Local News

JAMII IMETAKIWA KUUNGA MKONO UKUZAJI WA VIPAWA
Local News

JAMII nchini imetakiwa kuunga mkono jitihada mbalimbali zinazofanya na baadhi ya taasisi zinazo jihusisha na utoaji wa ujuzi na uendelezaji wa vipawa vya watoto na vijana ili kujenga jamii yenye tabia ya kujitegemea . Hayo yamebainishwa na Mkude Kilosa ambaye ni  mkurugenzi msaidizi wa kituo cha kulelea watoto na vijana cha baba watoto kilichopo jijini Dar es salaam wakati akizungumza na efm  juu ya maandalizi ya tamasha la wazi la sarakasi tamasha lililolenga kukuza na kuendeleza ujuzi wa vijana katika...

Like
246
0
Friday, 26 February 2016
SERIKALI YATAKIWA KUWEKEZA ZAIDI KATIKA UBORA WA ELIMU
Local News

SERIKALI ya awamu ya tano imetakiwa kuwekeza zaidi katika ubora wa elimu na sio katika kutanua upatikanaji na nafasi ya elimu ili kutekeleza sera ya Elimu bure kwa Shule za Serikali kwa kuwa tafiti zinaonesha kuwa kiwango cha ufaulu katika miaka 10 iliyopita kimeshuka katika Shule za Msingi na Sekondari licha ya mfumo huo kutumika katika elimu ya msingi.   Hayo yamesemwa leo jijini Dar es salaam wakati wa uwasilishaji wa ripoti iliyotolewa na Twaweza kuhusu maoni ya Wananchi juu...

Like
264
0
Thursday, 25 February 2016
TANZANIA NA ZAMBIA ZIMETAKIWA KUONGEZA USHIRIKIANO
Local News

WIZARA ya Mambo ya Nje ya Nchi Ushirikiano wa Afrika Mashariki Kanda na Kimataifa Nchini,  imezitaka  Nchi za Tanzania na Zambia kuongeza ushirikiano ili kuleta mafanikio ya pamoja katika Sekta mbali mbali ikiwa ni pamoja na Biashara, Uchumi, Mawasiliano, Elimu, Utamaduni, Utalii,Kilimo pamoja na maswala ya Tekinolojia.   Hayo yamebainishwa na Naibu katibu Mkuu wa Wizara hiyo Ramadhan Mwinyi alipozungumza  katika Ufunguzi wa Mkutano wa Tisa wa Tume  ya  Kudumu ya Pamoja -JPC- kati ya Tanzania na Zambia ambapo amesema...

Like
222
0
Thursday, 25 February 2016
SERIKALI YAITAKA KAMPUNI YA KADCO KUIMARISHA ULINZI KIA
Local News

SERIKALI imeitaka kampuni ya KADCO inayoendesha Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Kilimanjaro-KIA, kuongeza mapato na kuimarisha ulinzi ili kulinda hadhi ya uwanja huo, kuchangia pato la serikali na kudhibiti hujuma dhidi ya watu wasio waaminifu. Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa amesema hayo wakati akikagua utendaji na mradi wa ujenzi wa njia za kurukia ndege unaondelea katika uwanja...

Like
328
0
Wednesday, 24 February 2016
MAKAMU WA RAIS, SAMIA SULUHU AZINDUA PROGRAM MAALUM YA MWANAMKE NA WAKATI UJAO
Local News

MAKAMU wa rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan leo amezindua program maalumu ya mwanamke na wakati ujao ambayo itawajengea wanawake uwezo katika bodi za wakurugenzi wa taasisi na Kampuni mbalimbali. Katika uzinduzi huo uliofanyika kwenye hote ya Hayatt Regency jijini Dar es salaam, na kuhudhuriwa na watu mbalimbali wakiwemo kutoka nchini za Kenya na Uganda pamoja na wengine kutoka Ulaya na Asia, Mheshimiwa Suluhu amesema kuwa, wanawake ni watendaji wazuri na wanamaamuzi sahihi katika uongozi...

Like
322
0
Wednesday, 24 February 2016
WANANCHI WAMETAKIWA KUTUNZA BARABARA
Local News

SERIKALI imewataka wananchi kutunza barabara zinazojengwa  na Serikali kwa kushirikiana na wafadhili katika Halmashauri zote hapa nchini.   Akizungumza Jijini Dar es salaam katika hafla fupi ya kupokea ripoti ya utekelezaji wa mradi wa Ujenzi na ukarabati wa barabara za halmashauri nchini  Katibu Mkuu Ofisi ya Rais TAMISEMI bwana Mussa Iyombe amebainisha kuwa mradi huo umefadhiliwa  na  Shirika  la Maendeleo la Japan (JICA) .   Kwa mujibu wa Iyombe, Mradi huo unatekelezwa katika Halmashauri  za Iringa,Mufindi,Chamwino na...

Like
245
0
Wednesday, 24 February 2016
SEKTA YA MIFUGO HAICHANGII UCHUMI WA NCHI
Local News

IMEELEZWA kuwa sekta ya mifugo  nchini haichangii uchumi wa  nchi kama ilivyotarajiwa na serikali.   Akizungumza katika mkutano wa kwanza wa maaandalizi   ya  mpango mkakati wa sekta ya mifugo, Naibu Waziri wa kilimo mifugo na uvuvi Mheshimiwa  WILLIAM  OLE NASHA, amesema kutokana  na hali hiyo Serikali inakusudia kuandaa mkakati ambao utainua sekta hiyo  nakuweza kuchangia uchumi wa nchi  na wananchi na wananchi kwa ujumla.   Amesema kuwa pamoja na Tanzania kuwa nchi ya tatu Afrika kwakuwa na mifugo mingi ,lakini...

Like
308
0
Wednesday, 24 February 2016
BIBI ABIOLA DELUPE MWAKILISHI WA UBALOZI WA NIGERIA AITEMBELEA EFM
Local News

Mwakilishi wa ubalozi wa Nigeria, bibi Abiola Delupe aitembelea Efm Radio leo  katika vitengo tofauti na  kuona utendaji kazi wa radio. Huku akikutana na baadhi ya watangaziji  kujadili mambo tofauti tofauti na jinsi watakavyo weza kuendeleza kazi zoa nje ya mipaka ya Tanzania. Bibi Abiola Delupe akizungumza jambo na Mkurugenzi wa Efm radio Francis Ciza. Baadhi ya viogozi wa Efm Radio katika mazungumzo na Bibi Abiola Delupe. Meneja mkuu Dennis Ssebbo akijadili mambo tofauti kuhusiana na ufanisi wa kazi katika...

Like
1115
0
Tuesday, 23 February 2016
WANANCHI WAIUNGA MKONO SERIKALI KUTUMBUA MAJIPU
Local News

WAKATI Serikali kupitia Mawaziri,Wakuu wa Mikoa na Wakuu wa Wilaya ikiendelea na mpango wa kufukuza wafanyakazi wasiokidhi viwango vya utendaji kazi kwa kutumia Kauli ya Kutumbua Majipu iliyoanzishwa na Rais wa Awamu ya Tano Dokta John Pombe Magofuli, Wananchi wengi wameonesha kuunga mkono hatua hiyo. Wakizungumza na EFM kwa nyakati tofauti Wananchi hao wamesema Sehemu kubwa ya Wafanyakazi wamekuwa wakifanya kazi zao kwa mazoea na kufanya Ofisi na Taasisi za Serikali kama mali zao hivyo kitendo cha kuwaondosha kitasaidia kuongeza...

Like
252
0
Monday, 22 February 2016
MKUU WA CHUO CHA UTUMISHI WA UMMA ASIMAMISHWA KAZI
Local News

WAZIRI wa nchi ofisi ya Rais menejimenti ya utumishi wa umma na utawala bora mheshimiwa Angela Kairuki amemsimamisha kazi aliyekuwa mkuu wa chuo cha utumishi wa umma Said Nassoro kutokana na kushindwa kusimamia watumishi waliopo chini yake. Kairuki ametoa maagizo hayo leo Jijini Dar es salaam kwenye mkutano na waandishi wa Habari katika mkutano ulifanyika chuoni hapo. Aidha amebainisha kuwa usimamizi mbovu wa bwana Nassoro umetoa mwanya kwa viongozi mbalimbali wa matawi kufanya ubadhilifu wa mali za...

Like
299
0
Monday, 22 February 2016
TAMWA: VYOMBO VYA HABARI HAVIKUWAPA NAFASI YAKUTOSHA WANAWAKE UCHAGUZI MKUU 2015
Local News

CHAMA cha Waandishi wa Habari Wanawake Tanzania (TAMWA) kimesema wanawake waliogombea nafasi mbalimbali kwenye Uchaguzi Mkuu 2015 walikosa nafasi ya kutosha kuzungumza kwenye vyombo vya habari.   Kwa mujibu wa TAMWA,  utafiti mdogo walioufanya katika vyombo vya habari kadhaa ulibaini kuwa ni asilimia 11 tu ya wanawake wagombea ndio walipata nafasi ya kuandikwa katika magazeti wakati wa uchaguzi huo.   Takwimu hizo zilitolewa mwishoni mwa wiki katika semina ya wadau wa vyombo vya habari pamoja na baadhi ya wagombea na...

Like
251
0
Monday, 22 February 2016