RAIS wa Misri Abdel Fattah al-Sisi amesema kuna haja majeshi ya muungano wa jumuiya ya kiarabu ya Pan-Arab kutoa majeshi yao ili kukabiliana na ugaidi. Amesema kuwa mataifa kadhaa yametoa majeshi yao kukabiliana na kundi la wapiganaji wa Kiislam wa Islamic State tangu kuuawa kwa Wakristu huko nchini Libya. Mpaka sasa, Mataifa yaliyotoa misaada ya kifedha na kijeshi ni Jordan,Falme za Kiarabu na Marekani kwa lengo la kuangamiza kundi hilo Syria na Iraq....
OFISI ya Rais nchini Ufaransa imesema Viongozi wa Urusi,Ukraine, Ufaransa na Ujerumani wamekemea ukiukwaji wa makubaliano ya kusitisha mapigano Mashariki mwa Ukraine . Baada ya Mazungumzo ya simu kati ya Viongozi wanne wa Nchi hizo,wametoa wito wa utekelezwaji wa makubaliano yaliyowekwa mjini Minsk Juma lililopita, ikiwemo kuacha kabisa mapigano. Waangalizi wa Kimataifa wanaofuatilia utekelezaji wa makubaliano hayo nchini Ukraine wamesema pande zote mbili zinajutia kushindwa kutekeleza makubaliano...
SERIKALI ya Libya inayotambuliwa Kimataifa imeliomba Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kuiondolea nchi hiyo vikwazo vya silaha ili kukabiliana na kuzorota kwa hali ya Usalama nchini humo. Akihutubia Kikao cha dharura cha Baraza hilo, Waziri wa Mambo ya Nje wa Libya,MOHAMMED AL-DAIRI amesema hatua hiyo itaisaidia Serikali ya Libya kujenga jeshi lake, ili kuwatokomeza Islamic State na makundi mengine ya Wapiganaji. Waziri huyo wa Mambo ya nje wa Libya ameungwa mkono na Waziri wa Mambo ya nje wa...
RAIS BARACK OBAMA ameliambia kongamano dhidi ya misimamo mikali ya kidini akisema kuwa kuwa wako kwenye vita si na Waislamu bali na magaidi waliouchafua Uislamu. Bwana OBAMA amesema ni sharti dunia ikabiliane na Itikadi zilizopindishwa na makundi kama Islamic State yanayochochea vita na kuwapa vijana mafundisho yenye misimamo mikali ya imani ya dini . Rais huyo wa Marekani ameeleza hayo katika mkutano wa siku tatu unaofanyika mjini Washington ambapo amesema dunia inatakiwa kukabiliana na makundi ya aina...
IMEELEZWA kuwa kuna dalili za kulegezwa kamba katika mvutano wa madeni kati ya Ugiriki na nchi za kanda ya Euro. Kwa mujibu wa duru za serikali mjini Athens,Waziri wa Fedha wa Ugiriki YANNIS VAROUFAKIS amepanga muda wa mpango wa misaada urefushwe. Muda huo ulikuwa umalizike mwishoni mwa mwezi...
KUFUATIA mapigano makali katika mji wa Mashariki ya Ukraine,baraza la usalama la Umoja wa mataifa limehimiza makubaliano ya kuweka chini silaha yaheshimiwe haraka. Muswada wa azimio uliowasilishwa na Urusi umezitaka pande zote zinazohasimiana zitekeleze makubaliano yaliyofikiwa wiki iliyopita mjini Minsk. Tayari Wanadiplomasia wa nchi za Magharibi wameliangalia azimio hilo kuwa ni ushindi kwa sababu kwa mara ya kwanza mataifa yote 15 Wachama wa Baraza la Usalama wameyatambua matokeo ya mkutano wa Kilele wa...
RAIS wa Marekani BARACK OBAMA amesema hakubaliani na uamuzi wa Jaji wa Mahakama nchini humo wa kusitisha utekelezaji wa amri yake ya utendaji kuhusu mageuzi ya uhamiaji. Bwana OBAMA amesema sheria hiyo na historia viko upande wa utawala wake. Wizara ya Usalama wa Ndani wa nchi hiyo imesema itakata rufaa dhidi ya uamuzi wa mahakama na kwamba utawala umechukua mwelekeo mzuri kwa mujibu na utawala wake wa sheria, lakini imeeleza kuwa kwa sasa itabidi ikubaliane wa uamuzi wa mahakama....
KUNDI la mataifa ya nchi za Magharibi limetaka kuwepo kwa hatua za dharaua kutafuta suluhu ya kisiasa katika mzozo uliopo nchini Libya ambapo makundi hasimu yanang’ang’ania madaraka. Taarifa hiyo kutoka Marekani , Uingereza , Ufaransa , Ujerumani, Italia na Uhispania imejiri baada ya Misri kuomba msaada wa Jeshi la Kimataifa. February 15 mwaka huu Misri imethibitisha kuwa wanamgambo wa Islamic State waliwakata vichwa watu 21 raia wake ambao ni Wakisristo wa madhehebu ya Coptic ...
RAIS wa misri Abdel Fatah Al-Sisi ameutaka umoja wa mataifa kuidhinisha hatua za kijeshi za kimataifa dhidi ya kundi la Islamic State nchini Libya. Akizungumza na kituo kimoja cha radio cha Ufaransa, rais Sisi amesema kuwa watu nchini Libya wanataka hatua kali zichukuliwe ili kuleta usalama na udhabiti nchini mwao. Wito wa rais Sisi unakuja siku moja baada ya ndege za kivita za Misri kushambulia ngome za Islamic State kulipiza kisasi kuuawa kwa wamisri wa dhehebu la Coptic nchini Libya...
VIONGOZI wa Ujerumani, Urusi na Ukraine wamekubaliana hatua muhimu zitakazowezesha kikosi cha kimataifa cha waangalizi , kuangalia utekelezaji wa makubaliano ya kusitisha mapigano mashariki mwa Ukraine. Kansela wa Ujerumani ANGELA MERKEL , Rais VLADIMIR PUTIN na mwenzake wa Ukraine , PETRO POROSHENKO , wamezungumza kwa njia ya simu na kujadili njia za kuwaruhusu waangalizi kutoka Shirika la Usalama na ushirikiano barani Ulaya OSCE kuingia katika mji muhimu wa masuala ya usafiri wa treni wa Debaltseve. Katika eneo la Mashariki mwa...
MAMIA kwa maelfu ya raia wa Denmark wameomboleza vifo vya watu wawili waliouwawa katika mashambulizi mawili tofauti siku ya Jumapili mjini Copenhagen. Jana jioni, watu hao waliwasha mishumaa karibu na mgahawa ambapo kijana mwenye miaka 22 aliwashambulia kwa risasi watu waliokuwa wakihudhuria mjadala kuhusu uhuru wa kutoa maoni. Mtu mmoja alikufa katika tukio hilo na mwingine katika tukio la pili ambapo mshukiwa aliwashambulia kwa risasi watu waliokuwa nje ya sinagogi moja mjini...