MWANARIADHA wa Afrika Kusini Oscar Pistorius amehukumiwa jela miaka 5 baada ya kupatikana na hatia ya kumuua mpenzi wake Reeva Steenkamp. Hii ni baada ya mwanariadha huyo mlemavu kupatikana na hatia ya mauaji bila ya kukusudia. Jaji aliyetoa hukumu hiyo,Thokozile Masipa,alianza kutoa kauli yake ya mwisho kabla ya kutoa hukumu saa mbili na nusu asubuhi na akasema ni changamoto kubwa kwake kupata adhabu ambayo itaridhisha pande zote kwenye kesi hiyo. Upande wa mashitaka ulitaka mwanariadha huyo kupewa kifungo cha miaka...
KAMPUNI kubwa ya mafuta ya Ufaransa, Total imetangaza kwamba mkurugenzi wake mkuu, Christophe de Margerie ameuawa katika ajali ya ndege iliyotokea katika uwanja wa ndege wa Moscow nchini Urusi. Taarifa zimeeleza kuwa ndege ya binafsi aliyokuwa akisafiria afisa huyo imeanguka kwenye uwanja wa nukovo ulio nje kidogo ya jiji la Moscow. Vyombo vya habari vya Urusi vimesema kuwa ndege hiyo ilikuwa na abiria mmoja tu, pamoja na wahudumu watatu, wote wakiwa raia wa Ufaransa....
RAIS wa Nigeria Goodluck Jonathan amesema mafanikio ya nchi yake dhidi ya maradhi ya Ebola yametokana na imani ya wananchi wa kawaida kwa maagizo yaliyotolewa na serikali, kuwataka wabadili mienendo yao ya kila siku maishani kama vile kusalimiana kwa kupeana mikono, na utaratibu wa mazishi. Amesema serikali yake ilikuwa na wasiwasi kwamba makanisa yangekataa kuitikia wito huo katika suala la komunio ambapo watu wapatao 1,000 wanaweza kushiriki kikombe kimoja. Ameyasifu makanisa kwa kuusimamisha utaratibu huo, na hata ule wa kutakiana...
Mchezaji wa soka nchini India, Peter Biaksangzuala amefariki kutokana na majeraha aliyoyapata baada ya kuanguka vibaya uwanjani akisherehekea bao lake. Mchezaji huyo alikuwa na umri wa miaka 23 na alijeruhi uti wake wa mgongo baada ya kupiga pindu uwanjani akisherehekea bao lake la kusawazisha kw atimu yake Bethlehem Vengthlang FC dhidi ya Chanmari West FC. Biaksangzuala alikimbizwa hospitalini na kufanyiwa upasuaji lakini baadaye alifariki. Mechi hiyo ambapo alipata jerehe la mgongo, ilikuwa mechi muhimu katika ligi ya nchi hiyo. Taarifa...
Shirika la afya duniani linatarajiwa kutangaza rasmi kuwa taifa la Nigeria halina ugonjwa wa bola baadae hii leo, wiki sita baada ya kutoripotiwa kwa visa vya ugonjwa huo . Nchi giyo yenye idadi kubwa ya watu barani Afrika, alipokea sifa tele kwa hatua zake za haraka kukabiliana na Ebola baada ya mwanmadiplomasia Mliberia mwenye ugonjwa huo kwenda Nigeria mwezi Julai. Shirika la afya duniani lilitangaza Senegal kutokuwa tena na Ebola mnamo siku ya Ijumaa. Mlipuko unaoshuhudiwa wa Ebola, umewaua watu...
Rais wa Sudan Kusini, Salva Kiir na aliyekuwa makamu wake waliyehasimiana Riek Machar, leo wamealikwa kuhudhuria uzinduzi wa mazungumzo ya kutafuta muafaka ndani ya chama cha SPLM kinachoongoza taifa hilo lenye machafuko ya kisiasa. Mazungumzo hayo yanatarajiwa kufanyika Arusha chini ya usimamizi wa CCM, chama tawala nchini Tanzania. Endapo mahasimu hao wawili watafika na kukaa meza moja itakuwa ni hatua muhimu katika jitihada ambazo zimekuwa zikifanyika na jumuiya ya kimataifa kupata muafaka wa machafuko yanayoendelea katika taifa hilo changa...
Rais wa Marekani Barack Obama amethibitisha wito wa kulitumia jeshi la nchi hiyo na wale wa akiba iwapo watahitajika kupambana na mlipuko wa ugonjwa wa Ebola Afrika magharibi. Rais Obama amesema wanajeshi hao wataongeza nguvu ya jeshi katika kutoa misaada ya kibinadamu katika eneo hilo. Kundi la kwanza la wanajeshi hao linatarajiwa kupelekwa kusaidia ujenzi wa vituo 17 vya kutolea tiba ya ugonjwa huo, katikati mwa Liberia, moja ya nchi iliyoathiriwa vibaya na ugonjwa huo. Maafisa wa kikosi cha ulinzi...
Jeshi la DRC linasema kuwa watu 26 wameuawa nchini humo katika shambulizi liliofanywa katika mji wa Beni Mashariki mwa nchi. Wengi, wa waliofariki walikuwa raia wakiwemo watoto. Shirika moja la kutetea haki za binadamu, linasema kuwa wapiganaji wa kundi la waasi la Uganda la ADF au Allied Democratic Forces , lilivamia mji huo nyakati za usiku. Kikosi cha Umoja wa Matifa kikishirikiana na wanjeshi wa DRC, kimekuwa kikijaribu kuwatimua waasi hao wa ADF kutoka nchini DRC tangu mwanzoni mwa mwaka...
Mgonjwa mwingine wa Ebola amegundulika huko marekani kwenye hospitali ya jimbo la Texas ambapo kwa mara ya kwanza kisa cha kuwepo kwa ugonjwa huo kiliripotiwa baada ya Thomas Dancun raia wa Liberia kupatiwa matibabu katika hospitali hiyo. Baadae Thomas Dancun alifariki dunia oct 8 akiwa chini ya uangalizi wa wahudumu wa afya kwenye kituo cha Texas Presbyterian mgonjwa huyo ambae jina lake halikutajwa kuna uwezekano mkubwa alipata virusi hivyo wakati akimuhudumia Texas Presbyterian Kwa mujibu wa Daktari David Lakey ambaye ni kamishna wa...
Wapiga kura wanaelekea kwenye vituo vya kupigia kura nchini Musumbiji leo kumchagua rais mpya na wabunge kwenye uchaguzi wenye upinzani mkali tangu taifa hilo lipate uhuru mwaka 1975. Takriban watu 11 wamejiandikisha kupiga kura nchini humo wakiwemo wengine 90,00 wanaoishi mataifa ya kigeni. Zaidi ya watu milioni 10 wamejiandikisha kupiga kura katika uchaguzi wa leo, ambao unaonekana kuwa wa kwanza kidemokrasia tangu nchi hiyo ilipojipatia uhuru wake kutoka kwa Wareno mwaka 1975. Chama tawala, cha Frelimo, ambacho kimekuwa...
Kampuni kubwa zaidi ya kuunda magari, Toyota, imeagiza kurejeshwa kwa magari milioni moja nukta saba kote duniani kutokana na hitilafu ya breki za magari hayo. Kampuni hiyo imesema hitilafu tatu zimetambulika kwenye breki katika miundo mbali mbali za magari ya Toyota ikiwemo muundo wa Lexus. Magari yaliyo ndani na nje ya Japan yote yameathiriwa na hitilafu hizo. Hata hivyo kampuni yenyewe imesema haina habari yoyote kuhusu ajali za magari au watu kujeruhiwa kutokana na hitilafu hizo. Wadadisi wanasema hili ni...