nchini-VAT-la mwaka huu...

Like
333
0
Tuesday, 25 November 2014
OBAMA AMPA POLE KIKWETE
Local News

RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. Jakaya Mrisho Kikwete amepokea salamu za pole kutoka kwa Rais wa Marekani  Barak Obama. Katika salamu zake Rais Obama ameelezea kufurahishwa na taarifa kwamba Rais Kikwete anaendelea vyema kiafya baada ya kufanyiwa upasuaji kwa mafanikio na kuondoa tatizo la tezi dume alilokuwa nalo. Katika salamu zake, Rais Obama amesema kuwa alipata heshima kufanya ziara rasmi nchini Tanzania mwaka 2013, na pia kumualika Rais Kikwete kwenye mkutano wa  Marekani na viongozi wa Afrika...

Like
290
0
Tuesday, 25 November 2014
WANAWAKE 100 WA JAMII YA KIMASAI WAANDAMANA NA KULALA MSITUNI
Local News

  ZAIDI ya Wanawake 100 wa Jamii ya Kimasai wameandamana na kwenda kulala msituni kwa muda wa siku mbili wakipinga kitendo cha Serikali kukata miti ya Asili katika kijiji cha Matebete ,Kata ya Itamboleo Wilaya ya Mbarari mkoani Mbeya. Wanawake hao wamechukua uamuzi huo wakipinga hekta zaidi ya 30,000 za miti wanayoitegemea katika shughuli zao kukatwa bila wao kushirikishwa. Mmoja wa Wanawake hao aliefahamika kwa jina la SOFIA KALEI ameeleza kuwa hawako tayari kuona msitu huo ukiteketezwa kwa sababu umekuwa...

Like
371
0
Tuesday, 25 November 2014
UANDIKISHWAJI WA WAPIGA KURA WADORORA
Local News

UANDIKISHAJI wa Wananchi katika daftari la wapiga kura kwa ajili ya Uchaguzi wa Serikali za Mitaa ambao umeshaanza umeonekana kudorora. Hayo yamebainika baada ya EFM kutembelea vituo mbalimbali vya kujiandikisha jijini Dar es salaam. Akizungumza na EFM Mmoja wa Mawakala wa Uandikishaji Mtaa wa Msolome Kinondoni B ABDAN SENGODA ameeleza kuwa mahudhurio ya Wananchi sio mazuri tangu zoezi hilo...

Like
493
0
Tuesday, 25 November 2014
WANAJESHI 5 WAPEWA MAFUNZO YA KIVITA YA MAJINI KUPAMBANA NA MAHARAMIA UKANDA WA BAHARI YA HINDI
Local News

WANAJESHI kumi na tano wa Jeshi la Wananchi la Tanzania leo wamepewa mafunzo ya kivita ya majini ya namna ya kupambana na Maharamia kwenye Ukanda wa Bahari ya Hindi. Akizungumza na Waandishi wa Habari jijini Dar es Salaam Balozi wa Italia Dokta LUIGI SCOTTO amebainisha kuwa wanajeshi hao watafundishwa namna ya kutega na kutegua zana za kivita yakiwemo mabomu yanayotumiwa na maharamia kwenye shughuli za utekaji nyara wa Meli za mizigo na abiria. Dokta LUIGI ameeleza kuwa katika harakati za...

Like
403
0
Monday, 24 November 2014
TANESCO NA REA WATOLEA UFAFANUZI UCHELEWESHWAJI WA MRADI WA UMEME MKURANGA
Local News

SHIRIKA la umeme nchini -TANESCO kwa kushirikiana na Wakala wa Umeme Vijijini –REA wametoa ufafanuzi juu ya kuchelewa kwa ukamilikaji wa Mradi wa Umeme katika vijiji vya Wilaya ya Mkuranga Mkoani Pwani. Akizungumza na EFM Ofisini kwake jijini Dar es salaam Meneja wa-TANESCO Kanda ya Dar es salaam na Pwani MAHANDE MUGAYA amesema tatizo hilo linatokana na ufinyu wa Bajeti iliyowekwa kwa kuwa haikidhi mahitaji ya Umeme unaohitajika. Amewatoa hofu wananchi wa Vijiji hivyo kwa kuwa mradi huo unatarajia kukamilika...

Like
543
0
Monday, 24 November 2014