Local News

WAGANGA WAKUU WA MIKOA NA WILAYA WAMETAKIWA KUSIMAMIA MIKAKATI YA KUDHIBITI KIPINDUPINDU
Local News

WIZARA ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Watoto  na Wazee imewataka Waganga Wakuu wa Mikoa na Wilaya wasimamie utekelezaji wa mikakati yote ya kudhibiti mlipuko wa kipindupindu ikiwa  ni pamoja na kusimamia kanuni za afya na kuhakikisha kuwa wanadhibiti ugonjwa huo  kwa kutoa taarifa ya utekelezaji kila siku .   Akizungumza na Wanahabari jijini Dar es salaam  Waziri wa Wizara hiyo  Mheshimiwa  Ummy Mwalimu amesema licha ya kasi ya ongezeko la ugonjwa huo kupungua Dar es salaam kutoka wastani wa...

Like
259
0
Wednesday, 16 December 2015
WATUMISHI WA SEKTA YA AFYA WAMETAKIWA KUTOFANYA KAZI KWA MAZOEA
Local News

SERIKALI imewataka watumishi wa sekta ya afya nchini kutofanya kazi kwa mazoea na badala yake kufanya kazi kwa bidii na uadilifu ili kufikia malengo yaliyowekwa.   Hatua hiyo inaelezwa itasiaidia kurahisisha maendeleo ya kijamii na kiuchumi kwa wananchi kwa kutoa huduma bora na zinazofikiwa kwa wakati.   Akifungua mkutano wa Baraza la Wafanyakazi wa iliyokuwa Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii, Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu amesema kila mtumishi wa umma anapaswa...

Like
196
0
Wednesday, 16 December 2015
MAWAKILI WAASWA KUZINGATIA MAADILI YA TAALUMA YA SHERIA
Local News

JAJI MKUU wa Tanzania Mheshimiwa Othman Chande amewataka Mawakili kote nchini kufanya kazi zao kwa kuzingatia weledi na maadili ya taaluma ya Sheria na kwamba wasisite kuwaeleza ukweli wateja wao wanaopeleka mashauri Mahakamani ili kuepuka kupoteza muda na gharama katika masuala yanayoweza kupatiwa ufumbuzi nje ya Mahakama.   Akizungumza na Mawakili wapya 104 waliohitimu Shule ya Sheria  kwa mwaka 2015 wakati wa hafla ya 53 ya kuwapokea na kuwaapisha iliyofanyika katika viwanja vya Karimjee jijini Dar es salaam, amesema kuwa...

Like
232
0
Wednesday, 16 December 2015
UJERUMANI YAPUUZA WITO WA MAREKANI
Local News

WAZIRI wa Ulinzi wa Ujerumani Ursula Von Der Leyen amepuuza wito wa Marekani wa kuitaka Ujerumani kuchangia zaidi kijeshi katika kukabiliana na kundi la wanamgambo wenye itikadi kali wa Dola la Kiislamu IS. Von Der Leyen amesema Ujerumani tayari inapambana dhidi ya makundi yenye itikadi kali ikiemo nchini Mali na Afghanistan na kuongeza kuwa Ujerumani inatuma ndege za kufanya shughuli za upelelezi nchini Syria zinazohitajika kwa dharura. Hata hivyo Waziri huyo wa Ulinzi wa Ujerumani amesema ataiandikia Marekani kuifahamisha kuwa...

Like
221
0
Tuesday, 15 December 2015
WAHITIMU WA UWAKILI WAMETAKIWA KUFUATA SHERIA NA TARATIBU ZA KAZI ZA MAHAKAMA
Local News

WAHITIMU wa taaluma ya Uwakili Nchini wametakiwa kuzingatia sheria na kufuata utaratibu katika kufanya kazi za mahakama ili kusaidia haki kutendeka katika jamii. Wito huo umetolewa leo na Mwanasheria Mkuu wa Serikali George  Masaju alipozungumza katika hafla ya kuapishwa kwa Mawakili wapya zaidi ya 100 jijini Dar es salaam na kusema kuwa kitendo cha Wakili kufanya kazi bila kufuata kanuni na utaratibu wa kazi hiyo ni kosa na hatua zinaweza kuchukuliwa dhidi yao. Kwa upande wake Jaji Mkuu wa Tanzania...

Like
258
0
Tuesday, 15 December 2015
WAZIRI WA ULINZI NA JESHI LA KUJENGA TAIFA AANZA KAZI RASMI
Local News

WAZIRI wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, dokta Hussein Mwinyi, aliyeteuliwa na kisha kuapishwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri jeshi Mkuu ameripoti ofisini na kuanza kazi rasmi.   Waziri Mwinyi amewasili ofisini kwake na kulakiwa na Naibu Katibu Mkuu, Mkuu wa Majeshi Mnadhimu Mkuu, Mkuu wa Jeshi la Kujenga Taifa, wanajeshi na watumishi wa Umma wakiongozwa na Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Job Masima.   Akizungumza na Menejimenti ya Wizara, Waziri Mwinyi amesema matarajio...

Like
223
0
Tuesday, 15 December 2015
KAGERA: WANAOGUSHI NYARAKA ZA KUCHUKULIA DAWA KUCHUKULIWA HATUA
Local News

MFUKO wa Taifa wa Bima ya Afya umesema hautawavumilia watumishi wa hospitali ya Mkoa wa Kagera wanaojihusisha na vitendo vya kughushi nyaraka za kuchukulia dawa katika maduka ya dawa na kuusababishia Mfuko kulipa fedha ambazo hazijatumika kihalali.   Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko huo Michael Mhando ameyasema hayo mkoani humo wakati akizungumza na uongozi wa Hospitali ya Mkoa wa Kagera kabla ya uzinduzi wa mpango wa Madaktari Bingwa ili kusaidia kutoa huduma kwa wanachama na wananchi kwa ujumla.   Mhando...

Like
216
0
Tuesday, 15 December 2015
TANESCO YAAGIZWA KUKAMILISHA MRADI WA KINYEREZI ONE NA TWO
Local News

WIZARA ya Nishati na Madini imewaagiza watendaji wa Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) kuhakikisha uzalishaji wa umeme katika Mradi wa Kinyerezi One na Two unakamilika ifikapo mwezi Februari mwaka 2016  na kuanza uzalishaji ili kuongeza kiasi cha nishati ya  umeme kufikia zaidi ya Megawati 100.   Agizo hilo limetolewa jana na Naibu Waziri, Wizara ya Nishati na Madini dokta Medadi Kalemani alipofanya ziara yake katika kituo cha kuzalisha umeme kwa kutumia nishati ya Gesi cha Kinyerezi jijini Dar es Salaam....

Like
271
0
Tuesday, 15 December 2015
JIMBO LA MBAGALA LAKABILIWA NA UKOSEFU WA AJIRA KWA VIJANA
Local News

IMEELEZWA kuwa Jimbo la Mbagala linakabiliwa na changamoto mbalimbali ikiwemo suala la ajira kwa vijana pamoja na elimu  ya ujasiliamali . Mbunge wa Mbagala Issa Ali Mangungu kupitia chama cha mapinduzi -ccm- ameyasema hayo  leo jijini Dar es Salaam wakati alipokuwa akizungumza katika mahafali ya kituo cha elimu na mafunzo  ya afya –KEWOVAC- Amesema kuwa wilaya nzima ya Temeke kuna chuo kimoja tu cha ufundi hali inayosababisha vijana wengi kushindwa kupata ujuzi ambao utawakwamua kiuchumi na badala yake huishia...

Like
353
0
Monday, 14 December 2015
WAZIRI WA HABARI, UTAMADUNI SANAA NA MICHEZO AAHIDI KUSHIRIKIANA NA WANAHABARI
Local News

WAZIRI  wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Nape Nnauye ameahidi kushirikiana na Waandishi wa habari pamoja na wamiliki wa vyombo vya habari ili kutatua changamoto mbali mbali zinazoikabili sekta ya habari Nchini.   Waziri Nape ameyasema hayo katika Mkutano na Waandishi wa habari pamoja na Wafanyakazi wa Wizara hiyo alipoingia Wizarani hapo kuanza kazi rasmi ambapo amesema amekusudia kuwa mlezi wa wanahabari pamoja na vyombo vya habari huku akimtaka kila mtu katika tasnia hiyo kutekeleza wajibu wake kwa kufuata misingi...

Like
241
0
Monday, 14 December 2015
ICTR KUTOA HUKUMU YA MWISHO
Local News

MAHAKAMA ya Kimataifa ya Mauaji ya Kimbari ya Rwanda (ICTR) iliyokuwa ikishughulikia kesi za mauaji yaliyotokea miaka 20 iliyopita leo itatoa hukumu yake ya mwisho kabla ya kufungwa rasmi.   Hukumu hiyo itakuwa dhidi ya watuhumiwa Pauline Nyiramasu ambaye ni waziri wa zamani wa Maendeleo ya wanawake nchini Rwanda na mtoto wake ambaye wote wamekana mashtaka yanayowakabili.   Mahakama hiyo ambayo imekuwa nchini katika mji wa Arusha ilikuwa ikisikiliza kesi za watuhumiwa wa mauaji ya kimbari yaliyotokea nchini Rwanda mwaka...

Like
234
0
Monday, 14 December 2015