Global News

UGANDA: USHAHIDI WA VIDEO WABADILI KESI KUWA JARIBIO LA MAUAJI
Global News

POLISI Nchini Uganda wamebadilisha mashtaka ya mfanyakazi wa nyumbani aliyenaswa kwa kamera akimpiga na kumtendea unyama mtoto wa mwaka mmoja na nusu, kutoka kosa la kutesa na sasa anakabiliwa na kosa la jaribio la mauaji. Video hiyo iliyowaudhi watu wengi kwenye mitandao ya kijamii lakini baba wa mtoto huyo amesema walisambaza video hiyo ili kuwatahadharisha wazazi wengine. Mfanyakazi huyo wa nyumbani Jolly Tumuhirwe, alikuwa amezuiliwa katika gereza la Luzira na mahakama ya Nakawa kwa kosa la kutesa chini ya kifungo...

Like
314
0
Monday, 24 November 2014
SERIKALI YA MPITO BURKINA FASO KUFANYA MKUTANO WA KWANZA LEO
Global News

SERIKALI mpya ya mpito nchini Burkina Faso itakuwa na mkutano wa kwanza leo hii huku jeshi likishikilia nyadhifa muhimu Serikalini ikiwa ni Wiki tatu baada ya Jeshi kuchukuwa madaraka kufuatia kun’gatuka kwa Rais wa nchi hiyo kutokana na uasi wa umma. Kiongozi mwenye nguvu jeshini Luteni Kanali ISAAC ZIDA ataendelea kushikilia wadhifa wa Waziri Mkuu na Waziri wa Ulinzi. Katibu Mkuu wa Serikali hiyo mpya ALAIN THIERRY OUATTARA ametangaza kwamba jeshi, pia litadhibiti Wizara ya mambo ya ndani.  ...

Like
302
0
Monday, 24 November 2014
JESHI LA KENYA LAFANYA MASHAMBULIZI KWENYE KAMBI YA AL SHABAB
Global News

WANAJESHI nchini Kenya wamewashambulia na kuwaua zaidi ya wanamgambo 100 wa Al Shabaab na kuharibu Kambi yao nchini Somalia. Mashambulizi hayo yamekuja baada ya Wapiganaji wa kundi hilo kuvamia basi moja lililokuwa likisafiri kwenda Nairobi kutoka Mandera na kuwaua abiria 28 kati ya 60 waliokuwemo. Naibu Rais WILLIAM RUTO amesema kuwa majeshi ya Kenya yamefanya operesheni mbili ambazo zimefanikiwa ambapo mbali na vifo hivyo, pia magari Manne yaliyokuwa na silaha yameharibiwa na kambi yao kuteketezwa....

Like
387
0
Monday, 24 November 2014
WAJERUMANI 550 KUJIUNGA NA WANAMGAMBO WENYE ITIKADI KALI SYRIA NA IRAQ
Global News

MKUU WA SHIRIKA la kitaifa la ujasusi nchini Ujerumani HANS GEORGE MAASSEN amesema Maafisa wa Usalama nchini humo wanawafahamu watu 550 kutoka Ujerumani ambao wamesafiri kuelekea Syria na Iraq kujiunga na makundi ya wanamgambo wenye itikadi kali na kiasi cha watu sitini kati yao wameshakufa. Akihojiwa na gazeti linalochapishwa kila Jumapili la Welt am Sontag, Bwana MAASSEN amesema watu hao Sitini wameuawa au kujitoa Muhanga katika mashambulizi. Maafisa wa usalama Ujerumani na nchi nyingine za bara la Ulaya wamekuwa na...

Like
548
0
Monday, 24 November 2014
WANANCHI WA TUNISIA KUFANYA MAAMUZI MAGUMU LEO
Global News

WANANCHI wa Tunisia leo wanapiga kura katika uchaguzi wa kwanza wa Rais tangu kutokea vuguvugu la mapinduzi mwaka 2011. Mapinduzi hayo yalisababisha vuguvugu hilo la mabadiliko katika nchi nyingine za Kiarabu. Miongoni mwa wagombea katika kinyang’anyoro hicho ni mwanasiasa mkongwe Beji Essabsi, aliyewahi kushika nafasi muhimu wakati wa utawala kabla ya kutokea mapinduzi. Bwana Beji anayepewa nafasi kubwa ya kushinda uchaguzi huo ameahidi kurejesha kiwango cha juu cha utulivu wa kisiasa na kiuchumi....

Like
332
0
Monday, 24 November 2014
POLISI KENYA WALINDA BARABARA MOMBASA
Global News

POLISI waliojihami wanaendelea kushika doria katika barabara za mji wa Mombasa Pwani ya Kenya hata baada ya maombi ya Ijumaa Hii ni baada ya vurugu kati ya polisi hao na vijana baada ya kufanya msako katika baadhi ya misikiti mjini humo. Misikiti ambayo ilifanyiwa msako ambako inaaminika mafunzo ya itikadi kali za kidini inafanyika, ni Swafaa na Minaa. Polisi wanadai kuwa misikiti hiyo hutoa mafunzo ya itikadi kali ikilenga kuwaunga mkono wapiganaji wa kiisilamu nchini Somalia Al Shabaab....

Like
261
0
Friday, 21 November 2014
11 WAFARIKI KWA KUKANYAGANA ZIMBABWE
Global News

WATU 11 wamefariki katika mkanyagano nchini Zimbabwe baada ya ibada ya kidini kufanyika katika uwanja wa soka. Polisi wanasema kuwa watu wanne wamefariki katika uwanja huo ulio mjini Kwekwe wakati wengine saba wakifariki hospitalini. Mkanyagano huo ulitokea wakati maelfu ya waumini wakikimbilia kuondoka uwanjani humo baada ya ibada iliyoongozwa na mhubiri wa kipentekoste Walter Magaya...

Like
335
0
Friday, 21 November 2014
KERRY KUWAKILISHA MAREKANI KUZUNGUMZIA NYUKLIA IRAN
Global News

WAZIRI WA MAMBO ya Nje wa Marekani, JOHN KERRY, amewasili mjini Vienna, Austria, kushiriki Kongamano la Mataifa Sita yenye nguvu Duniani na Iran juu ya mpango wa nyuklia wa Iran. Msemaji wa Wizara hiyo, JENIFFER PSAKI, amesema bado haijafahamika lini Waziri huyo ataondoka Vienna kurejea Washington, huku timu za wapatanishi zikipigania kupatikana kwa makubaliano na Iran kabla ya muda wa mwisho siku ya Jumatatu ijayo. Taarifa zaidi zimeleeza kuwa ikiwa makubaliano hayo yatafikiwa, mkwamo wa Miaka 12 kwenye mpango wa...

Like
300
0
Friday, 21 November 2014
REPUBLICAN YATISHIA KUCHUKUA HATUA DHIDI YA OBAMA
Global News

RAIS BARACK OBAMA amelihutubia taifa kueleza mageuzi makubwa katika mfumo wa uhamiaji wa Marekani. Amesema atachukua hatua za kikatiba kutoa ruhusa ya muda kisheria kwa takriban wahamiaji haramu Milioni Tano. OBAMA amesema nchi hiyo imejengwa kwa uhamiaji na ameshutumu wanachama wa Republican kwa kuzuia mageuzi hayo pia Wanachama hao wametishia kuchukua hatua. Amebainisha kuwa watakaohalalishwa watalazimika kulipa kodi na wasiwe na rekodi ya uhalifu hata hivyo amesema urejeshwaji makwao kwa watu wenye makosa utaharakishwa....

Like
265
0
Friday, 21 November 2014
EBOLA YACHUKUA 5420 DUNIANI KOTE
Global News

SHIRIKA la Afya Duniani –WHO, limesema watu wapatao 5,420 wameshapoteza maisha hadi sasa kutokana na ugonjwa wa Ebola kati ya wagonjwa 15,145 walioambukizwa tangu Disemba mwaka jana. Ijumaa iliyopita, shirika hilo lilikuwa limeripoti kwamba waliokufa walikuwa 5,177 na walioambukizwa walikuwa 14,413. WHO inaamini kuwa idadi halisi ya vifo inaweza kuwa zaidi ya hapo, kwa kuzingatia kwamba asilimia 70 ya wanaoambukizwa hupoteza...

Like
284
0
Thursday, 20 November 2014
BILIONI 10 KUKUSANYWA KUSAIDIA NCHI MASIKINI
Global News

WAFADHILI wa Kimataifa wameanza mkutano wao leo mjini Berlin, Ujerumani, unaolenga kukusanya dola bilioni 10 kwa ajili ya Mfuko wa Mabadiliko ya Tabia Nchi, ambapo Mataifa 22 duniani yanatazamiwa kuhudhuria mkutano huo. Lengo la mfuko ulioanzishwa na Umoja wa Mataifa ni kuzisadia nchi masikini ili kupunguza utoaji wa hewa chafu na kujitayarisha na athari za kupanda kwa joto ulimwenguni. Mkuu wa Kitengo cha Mabadiliko ya Tabia Nchi cha Umoja wa Mataifa, Christiana Figueres, ametoa wito kwamba angalau mtaji wa dola...

Like
281
0
Thursday, 20 November 2014