BARAZA la Taifa la Ujenzi limepokea migogoro 41 na kufanikiwa kuitafutia ufumbuzi katika kipindi cha mwaka 2015 kwa kushirikiana na wadau wa sekta ya Ujenzi nchini. Hayo yamesemwa leo na Mtendaji Mkuu wa Baraza hilo, Mhandisi Dokta Leonard Chamuriho wakati wa mkutano na waandishi wa habari Jijini Dar es salaam. Akizungumzia majukumu ya Baraza hilo katika kutatua Migogoro inayojitokeza katika Sekta hiyo, Mhandisi Chamuriho amebainisha kuwa migogogoro iliyojitokeza imekuwa ikitegemea Ukubwa wa mradi, Hali ya eneo la mradi,...
KESI inayowakabili wafanyakazi wa Mamlaka ya mapato Tanzania (TRA) inatarajiwa kusikilizwa tena January 13, mwaka 2016 Akizungumza katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini dar es salaam Wakili wa Serikali Bi.Dianna Lukondo amesema kuwa kwa leo Kesi ilikuja kwa ajili ya kusikilizwa na kutoa dhamana kwa washtakiwa na hivyo imeshindikana kusikilizwa kutokana na upelelezi kutokamilika. Washtakiwa hao wanatuhumiwa kwa kosa la uhujumu uchumi, wakidaiwa kuhusika na upotevu wa makontena 329 katika Bandari ya Dar es Salaam...
KUFUATIA kukithiri kwa uchafu katika kata ya Upanga Magharibi licha ya kuwepo kwa kampuni ya TIRIMA iliyochukuwa tenda ya kufanya usafi katika kata hiyo, Uongozi umekusudia kuvunja mkataba na kampuni hiyo. Diwani wa kata ya Upanga Magharibi Adinani Kitwana Kondo amesema eneo lililopo hospitali ya Muhimbili limekithiri kwa uchafu kitendo ambacho kinahatarisha maisha ya watu wengi wanaoishi na wanaotembelea maeneo hayo. Kondo amesema kampuni hiyo ya TIRIMA imekuwa ikikusanya shilingi elfu kumi na tano kwa kila mkazi wa...
JUMLA ya ng’ombe sabini na tisa zimeuawa kwa kipindi kinacho ishia mwezi Desemba mwaka huu kutokana na mapigano kati ya wakulima na wafugaji yaliyotokea kwenye kijiji cha Dihinda Tarafa ya Turiani Wilaya ya Mvomero Mkoani Morogoro. Mkuu wa kitengo cha Habari na Mawasilano kutoka Wizara ya Mifugo ,Kilimo na Uvuvi ,JUDITH MHINA amesema kuwa kumekuwa na ukiukwaji wa haki za wanyama hususani ng’ombe katika wilaya hiyo kwani wanyama hao wamekuwa wakiuawa bila sababu maalum. JUDITH ameeleza kuwa kutokana na...
IMEELEZWA kuwa Fedha zitakazopatikana katika Tamasha la mkesha wa kuombea amani nchini zitatumika kuwasaidia watu wenye mahitaji hasa afya ya mama na mtoto. Hayo yamesemwa na Mwenyekiti wa Jumuiya wa Makanisa ya Pentekoste , ambaye pia ni Askofu wa huduma ya Tanzania Fellowship TFC, Askofu Godfrey Malassy alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es salaam. Askofu Malassy amesema kwamba, fedha zitakazopatikana katika tamasha hilo zitanunua vifaa vinavyotumia nishati ya jua ili kuwasaidi wamama...
WAZIRI wa Fedha na Mipango Dokta Philipo Mipango amesema kuwa wizara yake haitakuwa tayari kuona nchi ya Tanzania ikiendelea kujiendesha kwa kutegemea misaada kutoka nchi wahisani, bali itajiendesha kwa kukusanya mapato yakutosha yaliyopo ndani ya nchi ili jamii iweze kufaidika na matumizi ya mapato hayo. Dokta mipango ameyasema hayo leo Jijini Dar es Salaam baada ya kukabidhi ofisi aliyokuwa akikaimu ya Mamlaka ya Mapato nchini (TRA) kabla ya kuapishwa kuwa waziri wa fedha na mipango kwa kamishna mkuu mpya wa...
WATUMISHI Wizara ya Fedha na Mipango wameaswa kufanya kazi kwa weledi na kuwekeza nguvu zaidi katika ukusanyaji mapato ili kukuza uchumi wa nchi na kuifanya nchi iwe kitovu cha uchumi Barani Afrika. Hayo yamesemwa na Waziri wa Fedha na Mipango Mheshimiwa. Dokta. Philip Mpango alipokuwa akiongea na watendaji wa Wizara hiyo. Katika mazungumzo yake na watendaji hao, Dokta. Mpango, aliuagiza uongozi wa Wizara yake kuunda na kusimamia sera za mfumo wa ukusanyaji kodi ambao utabaki kuwa rafiki kwa wafanyabiashara...
RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania dokta John Pombe Magufuli anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika Mkesha wa kuiombea amani Tanzania utakaofanyika Disemba 31 mwaka huu katika uwanja wa Taifa. Kwa mujibu wa Mwenyekiti wa Jumuiya ya Makanisa ya Pentekoste nchini (TFC) Godfrey Malassy Cmaandalizi yote yamekamilika ikiwemo kibali kutoka polisi. Askofu Malassy ameongeza kuwa mkesha huo utakuwa ni kwa ajili ya kumshukuru Mungu kwa kuijalia Tanzania kumaliza Uchaguzi Mkuu uliofanyika mwezi Oktoba mwaka huu kwa Amani na utulivu, pamoja...
WAZIRI Wizara ya Maliasili na Utalii Mhe. Prof. Jumanne Maghembe amewasili wizara kwake leo mara tu baada ya kuapishwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ikulu Jijini Dar es salaam. Waziri Profesa Maghembe ni miongoni mwa Mawaziri wanne walioteuliwa hivi karibuni na rais kukamilisha baraza jipya la Mawaziri katika Serikali ya awamu ya tano chini ya Rais Dokta John Pombe Magufuli. Kufuatia hafla hivyo, hivi sasa Wizara zote zimekamilika kwa ajili ya utekelezaji wa kauli mbiu ya awamu hii ya...
AKINAMAMA wajawazito na watoto katika hospitali ya wilaya ya maswa Mkoani Simiyu, wamekuwa wakilazimika kulala kitanda kimoja watu wawili na muda mwingine kupeana zamu kutokana na ufinyu wa wodi, na upungufu wa vitanda suala ambalo linaweza kusababisha maambukizi ya magonjwa. Kufuatia hali hiyo, wakizungumza na Efm wameiomba serikali kuyafungua majengo mapya ambayo tayari yameshakamilika ili kuweza kupunguza adha hiyo. Kituo hiki kimeshuhudia akinamama hao wakiwa wamelala wawili wawili wodini, huku baadhi...
WAZIRI wa wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Nape Nnauye amekanusha taarifa ambazo kwa takribani siku mbili zilizopita zilienea juu ya katazo rasmi la mavazi ya nguo fupi ambalo ilisemekana limetolewa na Wizara hiyo. Akizungumza na EFM kwa njia ya simu, Mheshimiwa Nnauye amesema Wizara imesikitishwa na Taarifa hizo na kwamba sheria zinazosimamia makosa ya kimtandao ziko wazi, hivyo anaamini mamlaka zinazohusika zitatekeleza wajibu...