Global News

Uchaguzi wa rais nchini Cameroon wakabiliwa na vurugu
Global News

Ghasia zimezuka katika sehemu za Cameroon zinazotumia lugha ya kiingereza mara baada ya uchaguzi wa rais kuanza nchini humo. Kwa mujibu wa mbunge mmoja katika mji wa Bamenda, watu wawili wameuawa kwa kupigwa risasi. Waandishi wa habari hata hivyo wamearifu kwamba kwenye majimbo ya nchi hiyo ya Afrika ya kati yanayotumia lugha ya Kifaransa zoezi la uchaguzi limeendelea bila ya mushkeli wowote. Rais Paul Biya anawania muhula wa saba huku nchi yake ikiwa inakumbwa na vurugu katika mikoa inayotumia lugha ya Kiingereza....

Like
606
0
Monday, 08 October 2018
Wafungwa wateka gereza Sudan Kusini
Global News

Mamlaka nchini Sudan Kusini inaendelea na mazungumzo dhidi ya wafungwa ambao wamejihami kwa bunduki na visu, na ambao wanashikilia eneo la gereza hilo mjini Juba wakishinikiza kuachiwa huru kwa wafungwa wa kisiasa kama sehemu ya utekelezaji wa ahadi iliyotolewa na Rais Salva Kiir. Wafungwa hao walifanikiwa kuchukua Bunduki na visu kutoka ndani ya ghala la kuhifadhia silaha. Vikosi vya usalama vimelizingira gereza hilo ambalo pia ni makao makuu ya shughuli za wa taifa. Awali Rais Salva Kiir alitoa ahadi kwamba...

Like
662
0
Monday, 08 October 2018
Meng Hongwei: China yathibitisha inamzuia mkuu wa Interpol aliyepotea
Global News

China imethibitisha inamzuia mkuu wa Interpol aliyepotea Meng Hongwei. Beijing imesema alikuwa anachunguzwa na tume ya kupambana na rushwa nchini humo kwa ukiukaji wa sheria. Meng, ambaye pia ni naibu waziri wa wizara ya usalama wa umma China, aliarifiwa kupoeta baada ya kusafiri kutoka mji wa Lyon Ufaransa , kuliko na makao makuu ya Interpol kwenda China mnamo Septemba 25. Interpol imesema imepokea barua ya kujiuzulu kwake mara moja kutoka kwa ofisi ya rais. Familia yake Meng haijawasiliana naye tangu...

Like
558
0
Monday, 08 October 2018
Kavanaugh akaribia kupitishwa jaji Mahakama ya Juu
Global News

Kuna uwezekano mkubwa wa baraza la Seneti kumpitisha mteule wa Rais Donald Trump kwa nafasi ya jaji wa Mahakama ya Juu ya Marekani, Brett Kavanaugh, licha ya shutuma za mashambulizi ya ngono dhidi yake. Katika hatua inayoonekana kama mafanikio makubwa kwa Rais Trump, wajumbe kadhaa wa Seneti walionesha uungaji mkono wao kwa uteuzi wa Jaji Kavanaugh, hata kutoka kundi la wabunge wa Democrat. Seneta Susan Collins wa Republican na Joe Manchin wa Democrat walikuwa wa mwanzo kupiga kura za kumpitisha...

Like
420
0
Saturday, 06 October 2018
Dk. Mukwege na Murad washinda Tuzo ya Nobel ya Amani
Global News

Daktari raia wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, Dennis Mukwege na mwanaharakati kutoka jamii ya Wayazidi, Nadia Murad, wameshinda Tuzo ya Nobel ya Amani, 2018 kwa jitihada zao za kupambana na unyanyasaji wa kingono. Tangazo la ushindi wa Dk. Mukwege na Murad wa Tuzo ya Nobel limetolewa na mwenyekiti wa kamati ya tuzo hiyo Berit Reiss-Andersen mjini Oslo muda mchache uliopita. Bi Reiss Andersen amesema wote wawili wamekuwa nembo ya mapambano dhidi ya janga la unyanyasaji wa kingono, ambalo limeenea...

Like
515
0
Saturday, 06 October 2018
Diane Rwigara na mamake waachiliwa huru na mahakama Rwanda
Global News

Mahakama Kuu mjini Kigali imeamua kumuachilia huru kwa dhamana mwanasiasa wa upinzani Diane Rwigara na mamake na watafuatiliwa wakiwa nje ya gereza. Jaji wa mahakama kuu mjini Kigali ametangaza kwamba maombi yao ya dhamana yamekubaliwa lakini wakawekewa masharti ya kukabidhi pasipoti zao kwa mwendesha mashitaka. Aidha wametakiwa kutovuka mipaka ya jiji la Kigali bila kibali...

Like
409
0
Friday, 05 October 2018
Pence adai China inaingilia Siasa za Marekani
Global News

Pence amesema China imeanzisha njama ya kutaka kushawishi visivyo maoni ya Wamarekani, kuingilia chaguzi za majimbo zinazofanyika hivi karibuni na kuweka mazingira hasi kuelekea uchaguzi wa urais wa mwaka 2020. Makamu huyo wa Rais wa Marekani ameendelea kusema China inatumia nguvu zake kwa njia isiyokuwa na mfano kuingilia sera na siasa za Marekani. Akizungumza katika taasisi ya utafiti ya Hudson, Pence amesema utawala wa Trump unafanya kazi na ni jambo ambalo Wachina wamepania kulihujumu kwa kutaka kuwepo Rais mwingine mbali...

Like
400
0
Friday, 05 October 2018
Tetemeko Indonesia: Shughuli ya kuwatafuta manusura kusitishwa Ijumaa, Rais Joko Widodo azuru Sulawesi
Global News

Mamlaka nchini Indonesia imesema kuwa ifikapo Ijumaa ya Oktoba 5 itasitisha utafutwaji wa manusura wa tetemeko na tsumani iliyotokea mwishoni mwa juma lililopita katika kisiwa cha Sulawesi. Takriban watu 1400 wamefariki, lakini maofisa wanasema idadi inatarajiwa kuongezeka zaidi. Rais wa Indonesia Joko Widodo ametembelea kwa mara ya pili kisiwa hicho na kusema juhudi za utafutwaji wa manusura zinaridhisha. Misaada inaingia katika maeneo yaliyoathirika kupitia uwanja wa ndege wa Palu licha ya kuwa nao uliharibika kwa kiasi. Baadhi ya wahanga wa...

Like
505
0
Thursday, 04 October 2018
Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kuingia DRC kukabiliana na Ebola
Global News

Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa linafanya ziara ya dharura kuelekea Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo kufuatia mapigano makali nchini humo ambayo yametatiza jitihada za kudhibiti kuzuka kwa virusi vya Ebola. Baraza hilo lenye wanachama 15 pia imeonya kuenea kwa Ebola kwa nchi za jirani na kuifanya kuwa vigumu zaidi kudhibiti. Ugonjwa huo umeua watu zaidi ya mia moja tangu Agosti 1. Mapigano makali kati ya makundi yaliyojihami katika mji wa Beni Mashariki mwa nchi yamewalynga pia wahudumu wa...

Like
397
0
Thursday, 04 October 2018
Theresa May ahimiza mshikamano ndani ya chama chake
Global News

Theresa May amekitolea wito chama chake cha Conservative kumuunga mkono na kuiunganisha Uingereza. May amewataka wanachama hao kuunga mkono mpango wake kuhusu mchakato wa Uingereza kujiondoa kwenye Umoja wa Ulaya Waziri Mkuu wa Uingereza, Theresa May amekitolea wito chama chake cha Conservative kumuunga mkono na kuiunganisha Uingereza ambayo imegawanyika kutokana na tofauti za maoni zilizochochewa na mpango wake wa Uingereza kujiondoa kwenye umoja wa Ulaya. Akizungumza mjini Birmingham katika hotuba yake ya kuufunga mkutano mkuu wa mwaka wa...

Like
569
0
Thursday, 04 October 2018
Redoine Faid: Mhalifu sugu akamatwa miezi 3 baada ya kutoroka jela akitumia helikopta Ufaransa
Global News

Redoine Faid, mhalifu sugu raia wa Ufaransa ambaye alitoroka jela akitumia helikopta iliyokuwa imetekwa nyara amekamatwa tena na polisi. Mhalifu huyo aliyekuwa akitafutwa sana nchini Ufaransa, alishikwa kaskazini mwa Paris, akiwa na ndugu yake na wanaume wengine wawili kwa mujibu wa ripoti. Faid, 46, amejiita kuwa shabiki wa filamu za uhalifu, ambazo anasema zimemfundisha jinsi ya kufanya uvamizi. Kwanza alishikwa mwaka 1998 kwa wizi ya mabavu. Kutoroka kutoka jela mwezi Julai ilikuwa ndiyo mara ya pili amefanya...

1
546
0
Wednesday, 03 October 2018