Slider

MAELFU WAMUAGA PAPA WEMBA KINSHASA:
Global News

Maelfu ya waombolezaji walijitokeza kuadhimisha misa ya wafu kwa heshima ya mwanamuziki nyota wa muziki wa Soukus na Rhumba raia wa Jamhuri ya Congo Papa Wemba. Waomboloezaji walipiga foleni ilikupata fursa ya kutoa heshima zao za mwisho kwa msanii huyo nguli aliyeaga dunia juma lililopita alipokuwa akiwatumbuiza mashabiki wake huko Abidjan Ivory Coast. Mwili wake umewekwa katika majengo ya bunge mjini Kinshasa. Serikali imetangaza siku tatu za maombolezi kuanzia leo hadi jumatano atakapozikwa. Tayari amepewa tuzo kwa mchango wake. Msanii...

Like
292
0
Tuesday, 03 May 2016
MWANZA: KILELE CHA MAADHIMISHO YA SIKU YA UHURU WA VYOMBO VYA HABARI
Local News

WAKATI Leo ni kilele cha siku ya Uhuru wa Vyombo vya Habari, katibu wa baraza la habari Tanzania MCT-KAJUBI MUKAJANGA  amesema kuwa  uwepo  wa vikwazo mbalimbali katika uhuru wa vyombo vya habari ikiwemo uingiliwaj wa urushwaji wa matangazo ya bunge moja kwa moja unaweza kuchangia  kwa kiasi kikubwa urudishwaji nyuma wa  mafanikio yaliopatikana katika tasnia ya habari nchini. Akizungumza na Efm Mukajanga amesema kuwa wadau wa habari wakiwemo waandishi wa Habari na serikali wana kazi kubwa ya kulinda mafanikio yaliopatikana katika...

Like
314
0
Tuesday, 03 May 2016
LEICESTER CITY MABINGWA EPL, HUU NDIO MKWANJA WALIOVUTA
Slider

Leicester City watajizolea $200m (£150m) baada yao kufanikiwa kushinda Ligi Kuu ya Uingereza Jumatatu, watathmini wa michezo na utangazaji wa Repucom wanasema. Pesa hizo zinatokana na tuzo ya kushinda Ligi ya Premia, pesa za kushiriki Ligi ya Klabu Bingwa Ulaya, na ongezeko la mapato ya kila siku kutokana na mauzo ya tiketi. Klabu hiyo pia itajivunia kupanda kwa thamani ya udhamini na pia ongezeko la mashabiki duniani. Klabu hiyo inayotoka East Midlands itashiriki katika Ligi ya Klabu Bingwa Ulaya msimu...

Like
344
0
Tuesday, 03 May 2016
WANAJESHI WA UINGEREZA WATUA SOMALIA
Global News

IMEELEZWA kuwa Wanajeshi wa Uingereza wamewasili nchini Somalia kusaidia katika juhudi za kukabiliana na wapiganaji wa Kiislamu wa Al-Shabaab. Wanajeshi 10 waliowasili nchini Somalia ni sehemu ya kikosi cha umoja wa mataifa na watasaidia kikosi cha wanajeshi wa Umoja wa Afrika (Amisom) kukabiliana na Al-Shabaab. Idadi ya wanajeshi wa Uingereza nchini Somalia inatarajiwa kupanda hadi 70 ambao watahusika na shughuli za matibabu, mipango na...

Like
263
0
Monday, 02 May 2016
KERRY AFUNGUA SIKU YA PILI YA MAZUNGUMZO MJINI GENEVA
Global News

WAZIRI wa mambo ya nchi za nje wa Marekani John Kerry amefungua siku ya pili ya mazungumzo mjini Geneva yenye lengo la kutafuta njia  ya kupata suluhu ya mapigano nchini Syria. Kerry  amekutana na Waziri wa  mambo ya nchi za nje wa Saudi Arabia  Adel Al-Jubeir na anapanga pia kuwa na mazungumzo baadae na  mjumbe maalumu wa Umoja wa Mataifa anayehusika na Syria Staffan De Mistura. Waziri Kerry amesema hatua za maelewano kuhusu njia ya kupunguza mashambulizi mjini Aleppo zinaendelea kuimarika,...

Like
310
0
Monday, 02 May 2016
TAKRIBANI WATU MILIONI 700 DUNIANI WANAISHI KWENYE UMASIKINI ULIOKITHIRI
Local News

WAKATI Tanzania Leo ikiungana na Mataifa mengine Duniani kuadhimisha siku ya Uhuru wa Vyombo vya Habari, imeelezwa kuwa watu takribani milioni 700 duniani wanaishi katika hali ya umasikini uliokithiri. Hayo yameelezwa na ofisa Habari wa ofisi ya ya umoja wa mataifa Tanzania USIA NKOMA wakati akizungumza katika siku ya kwanza ya maadhimisho ya Uhuru mkoani Mwanza. USIA amesema kuwa watu wengi wameendelea kushuhudia kuongezeka kwa ukosefu wa usawa hata baada ya nchi kufaulu kupata wastani wa maendeleo ya kiuchumi....

Like
286
0
Monday, 02 May 2016
WAKUU WA IDARA WA MANISPAA ZA JIJI LA DARESALAAM WALA KIAPO KUTAFUTA WATUMISHI HEWA
Local News

WAKUU wa Idara zote za Mkoa wa Dar es Salaam wametakiwa kuhakikisha wanatoa majina yote ya watumishi hewa ndani ya muda wa siku saba kuanzia leo. Agizo hilo limetolewa na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mheshimiwa Paul Makonda wakati akizungumza na wakuu wa idara mbalimbali nchini, maafisa utumishi, wakurugenzi wa wilaya na viongozi wengine. Baada ya kutoa agizo hilo Mheshimiwa makonda amewataka Wakuu wa idara zote za mkoa huo, kusaini Mkataba wa kiapo cha kutojihusisha na suala la...

Like
408
0
Monday, 02 May 2016
UKURASA MPYA WA JOTO LA ASUBUHI
Slider

Watangazaji mahiri Gerald Hando na Paul James (PJ) wameanza rasmi kutangaza 93.7 Efm redio siku ya  leo ya  tarehe 02/05/2016  katika kipindi cha Joto la asubuhi  kilichoboreshwa wakiwa pamoja  na Adela Tilya live nje ya jengo la  K- net house zilipo ofisi za E fm. Kipindi hiki kinarushwa kuanzia Jumatatu hadi Ijumaa  saa 12:00 hadi saa 3:00 Asubuhi. Usipitwe. Kutoka kushoto ni Gerald Hando, Adella Tillya, pamoja na Paul James wakitangaza live chini ya jendo la K-net house. Rdj Spar akisababisha muziki live katika kipindi cha...

1
1784
0
Monday, 02 May 2016
UKIWA NAIROBI MSIMU HUU WA MVUA EPUKA NJIA HIZI
Global News

Kwa mujibu wa taarifa iliyochapishwa kwenye tovuti ya Standard Digital nchini Kenya zinasema kuwa mashirika mawili ya serikali nchini humo yamewatangazia watumiaji wa njia za Lang’ata, Muhoho, Popo, Lusaka, Gichuru, Ushirika, Jakaya Kikwete, Lenana, Jogoo kuwa makini na barabara hizo kutokana na mafuriko, hivyo watumiaji wametakiwa kuepuka njia hizo katika kipindi cha mvua kubwa zinazopelekea kuharibika kwa miundombinu ya...

Like
435
0
Monday, 02 May 2016
EPL: LEICESTER CITY YANYEMELEA UBINGWA!!!
Slider

Leicester City wamebakiwa na alama mbili pekee kuupata ushindi wa ligi kuu ya England baada ya kupata sare ya 1-1 dhidi ya klabu ya Manchester United katika dimba la Old Trafford huku wakitegemea matokeo ya mchezo kati ya Chelsea dhidi ya Tottenham utakaopigwa leo hii majira ya saa nne usiku kwa saa za afrika mashariki katika dimba la Stamford Bridge. Mbweha walipata afueni baada ya kuwa nyuma kwa goli moja lililofungwa na Antony Martial dakika ya nane ya mchezo kabla...

Like
272
0
Monday, 02 May 2016
TENISI: GRIGOR DIMITROV AOMBA RADHI
Global News

Mcheza tenisi wa Bulgaria Grigor Dimitrov ameomba radhi baada ya kuonyesha utovu wa nidhamu pale alipoibamiza chini mara tatu fimbo yake ya kuchezea baada ya kukubali kichapo dhidi ya Diego Schwartzman katika michuano ya wazi ya Istanbul. Mbulgaria huyo aliyekuwa akilisaka taji lake la kwanza katika kipindi cha miaka miwili alipoteza kwa seti 6-7,5-7,7-6, 7-4,na 6-0. Dimitrov alipewa onyo kali aliporusha kwa mara ya kwanza na kwa hasira fimbo yake ya kuchezea mapema mnamo seti ya tatu na kisha akapewa...

Like
253
0
Monday, 02 May 2016