KIONGOZI wa mpito wa Burkina Faso ametupilia mbali muda wa wiki mbili wa kukabidhi madaraka uliotolewa na Umoja wa Afrika wa kukabidhi madaraka kwa Raia. Luteni Kanali Isaac Zida amesema haogopi vikwazo , na kuwa wanajali zaidi kuhusu uimara wa nchi yao.Zida alifanya mazungumzo na upinzani na asasi za kiraia na kukubaliana kuitisha uchaguzi mwakani. Jeshi lilishika madaraka baada ya kifo cha Rais Blaise Compaore ambaye alishinikizwa kujiuzulu baada ya kutokea maandamano wiki iliyopita. ...
UTATA umetanda miongoni mwa wananchi nchini Marekani kutaka kujua ni askari yupi hasa aliyefyatua risasi iliyomuua Osama Bin Laden, zaidi ya miaka mitatu baada ya kifo cha kiongozi huyo wa kundi la kigaidi la al-Qaeda, baada ya kuibuka madai mbalimbali. Askari wa zamani wa kikosi cha Seal cha wanamaji wa Marekani, Robert O’Neill, mwenye umri wa miaka 38, ameliambia gazeti la Washington Post katika mahojiano mapya kuwa ndiye alifyatua risasi iliyomuua Osama. Maelezo hayo yanapingana na yale ya Matt Bissonnette,...
TAKWIMU zinaonyesha kuwa ukame umekuwa na madhara makubwa katika mji mkubwa nchini Brazil wa Sao Paulo. Dokta ANTONIO NOBRE ambaye ni Mtaalamu wa hali ya Hewa amesema vyanzo vya maji vinaweza kutoweka na kusababisha madhara kwa zaidi ya watu Milion 20 iwapo hali hiyo ya uharibifu katika msitu wa Amazon hautadhibitiwa. Baada ya kuwa ndani ya ukame kwa zaidi ya miaka nane mfululizo kina cha maji kwa sasa mjini Sao Paulo kipo katika hali ya hatari. Serikali nchini humo...
RAIS BARACK OBAMA wa Marekani ameliomba Bunge la nchi hiyo Dola Bilioni 6 nukta 2 kwa ajili ya Mfuko wa Dharura wa kupambana na maradhi ya Ebola katika eneo la Magharibi mwa Afrika, na kuzuia uwezekano wa Ugonjwa huo kusambaa hadi Marekani. Sehemu ya mfuko huo Dola Bilioni Mbili zinatarajiwa kukabidhiwa kwa Shirika la Marekani la Msaada wa Kimataifa – USAID, huku Dola Bilioni 2 nukta 4 zikienda Idara ya Afya na Huduma za Binadamu nchini humo. Taarifa zaidi zimebainisha...
WASIMAMIZI wa Vyuo Vikuu nchini Kenya wameagizwa kufungua Mitandao ya Twitter na Facebook ambayo wanafunzi watatumia kutoa malalamiko yao kwa lengo la kuzuia machafuko katika Taasisi hizo. Waziri wa Elimu nchini Kenya JACOB KAIMENYI amesema kuwa vifaa hivyo vya mawasiliano vitawasaidia wanafunzi kutoa malalamiko yao mbali na kupata majibu kutoka kwa Wasimamizi. Waziri KAIMENYI ameshtumu mbinu zinazotumiwa na Vyuo Vikuu kukandamiza upinzani mbali na kudhibiti masuala ya wanafunzi kama vile Uchaguzi wao na kuwasingizia katika masuala ya utovu wa...
VYAMA vya siasa nchini Burkina Faso vimekubaliana kuwa na uchaguzi mkuu mwezi Novemba 2015 ikiwa ni harakati za kurejesha utawala wa kiraia na demokrasia.. Hata hivyo mazungumzo hayo yameisha bila kuwa na ufumbuzi kuhusiana na nani atakayekuwa kiongozi wa mpito hadi kufikia muda wa kufanyika kwa uchaguzi mkuu wa nchi hiyo kufuatia kuangushwa kwa aliyekuwa rais wa taifa hilo la Afrika Magharibi Blaise Compaore. Jeshi la nchi hiyo limekuwa likishikilia madaraka tangu aondolewe madarakani kiongozi huyo kutokana na maandamano ya...
WANAJESHI kutoka nchini Libya wamerejeshwa nchini kwao kutokana na kukosa uadilifu wakiwa mafunzoni Uingereza huku wengine wakituhumiwa kufanya vitendo vya ukatili wa kimapenzi. Wanajeshi hao waliokuwa mafunzoni nchini Uingereza, 300 kati yao wamesharejeshwa Libya kutokana na tuhuma kuhusiana na unyanyasaji wa kimapenzi. Waziri wa Ulinzi wa Libya amethibitisha kurejeshwa kwa askari hao na kuongeza kuwa wengine watarejeshwa siku chache zijazo. wanajeshi wawili wa Libya wamekiri kufanya vitendo vya unyanyasaji wa kingono dhidi ya wanawake huko...
POLISI nchini Israel wamepambana na vijana wa Kipalestina waliokuwa wakirusha mawe ndani ya uwanja wa msikiti wa Al-Aqsa leo baada ya makundi ya Wayahudi wenye msimamo mkali kutangaza mipango ya kuzuru eneo hilo licha ya wiki kadhaa za hali ya wasi wasi. Ziara hiyo iliyopangwa na kundi la Wayahudi ikiwa ni pamoja na wanasiasa wa siasa za kizalendo zaidi ilikuwa ifanyike wiki moja baada ya jaribio la mauaji dhidi ya mmoja kati ...
MATOKEO ya awali ya uchaguzi mdogo nchini Marekani yanaonesha kuwa chama cha Republican kimechukua udhibiti wa baraza la Seneti kwa kupata kiasi ya viti 51 katika baraza hilo lenye viti 100. Pia chama hicho kinaelekea kupata ushindi wa kishindo katika baraza la wawakilishi kwa miongo kadhaa. Warepublican wamefaidika na wimbi la kutoridhika kwa wapiga kura na kutoa pigo kwa rais Barack Obama ambalo litapunguza uwezo wake wa kupitisha ajenda ...
AFISA wa Umoja wa Mataifa anayehusika na mapambano dhidI ya maradhi ya Ebola, ameionya jumuiya ya kimataifa isilegeze kamba katika harakati za kuyatokomeza maradhi hayo hatari. Akizungumza baada ya kukutana na rais wa Liberia Ellen Johnson Sirleaf mjni Monrovia, afisa huyo Anthony Banburry amesema ingawa zipo dalili za kupungua kwa maambukizi ya ugonjwa huo, kila mtu anapaswa kuendelea kuwa makini. Banburry amesema Umoja wa Mataifa umejenga vituo vya kupambana na Ebola, na inahitaji watu wa kujitolea kuviendesha vituo hivyo. Wakati...
MAREKANI imesema itapeleka rasimu ya maazimio ndani ya Baraza la usalama la Umoja wa Mataifa kuweka vikwazo dhidi ya Watu wanaozorotesha hali ya kisiasa nchini Sudani Kusini. Rais wa Baraza la usalama la Umoja wa Mataifa ambaye ni Rais wa Australia amesema baadhi ya wanachama wa baraza hilo wanaunga mkono hatua ya kuwekewa vikwazo na kuzuia biashara ya silaha. Haijajulikana ni lini hatua hiyo itatekelezwa. Lakini Mapigano yameendelea nchini Sudani Kusini ,ingawa kumekuwa na jitihada za kimataifa kuhakikisha makubaliano ya...