IMEELEZWA kuwa Mkia wa ndege ya Air Asia iliyoanguka umepatikana kwenye bahari ya Java, baada ya kikosi kilichokuwa kikiisaka ndege hiyo. Mkia huo wa ndege hutunza Visanduku vyeusi vinavyorekodi Mawasiliano ndani ya ndege ambavyo vingeweza kuwasaidia wachunguzi kubaini chanzo cha ajali....
MSHAMBULIAJI wa Kike wa kujitoa muhanga amejilipua na kumuua Afisa wa Polisi wa Uturuki na kumjeruhi mwingine katika shambulizi lililofanywa katika Wilaya Mashuhuri kwa watalii ya Sultanahmet mjini Istanbul. Serikali imelaani shambulizi hilo ambalo ni la Pili kufanywa dhidi ya Polisi na kuutikisa mji wa Istanbul katika kipindi cha wiki...
RAIS BARACK OBAMA anakutana na Rais wa MEXICO ENRIQUE PENA NIETO katika Ikulu ya Marekani na akitafuta msaada wa utekelezaji wa mabadiliko ya sera zake kuhusiana na uhamiaji pamoja na Cuba. Bwana OBAMA anamtaka Bwana PENA NIETO kujiunga naye kuishinikiza Cuba kufanya mageuzi ya Kidemokrasia wakati ambapo Ikulu ya Marekani inachukua hatua za kurejesha Mahusiano ya Kidiplomasia na...
WAKATI UGONJWA wa maradhi ya Ebola ukiendelea kuwa tishio katika baadhi ya nchi Afrika Magharibi, Wataalam wa Afya nao wameendelea kuweka jitihada zaidi kuhakikisha kuwa wanaumaliza ugonjwa huo. Katika jitihada zao hivi sasa wamebuni mpango wa mawasiliano ya simu ya mkononi wenye mpango maalum inayotoa taarifa kutoka maeneo yaliyokumbwa na...
PAKISTAN imeishutumu India kwa mauaji ya Raia wake Wanne katika mpaka wa nchi hizo mbili huku India ikisema mlinzi wa mpakani ameuwawa katika hatua inayoongeza hali ya wasiwasi kabla ziara ya Rais wa Marekani BARACK OBAMA baadaye mwezi huu. India imesema imewaua Wapakistan Wanne waliokuwa wakipanga kufanya shambulizi katika ardhi yake, ingawa vyombo vya Habari vya India na Vyama vya Upinzani vinahoji taarifa hiyo rasmi....
WAPIGANAJI wa Kikurdi wamesonga mbele katika mji wa Kaskazini wa Syria wa Kobane na kudhibiti eneo muhimu lenye majengo ya Serikali baada ya mapigano na wanamgambo wa kundi la Dola la Kiislamu. Kwa mujibu wa Afisa wa Mji wa Kobane IDRISS HASSAN na Shirika la Haki za Binadamu la Syria vikosi vya wakurdi wa Syria wameliteka eneo hilo la usalama kunakopatikana pia makao makuu ya...
Umoja wa Mataifa umeahirisha mazungumzo ya Amani baina ya pande zinazolumbana nchini Libya ambayo yamepangwa kufanyika leo, bila kutangaza tarehe mpya. Mazungumzo hayo yamepangwa kufanyika Desemba 9 lakini yamekuwa yakicheleweshwa mara kwa mara kutokana na kuongezeka kwa mapigano kati ya Serikali dhaifu inayotambulika Kimataifa na wapiganaji wanaoungwa mkono na makundi ya Kiislamu. Msemaji wa ujumbe wa Umoja wa Mataifa SAMIR GHATTAS amesema kuwa juhudi zinaendelea kufanyika ili kuyaanda mazungumzo...
RAIS WA UFARANSA FRANCOIS HOLLANDE amesema kuwa vikwazo vya nchi za Magharibi vinavyoendelea kuiathiri Urusi vinapaswa kuondolewa kama hatua zitapigwa katika ufumbuzi wa mgogoro wa Ukraine. HOLLANDE amekiambia kituo kimoja cha Radio nchini Ufaransa kuwa anatarajia kupatikana mafanikio katika mazungumzo ya Kimataifa yanayopangwa nchini Kazakhstan mnamo Januari 15 katika juhudi mpya za kushinikiza mpango wa amani, ambapo kiongozi wa Ukraine anayeungwa mkono na nchi za Magharibi Rais PETRO POROSHENKO anatarajiwa kukutana na Rais VLADMIR PUTIN wa...
WATU WANNE wameuwawa katika shambulizi la bomu lililotegwa kwenye gari karibu na Uwanja wa ndege wa Kimataifa katika mji Mkuu wa Somalia, Mogadishu. Afisa wa Polisi amesema mshambuliaji amegongesha gari lililosheni mabomu na gari jingine na kusababisha mlipuko ulioutikisa mji wa Mogadishu na kusikika katika maeneo mengine ya mji huo. Msemaji wa Kitengo cha Kijeshi cha kundi la Al Shabab lenye mafungamano na mtandao wa Kigaidi wa Al Qaeda, Sheikh ABDUL AZIZ MUSAB amethibitisha wanamgambo wa kundi hilo kufanya hujuma...
RAIS WA MAMLAKA ya ndani ya Wapalestina MAHMOUD ABBAS amesema Wapalestina watawasilisha tena kwa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa azimio litakaloiwekea Israel muda wa miaka mitatu kuondoka katika maeneo ya Wapalestina. Azimio hilo limekataliwa wiki iliyopita huku wanachama Nane kati ya 15 wa Baraza la Usalama wakipiga kura kuliunga mkono. Akizungumza katika ufunguzi wa maonesho kuhusu mji wa Jerusalem mjini Ramallah Rais ABBAS amesema hawajashindwa katika baraza la usalama, bali baraza hilo ndilo lililoshindwa kutimiza wajibu wake kwa...
WAZIRI MKUU wa Jimbo kubwa zaidi nchini India la Uttar Pradesh amewafuta kazi Polisi wawili wanaoshutumiwa kumteka nyara na kumbaka Msichana wa umri wa Miaka 14. AKHILESH YADAV ameamrisha hatua za kinidhamu kuchukuliwa dhidi ya polisi hao . Mahakama imesema kuwa polisi wamemlazimisha Msichana huyo kuingia ndani ya gari lao alipotoka nyumbani kwenda Msalani...