KIONGOZI wa Kanisa Katoliki Papa FRANCIS anatarajiwa kuwasili nchini Sri Lanka kesho, wiki moja baada ya Rais aliyekuwapo madarakani kwa muda mrefu nchini humo kushindwa katika uchaguzi. Jamii ndogo ya waumini wa madhehebu ya Katoliki nchini humo inatarajia kwamba Papa FRANCIS anaweza kusaidia kuponya majeraha ya vita vya wenyewe kwa wenyewe vilivyodumu kwa miaka 25 nchini...
WAZIRI wa Mambo ya Kigeni wa Marekani JOHN KERRY amesema anatarajia kwenda mjini Paris wiki hii kwa mazungumzo ya kupambana na makundi yenye itikadi kali yanayotumia nguvu. Bwana KERRY atakuwa nchini Ufaransa siku ya Alhamis na...
RAIS wa Haiti na Wabunge wa Upinzani wanaendelea na mazungumzo, kujaribu kufikia makubaliano ya dakika za mwisho, kutatua mgogoro unaokwamisha uchaguzi katika taifa hilo linalokabiliwa na matatizo. Rais MICHEL MARTELLY na Maafisa wa upinzani wamekuwa katika mvutano kuhusu uchaguzi wa Bunge uliopaswa kuitishwa mwaka...
Umoja wa Mataifa umekemea wimbi la mashambulizi dhidi ya Watu wenye ulemavu wa ngozi, Albino, baada ya tukio la kutekwa kwa mtoto wa miaka minne mjini Mwanza. Mwakilishi wa UN nchini ALVARO RODRIGUEZ ameitaka Serikali ya Tanzania kuzidisha juhudi za kupambana na vitendo vya unyanyapaa dhidi ya...
WANAMGAMBO wa kundi la Boko Haram wameripotiwa kuwauwa watu kadhaa katika mashambulio kaskazini mashariki mwa Nigeria. Nyumba pia zimechomwa katika wimbi la hivi karibuni la mashambulizi katika jimbo la Borno. Hali hiyo imekuja baada ya kundi hilo lenye Itikadi Kali ya Kiislamu kuuteka mji wa Baga mwishoni mwa Juma....
RAIS MPYA wa Sri Lanka MAITHRIPALA SIRISENA anatarajiwa kuapishwa baadaye hii leo. Hatua hiyo inakuja baada ya Rais anayemaliza muda wake, MAHINDA RAJAPAKSA kukubali kushindwa katika uchaguzi mkuu uliofanyika January 08 mwaka...
Mamilioni ya Raia wa Sri Lanka wanapiga kura, uchaguzi ambao unampambanisha Rais wa nchi hiyo MAHINDA RAJAPAKSA na Mshirika wake wa zamani. Bwana RAJAPAKSA,ambaye alikuwa madarakani tangu mwaka 2005, aliitisha uchaguzi miaka miwili iliyopita huku wachambuzi wa mambo wakitabiri kuwa atashinda uchaguzi...
UFARANSA imetangaza leo kuwa ni siku ya maombolezo ya Kitaifa baada ya watu 12 waliouawa katika shambulio la ofisi za jarida la vikaragosi la CHARLIE HEBDO mjini Paris hapo jana. Akizungumza kupitia kituo cha Luninga, Rais FRANCOIS HOLLANDE amesema kuwa Umoja ndiyo silaha kubwa katika kukabiliana na mauaji...
UMOJA WA MATAIFA umesema Rais JOSEPH KABILA ameahidi kuwa jeshi lake litaungana na la UN katika operesheni dhidi ya waasi wa FDLR. Kikosi cha Wanajeshi Elfu 20 wa Umoja huo watashirikiana na wale wa Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo katika kampeni zilizopangwa kuanza karibuni dhidi ya waasi wa Kihutu wa Rwanda. ...
WATUHUMIWA wawili wanaodaiwa kuwaua Wanawake katika nyumba za Kulala wageni wamepandishwa Kizimbani katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu. ABUBAKARY KASANGA anayeishi katika nyumba ya Kulala wageni na EZEKIEL KASENEGELA mkazi wa Tandika jijini Dar es salaam wamefikishwa Mahakamani. Washtakiwa hao wamefikishwa Mahakamani hapo wakikabiliwa na kesi mbili za mauaji huku moja ikiwahusisha wote ambazo zimesomwa mbele ya Mahakimu...
WAZIRI MKUU wa Uingereza DAVID CAMERON na Kansela wa Ujerumani ANGELA MERKEL wanatarajiwa leo kuzungumzia mipango ya CAMERON kujadili upya uhusiano wa Uingereza na Umoja wa Ulaya. Ziara ya MERKEL jijini London ni sehemu ya msururu wa safari katika Mataifa kadhaa ya Kigeni ili kuweka mambo sawa kabla ya mkutano wa kilele wa kundi la Mataifa Saba yenye nguvu Kiuchumi Ulimwenguni – G7 ambao atauandaa Mnamo Juni 7 na 8 mjini Munich....