Global News

WAMAREKANI WASHIKA MPINI WA BARAZA LA SENETI
Global News

WAPIGA kura nchini Marekani wanashiriki katika uchaguzi, utakaoamua ni chama gani kitalidhibiti baraza la Seneti na kutoa sura ya muelekeo wa rais BARACK OBAMA katika kipindi cha miaka miwili iliosalia ya utawala wake. Bwana OBAMA binafsi amesema anauangalia uchaguzi huo kuwa kipimo cha maoni ya wamarekani kuhusu sera zake. Wagombea wa chama cha Republican wana matumaini kwamba kuvunjwa moyo kwa wapiga kura na sera za Bwana OBAMA kutawapa fursa ya kulidhibiti baraza la Seneti. Kuna viti 36 kati ya100 vinavyogombewa...

Like
321
0
Tuesday, 04 November 2014
UNHCR KUTOA URAIA KWA WATU MILIONI 10 ULIMWENGUNI
Global News

SHIRIKA la Umoja wa Mataifa la kuhudumia Wakimbizi – UNHCR limeanzisha kampeni inayolenga kumaliza tatizo la watu wasio na uraia wa nchi yoyote, ambao kwa mujibu wa shirika hilo wanafikia milioni 10 kote ulimwenguni. Mkurugenzi wa Shirika hilo ANTONIO GUTERRES amesema hali ya watu hao haikubaliki hata kidogo, na kuongeza kuwa lengo ni kuwa tatizo lao liwe limepatiwa ufumbuzi wa kudumu katika muda wa miaka 10. UNHCR imesema kupitia kampeni hiyo inataka kuziangazia changamoto wanazokabiliana nazo watu wasio na uraia...

Like
309
0
Tuesday, 04 November 2014
MELI YA JESHI LA LIBYA YASHAMBULIWA 13 WAUAWA
Global News

MELI ya Jeshi la Libya imeshambuliwa na watu 13 wameuawa katika mapigano makali yaliyoshirikisha ndege na vifaru kati ya jeshi na wanamgambo wenye itikadi kali karibu na mji wa Benghazi. Jeshi la serikali likiungwa mkono na vikosi vitiifu kwa jenerali wa zamani, Halifa Khaftar lilifanya mashambulizi dhidi ya wanamgambo hao. Wakaazi wa eneo hilo wamesema, raia kadhaa wanauhama mji huo,wakiitika wito wa jeshi kuwataka waondoka katika mji huo wa bandari ambako maafisa wa usalama wamesema wanamgambo wa wamejificha baada ya...

Like
401
0
Tuesday, 04 November 2014
DAKTARI MWINGINE AFARIKI KWA EBOLA SIERRA LEONE
Global News

DAKTARI mwingine amekufa kwa ugonjwa wa Ebola nchini Sierra Leone. Daktari huyo ambaye alikuwa muuguzi mkuu katika hospitali ya Kambi kaskazini mwa Siearra Leone ni wa tano kuuawa na ugonjwa huo nchini humo na inaaminika kwamba aliambukizwa Ebola na mgonjwa ambaye alimtibu maradhi mengine, kwa sababu hakuwahi kumtibu mgonjwa mwenye maradhi hayo hatari. Kwa ujumla, wahudumu wa afya wapatao 100 wameuawa na maradhi hayo nchini Sierra Leone. Shirika la Afya Ulimwenguni WHO limesema watu zaidi ya 4,900 wamekufa kutokana na...

Like
325
0
Tuesday, 04 November 2014
JESHI LA BURKINA FASO KUUNDA SERIKALI YA UMOJA WA KITAIFA
Global News

JESHI la Burkina Faso limeapa kuunda serikali ya umoja wa kitaifa baada ya kuimarisha udhibiti wake katika nchi hiyo ya Afrika Magharibi. Vikosi vya usalama hapo jana vimefyatua mabomu ya kutoa machozi na risasi angani ili kuwatawanya waandamanaji wanaopinga hatua ya jeshi kutwaa madaraka baada ya Rais Blaise Compaore kujiuzulu. Majeshi yaliingia katika uwanja maarufu wa Place de la Nation mjini Ouagadougou na kuchukua udhibiti wa makao makuu ya televisheni ya taifa katika hatua ya kuonyesha ubabe, licha ya wito...

Like
313
0
Monday, 03 November 2014
BOMU LAUA 60 PAKISTAN
Global News

WATU 60 wameuawa katika shambulizi la bomu la kujitoa mhanga nchini Pakistan karibu na mpaka na India, ikiwa ni shambulizi baya zaidi la kigaidi kuwahi kutokea nchini humo katika miaka ya hivi karibuni. Makundi kadhaa, likiwemo la Taliban, yamedai kuhusika na shambulizi hilo ambalo liliwajeruhi zaidi ya watu 120, lililotokea karibu na kivuko pekee cha mpaka kati ya Pakistan na India cha Wagah mashariki ya mji wa mashariki mwa Pakistan, Lahore. Shambulizi hilo lilitokea baada ya kukamilika sherehe maalumu za kijeshi...

Like
315
0
Monday, 03 November 2014
LIST YA MARAIS TAJIRI BARANI AFRIKA
Global News

9..Robert Mugambe rais wa Zimbabwe amekuwa madarakani kwa takribani miaka 25 richa ya chaguzi znazofanyika nnchini humo lakini hadi hii leo bado anashikilia madaraka, anautajiri wa dola million kumi 10 za kimarekani 8..General Idrid Deby Itno huyu ni mwanasiasa kutoka Chad ambae amekuwa madarakani toka mwaka 1990, mwezi October mwaka 2006 jarida la Forbes lilitaja Chad kuwa ndio nnchi inayoongoza kwa rushwa duniani.ruzuku Kutoka kwenye mradi wa mafuta wa Chad-Cameroon na bomba la mafuta ambapo fedha zake zilikusudiwa kupambana na...

2
6230
0
Thursday, 30 October 2014
EBOLA: MAAFISA WA AFYA MAREKANI WATOA MWONGOZO MPYA
Global News

Maafisa wa afya wa Marekani wametoa mwongozo mpya juu ya kuwashughulikia matabibu wanaorudi Marekani baada ya kuwahudumia wagonjwa wa Ebola Afrika Magharibi. Mwongozo huo unapendekeza kuwa wanaoshukiwa kuwa katika hatari ya kuwaambukiza wengine watazuiliwa nyumbani kwao; ingawa majimbo tofauti yatakuwa na uhuru wa kutoa mwongozo thabiti zaidi. Katibu mkuu wa umoja wa mataifa amepinga hatua hizo za kuwaweka karantini walioathirika.                     Mlipuko wa ugonjwa wa ebola afrika magharibi...

Like
345
0
Tuesday, 28 October 2014
HOFU YATANDA MAREKANI BAADA YA EBOLA KUINGIA NEWYORK
Global News

Daktari wa Marekani aliyekuwa akiwahudumia wagonjwa wa Ebola Nchini Guinea amepimwa na kukutwa na virusi vya ugonjwa huko katika hospitali  ya Bellevue mjini Newyork. Dr Craig Spencer ambaye ni mmoja kati ya madaktari wasio na mipaka alianza kujisikia maumivu na homa siku chache tu baada ya kurejea Marekani akitokea Afrika Magharibi. Siku ya Alhamisi wiki hii Craig alipelekwa hospitali kwaajili ya vipimo na kisha akatengwa kwa uchunguzi zaidi wa afya yake. Katika taarifa yake kwa vyombo vya habari Meya wa mji...

Like
339
0
Friday, 24 October 2014
MCT YAZINDUA TUZO ZA UMAHIRI ZA UANDISHI WA HABARI
Global News

 BARAZA la habari nchini-MCT kwakushirikiana na Kamati ya maandalizi ya tuzo za Umahiri za uandishi wa habari Tanzania-EJAT, leo imezindua rasmi tuzo hizo ikiwa ni mara ya sita tangu kuanzishwa kwake. Akizungumza na wandishi wa habari Jijini Dar es salaam, kwa niaba ya Mwenyekiti wa Kamati ya maandalizi ya EJAT, Meneja udhibiti na viwango wa MCT, Pili Mtambalike amesema tuzo za mwaka huu zimeongezewa mambo mapya mawili nakufanya jumla ya makundi ya kushindaniwa kuwa 21 kutoka 19. PICHA NI BAADHI...

Like
507
0
Tuesday, 21 October 2014
KAULI YA UN KUHUSU MATUMIZI YA NGUVU KINGONO SUDANI KUSINI
Global News

UMOJA wa  Mataifa  umesema  ubakaji  na  njia  nyingine za matumizi  ya  nguvu yanafanywa  na  pande  zote katika  vita vya  wenyewe  kwa  wenyewe  nchini  Sudan  kusini. Mwakilishi maalumu  wa  Umoja  wa  Mataifa  kuhusu  matumizi  ya  nguvu kingono katika  mizozo  ya  kivita, Zainab Hawa  Bangura, amesema hali  hiyo  imesambaa  mno  ambapo  hadi  mtoto  wa  miaka  miwili alikuwa  miongoni  mwa  wahanga. Mapigano  yalizuka Desemba mwaka  jana  nchini  Sudan kusini baada  ya  miezi ya  hali  ya...

Like
369
0
Tuesday, 21 October 2014