Slider

TCU YAFUTA VYUO VIKUU VISHIRIKI VIWILI
Local News

TUME  ya Vyuo Vikuu Tanzania TCU leo imevifuta  vyuo vikuu vishiriki viwili vya Sayansi za Kilimo na Teknolojia,  pamoja  na Teknolojia ya Habari   vya  Chuo cha Mtakatifu Yosefu Tanzania kutokana na kuwepo kwa matatizo ya muda mrefu ya ubora wa elimu, uongozi, ukiukwaji wa sheria na taratibu za uendeshaji wa chuo kikuu ambao hauzingatii matakwa ya Sheria ya Vyuo Vikuu.   Katibu Mtendaji wa TCU Profesa Yunus Mgaya amesema kuwa kifungu cha 5(1)cha Sheria ya Vyuo Vikuu , sura ya...

Like
316
0
Friday, 19 February 2016
NECTA YATANGAZA MATOKEO YA KIDATO CHA NNE
Local News

BARAZA la mitiani Tanzania NECTA limetangaza Matokeo ya kidato cha nne mwaka 2015 , ambapo  ufaulu  unaelezwa kushuka  kwa asilimia 1.85  kutoka  asilimia 69.75  mwaka 2014  hadi asilimia 67.91 kwa  mwaka  2015.   Katibu Mtendaji wa NECTA Dokta Charles Msonde ameeleza kuwa  takwimu za matokeo zinaonesha kuwa bado ufaulu wa masomo yaliyomengi upo chini ya asilimia hamsini na idadi ya watahiniwa waliopata daraja la kwanza, daraja la pili na daraja la tatu ni takribani robo ya watahiniwa waliofanya mtihani. Aidha, Dokta Msonde...

Like
514
0
Thursday, 18 February 2016
ALIYEKUWA KATIBU MKUU WA UMOJA WA MATAIFA BOUTROS-GHALI AFARIKI DUNIA
Global News

UMOJA wa Mataifa umetangaza kuwa aliyekuwa Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa, Boutros Boutros-Ghali amefariki dunia akiwa na umri wa miaka 93. Mmisri huyo, aliyekuwa katibu mkuu wa kwanza kutoka Afrika pamoja na Ulimwengu wa Kiarabu, alifariki dunia jana mjini Cairo, kutokana na maradhi yasiyojulikana. Wakati akisifiwa kwa operesheni ya kwanza kubwa ya msaada wa dharura kuwahi kufanywa na Umoja wa Mataifa kwa ajili ya kuwaisaidia waathiriwa wa baa la njaa nchini Somalia, uongozi wake ulikosolewa kutokana na Umoja wa...

Like
310
0
Wednesday, 17 February 2016
KAMPUNI YA APPLE YATANGAZA KUPINGA AMRI YA MAHAKAMA
Local News

KAMPUNI ya Apple imesema itapinga amri ya mahakama ya kuwasaidia wachunguzi wa shirika la kijasusi nchini Marekani FBI kuchukua habari katika simu ya muuaji wa watu 14 katika eneo la San Bernadinho nchini Marekani.   Kampuni hiyo ilikuwa imeamrishwa kulisaidia shirika hilo la FBI kuifungua simu ya aina ya iphone ya Farook Syed ambayo wanasema ina habari muhimu.   Katika taarifa yake mkurugenzi mkuu wa Apple Tim Cook amesema Serikali ya Marekani inaitaka Apple Kuchukua hatua kama hizo ambazo zinatishia...

Like
276
0
Wednesday, 17 February 2016
MKURUGENZI WA TAASISI YA ELIMU YA WATU WAZIMA AOMBWA KUTUMBUA MAJIPU
Local News

WIZARA ya Elimu Sayansi Teknolojia na Ufundi imemtaka Mkurugenzi wa Taasisi ya Elimu ya Watu wazima kuwasimamisha kazi Wakufunzi wakazi wa tatu, kwa kukiuka utaratibu wa kuchagua wanafunzi wa kidato cha kwanza kufuatia upotoshaji uliofanywa kwa makusudi wa kuwadanganya Wanafunzi kuwa wamechaguliwa katika shule ya Serikali jambo ambalo sio kweli.   Hatua hiyo imefikiwa kufuatia kuwepo kwa  Wakufunzi wakazi katika baadhi ya Mikoa kutangaza kuwa Wanafunzi hao wamechaguliwa kujiunga na kidato cha kwanza kama Wanafunzi wa chaguo la pili na...

Like
412
0
Wednesday, 17 February 2016
OBAMA: TRUMP HATAKUWA RAIS
Global News

RAIS Barack Obama wa Marekani amesema  anaamini mgombea urais wa Chama cha Republican Donald Trump hatakuwa rais wa Marekani. Bwana Trump, Mfanyabiashara tajiri kutoka New York, anaongoza kwenye kura za maoni katika kinyang’anyiro cha kuteua mgombea wa chama cha Republican na tayari ameshindakatika Uchaguzi wa mchujo jimbo moja. Akiongea wakati wa Mkutano Mkuu wa Kiuchumi wa nchi za Kusini Mashariki mwa Asia unaofanyika katika jimbo la California, alitoa kauli hiyo baada ya mwandishi wa Habari Mmoja kumuuliza swali lililomhusu...

Like
212
0
Wednesday, 17 February 2016
KENYA KUJENGA JELA YA WAHALIFU WA MAKOSA YA UGAIDI
Global News

RAIS wa Kenya Uhuru Kenyatta amesema Nchi hiyo itajenga jela mpya ya kuwafunga wafungwa wenye makossa ya itikadi kali. Kiongozi huyo amesema hatua hiyo itazuia wafungwa hao kutoeneza itikadi hizo kwa wafungwa wengine. Kwa sasa ni wafungwa waliohukumiwa pekee ambao hutengwa na wafungwa wengine gerezani nchini...

Like
223
0
Wednesday, 17 February 2016
SERIKALI YAOMBWA KUFANYA UKAGUZI WA MAENEO YALIYOTENGWA KWA AJILI YA SHUGHULI ZA KIJAMII
Local News

SERIKALI imeombwa kufuatilia na kukagua maeneo yaliyotolewa kwa ajili ya shughuli mbalimbali za kijamii ikiwemo shule, hospitali na zahanati ili kuwaletea maendeleo wananchi. Rai hiyo imetolewa Jijini Dar es salaam na Diwani wa kata ya Buguruni Adam Fugame alipokuwa akizungumza na wanahabari kwa lengo la kumuomba mkuu wa mkoa wa Dar es salaam Said Meck Sadik kuukabidhi uongozi wa kata kiwanja alichowahi kukikabidhi mwaka 2011 kwa ajili ya ujenzi wa shule ya sekondari ambacho kimekodishwa kwa kampuni ya Yasser General...

Like
233
0
Wednesday, 17 February 2016
MWANZA: WANANCHI WATAHADHARISHWA JUU YA WEZI WANAOTUMIA BODABODA
Local News

MWENYEKITI wa chama cha waendesha pikipiki Mkoa wa Mwanza, Makoye Kayanda, amewatahadharisha wakazi wa jiji hilo kuwa makini wawapo barabarani ili kuepukana na vitendo vya ukwapuaji  mikoba na mabegi vinavyofanywa na baadhi ya wahalifu kwakutumia pikipiki maarufu Boda boda. Kayanda ametoa tahadhari hiyo jijini Mwanza baada ya kupokea malalamiko ya kukithiri kwa vitendo hivyo vinavyofanywa na baadhi ya watu wanaojifanya waendesha pikipiki  jambo linalochafua taswira ya waendesha pikipiki wa...

Like
303
0
Wednesday, 17 February 2016
UTURUKI YAENDELEZA MASHAMBULIZI DHIDI YA WAKURDI SYRIA
Global News

UTURUKI imeendelea kuyashambulia maeneo ya Wakurdi nchini Syria kwa siku ya pili, licha ya kuongezeka shinikizo la kimataifa kuitaka nchi hiyo isitishe mashambulizi yake kwenye eneo la mpakani. Uturuki inataka wapiganaji wa Kikurdi waondoke kwenye eneo hilo la mpaka. Akizungumza kwa njia ya simu na Kansela wa Ujerumani, Angela Merkel, Waziri Mkuu wa Uturuki, Ahmet Davutoglu amesema vikosi vya usalama vya nchi yake havitowaruhusu Wakurdi wafanye vitendo vya uchokozi. Syria imeyalaani mashambulizi ya Uturuki, huku ikiutolea wito Umoja wa Mataifa...

Like
223
0
Monday, 15 February 2016
WANADIPLOMASIA KUANDAA RIPOTI YA USALAMA ISRAEL NA PALESTINA
Global News

WANADIPLOMASIA wa mataifa manne wapatanishi katika amani ya Mashariki ya Kati wamesema wataandaa ripoti kuhusu hali ya sasa ya usalama kati ya Israel na Palestina huku wakiangazia zaidi kuanza tena kwa mazungumzo ya amani. Baada ya kukutana mjini Munich, Marekani, Umoja wa Mataifa, Umoja wa Ulaya na Urusi, zimesema ripoti hiyo itajumuisha mapendekezo ambayo yanaweza kusaidia kuyajulisha mazungumzo ya kimataifa kuhusu njia bora ya kupatikana kwa suluhisho la mataifa hayo...

Like
196
0
Monday, 15 February 2016