Global News

MAZUNGUMZO YA KUSULUHISHA MZOZO WA BURUNDI KUANZA TENA LEO KAMPALA
Global News

MAZUNGUMZO ya kusuluhisha mzozo wa Burundi yataanza tena leo mjini Kampala, chini ya usimamizi wa rais Yoweri Museveni wa Uganda.   Rais Museveni aliteuliwa na Jumia ya Afrika Mashariki kuongoza mchakato wa amani ya Burundi, kufuatia machafuko yaliozushwa na uamuzi wa rais Pierre Nkurunziza kupigania muhula wa tatu, kinyume cha maana ya mapatano ya Arusha na katiba ya Burundi inayoruhusu mihula miwili.   Baada ya kuzinduliwa rasmi mjini Kampala leo, mazungumzo hayo yatahamishiwa Arusha...

Like
239
0
Monday, 28 December 2015
WASHUKIWA WA UGAIDI WANASWA PARIS
Global News

WANAUME wawili wamekamatwa kuhusiana na jaribio la shambulizi la kigaidi karibu na eneo la Orleans kusini mwa mji mkuu wa Ufaransa, Paris. Polisi imesema washukiwa hao walipanga kufanya mashambulizi yanayolenga asasi za kiusalama. Waziri wa mambo ya ndani wa Ufaransa Bernard Cazeneuve amesema mashambulizi hayo yaliyotibuliwa na shirika la ujasusi la Ufaransa, yalikusudia kuwalenga maafisa wa usalama katika eneo la...

Like
313
0
Wednesday, 23 December 2015
KIKOSI MAALUM CHA JESHI LA IRAQ KIMEFANYA MASHAMBULIZI DHIDI YA IS
Global News

KIKOSI maalumu cha jeshi la Iraq cha kupambana na ugaidi kimeingia katikati mwa mji wa Ramadi unaodhibitiwa na wanamgambo wenye itikadi kali wa kundi la Dola la Kiislamu IS Msemaji wa jeshi Sabah al Numani, amesema kikosi hicho maalumu hakikukumbana na upinzani mkali isipokuwa mashambulizi machache kutoka kwa washambuliaji wa kujitoa muhanga katika juhudi za kuukomboa mji huo mkuu wa jimbo la Anbar kutoka kwa IS. Taarifa za kiusalama zinaarifu kuwa huenda kuna kati ya wanamgambo 250 hadi 300 wa...

Like
240
0
Wednesday, 23 December 2015
SHIRIKA LA AMNESTY INTERNATIONAL YAITUHUMU BURUNDI
Global News

SHIRIKA la kutetea haki za Binadamu Duniani la Amnesty International, limeituhumu serikali ya Burundi kwa mauaji ya watu wasio na hatia na matumizi mabaya ya Jeshi la nchi hiyo. Aidha limelaani mauaji yaliyotokea Disemba 11 mwaka huu ambapo watu nane waliuawa wakati jeshi la serikali lilipokuwa likijihami dhidi ya mashambulizi ya waasi watatu waliovamia vituo vitatu tofauti vya Jeshi. Hata hivyo Serikali ya Burundi imeeleza kwamba wale waliouawa ni maadui, ingawa maelezo hayo yamepingwa vikali na Amnesty ambao wamesema kuwa...

Like
205
0
Tuesday, 22 December 2015
UGAIDI: WATOTO MILIONI MOJA WAACHA MASOMO
Global News

SHIRIKA la umoja wa Mataifa linaloshughulikia masuala ya watoto-UNICEF- limesema kuwa mashambulizi kutoka kwa wanamgambo wa Boko Haram nchini Nigeria na kwenye nchi zingine yamesababisha zaidi ya watoto milioni moja kuacha masomo. Katika ripoti mpya, iliyotolewa na shirika hilo imeeleza kuwa mamia ya shule nchini humo zimeshambuliwa, kuporwa na kuchomwa moto wakati wa mzozo huo ambao umedumu kwa kipindi cha miaka sita. Licha ya Amri ya rais mpya wa Nigeria Muhammadu Buhari kwa makamanda wake wa jeshi kuzuia mashambulizi ya...

Like
199
0
Tuesday, 22 December 2015
UMOJA WA ULAYA WAONYESHA MATUMAINI HISPANIA
Global News

RAIS wa halmashauri kuu ya Umoja wa Ulaya Jean-Claude Juncker, amesema kuwa umoja huo una matumaini kwamba hispania itaunda serikali imara, kufuatia uchaguzi ambao waziri mkuu Mhafidhina Mariano Rajoy, amepoteza viti vingi vya Ubunge kwa vyama vya mrengo wa kushoto. Juncker amewambia wandishi wa habari mjini Brussles kuwa amezingatia matokeo ya uchaguzi huo na maelezo ya hisia za Wahispania na kuongeza kuwa zipo juu ya mamlaka ya nchi hiyo katika kuunda serikali inayoweza kutimiza wajibu wake. Hata hivyo vyama vya...

Like
236
0
Tuesday, 22 December 2015
AFGHANISTAN: SHAMBULIO LA KUJITOA MUHANGA LAUA ASKARI 6 WA MAREKANI
Global News

MSHAMBULIAJI wa kujitoa muhanga nchini Afghanistan amewaua askari sita wa vikosi vya Jeshi la Marekani likiwa ni miongoni mwa shambulio baya kuwahi kutokea katika kipindi cha miezi ya hivi karibuni. Mshambuliaji huyo akiwa kwenye pikipiki, amewalenga askari wa vikosi vya muungano kati ya majeshi ya NATO na askari wa doria wa Afghanistan karibu na kambi ya vikosi vya anga. Kamanda wa kikosi kimojawapo cha polisi amesema kwamba yeye na wasaidizi wake pamoja na kikosi cha askari walizingirwa na baadhi ya...

Like
253
0
Tuesday, 22 December 2015
NIGERIA: JESHI LAPEWA MWEZI MMOJA KUISAMBARATISHA BOKO HARAM
Global News

MSEMAJI wa jeshi la Nigeria Kanali Sani Usman, amesema wanajeshi wake wamewauwa wapiaganaji 12 wa kundi la Boko Haram, na kukamata shehena ya silaha na risasi kutoka kwa kundi hilo, ambalo uasi wake wa miaka sita umegharimu maisha ya maelfu ya raia.   Usman amesema wanajeshi waliwaua washukiwa wa ugaidi wa Boko Haram waliokuwa wanazitesa jamii za maeneo ya Sabon Gari na Damboa, na kwamba miongoni mwa waliouawa ni kiongozi wa magaidi hao katika mji wa Bulayaga.   Rais Muhammadu...

Like
333
0
Monday, 21 December 2015
BURUNDI: BUNGE LAJADILI MPANGO WA AU KUPELEKA VIKOSI VYA USALA
Global News

BUNGE la Burundi leo linajadili mpango wa Umoja wa Afrika kutuma kikosi cha wanajeshi wa kuwalinda raia nchini humo, ambao tayari serikali  imeukataa na kukitaja kikosi hicho kuwa ni cha uvamizi. Wabunge wanatarajiwa kupinga kuletwa kwa kikosi hicho, kilichopendekezwa na Umoja wa Afrika wiki iliyopita, wakati ambapo wasiwasi unazidi kuhusu kuongezeka kwa machafuko katika taifa hilo dogo. Chama tawala cha CNDD-FDD kimesema lengo la kikao hicho kisicho cha kawaida kilichotarajiwa kutangazwa moja kwa moja kupitia redio na televisheni za Umma,...

Like
253
0
Monday, 21 December 2015
HISPANIA YASUBIRI MAJIBU YA UCHAGUZI
Global News

CHAMA cha kihafidhina cha nchini Hispania kinachoongozwa na Waziri Mkuu Mariano Rajoy kimeshinda katika uchaguzi mkuu lakini kimeshindwa kupata wingi wa kura za kutosha za kukiwezesha kuunda serikali ijayo. Rajoy amesema atajaribu kuunda serikali mpya iliyo thabiti baada ya chama chake cha Popular-PP-kushinda kwa asilimia 28.71 na hivyo kujinyakulia viti 123 vya Ubunge. Chama cha Kisosholisti kiliibuka mshindi wa nafasi ya pili katika uchaguzi huo kwa kupata viti tisini huku vyama viwili vipya vya Podemos na cha mrengo wa kati...

Like
253
0
Monday, 21 December 2015
LUBANGA NA KATANGA WAREJESHWA CONGO
Global News

MAHAKAMA ya kimataifa ya uhalifu wa kivita ICC, imewarejesha nchini Kongo waasi wawili, Thomas Lubanga na Gemain Katanga ili waweze kutumikia vifungo vyao nchini humo. Lubanga alishtakiwa na mahakama hiyo kutokana na makosa ya kuwa ajiri watoto wadogo katika kundi lake la waasi na kusababisha mauaji na vitendo vya ukiukwaji wa haki za binadamu kati ya mwaka 2002 na 2003. Germain Katanga yeye anayedaiwa kuongoza kundi lililofanya mauaji ya zaidi ya watu Elfu 2, katika wilaya ya Ituri Mashariki mwa...

Like
232
0
Monday, 21 December 2015