Slider

SERIKALI YAAHIDI KUENDELEZA UJENZI WA BARABARA KWA KINGO CHA RAMI
Local News

SERIKALI imeahidi kuendelea na ujenzi wa barabara katika maeneo tofauti nchini kwa kiwango cha lami ili kutatua adha kubwa ya ubovu wa barabara ulipo katika maeneo mengi nchini.   Hayo yamesemwa leo Mjini Dodoma na Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano  Mhandisi Godwin Ngonyani wakati akijibu maswali ya wabunge waliouliza kuhusu mpango wa serikali kuboresha barabara zilizopo.   Akijibu swali la Mhe Richard Mganga Ndassa Mbunge wa Sumve (CCM) Mhandisi Godwin Ngonyani amesema katika mwaka wa fedha 2014/2015 na...

Like
281
0
Thursday, 28 January 2016
SERIKALI YATOLEA UFAFANUZI TAARIFA YA URUSHAJI WA MATANGAZO YA BUNGE
Local News

SERIKALI imetolea ufafanuzi kuhusu taarifa za upotoshaji kwa umma kuwa imefuta vipindi vya shughuli za Bunge kuoneshwa katika televisheni ya Shirika la Utangazaji la Tanzania (TBC) zilizoenea katika maeneo mbalimbali.   Hayo yamesemwa leo Mjini Dodoma na Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mheshimiwa Nape Nnauye wakati akizungumza na wananchi moja kwa moja kupitia vyombo mbalimbali vya habari nchini kutolea ufafanuzi taarifa hizo.   Mheshimiwa Nape amesema Serikali haijafuta vipindi vya Bunge bali ilichofanya ni kubadilisha...

Like
263
0
Thursday, 28 January 2016
SERIKALI YATOA UFAFANUZI WA URUSHAJI WA MATANGAZO YA BUNGE
Local News

SERIKALI imesema kuwa kusitishwa kwa baadhi ya matangazo ya moja kwa moja ya vikao vya Bunge haina maana kuwa matangazo hayo hayataoneshwa bali matangazo yataendelea kwa muda husika uliopendekezwa ili kuruhusu Kituo cha matangazo cha Taifa TBC kuendelea na majukumu mengine hata kabla ya kikao cha Bunge kukamilika. Akijibu swali la mheshimiwa Freeman Mbowe leo Bungeni mjini Dodoma katika kipindi cha maswali ya moja kwa moja kwa waziri mkuu, Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania mheshimiwa Kassim Majaliwa...

Like
376
0
Thursday, 28 January 2016
MALYSIA: KESI YA UFISADI YA RAZAK KUKATIWA RUFAA
Global News

SHIRIKA la kukabiliana na ufisadi nchini Malaysia limesema kuwa litakata rufaa kuhusu uamuzi wa kuondoa tuhuma za ufisadi dhidi ya waziri mkuuu, Najib Razak. Siku ya jumanne, mkuu wa sheria amesema kuwa uchunguzi haukupata ushahidi kwamba Najib alivunja sheria. Kesi hiyo imeitikisa nchi ya Malaysia na kutishia kumwondoa madarakani ikichangiwa na Uamuzi wa kumuondelea mashtaka hali iliyozua hisia kali kwa...

Like
271
0
Wednesday, 27 January 2016
AL-SHABAB WADHIBITI MIJI ILIYOKUWA IKISHIKILIWA NA MAJESHI YA KENYA
Global News

WAPIGANAJI wa kundi la Al-Shabab wameingia na kudhibiti miji ambayo majeshi ya Kenya yaliondoka jana nchini Somalia. Wakazi wa maeneo ya jirani na miji hiyo wamewaambia waandishi wa habari kwamba wapiganaji wa kundi hilo la Kiislamu wameingia kwenye miji ya Al-Adde, Hosingoh na Badhaadhe. Katika mji wa Hosingoh, mamia ya wapiganaji wanaripotiwa kuingia na kuhutubia wakazi na kisha wakamteua kiongozi wa kusimamia eneo...

Like
301
0
Wednesday, 27 January 2016
MRADI WA KUCHAKATA TAKA KUJENGWA KINONDONI
Local News

HALMASHAURI ya Manispaa ya Kinondoni inatarajia kujenga mradi wa kuchakata taka hususani zile zinazozalishwa kwenye masoko yanayopatikana kwenye manispaa hiyo lengo ikiwa ni kuondoa taka hizo ili manispaa iwe safi. Akizungumza na waandishi wa habari Jijini Dar Es Salaam leo Meya wa Manispaa ya kinondoni Boniface Jacob amesema kuwa mradi huo unaogharimu zaidi ya shilingi bilioni 2 za kitanzania utajengwa kwa ushirikiano kati ya serikali ya Ujerumani, Halmashauri ya Hambag na Halmashauri ya Manispaa ya kinondoni. Boniface ameeleza kuwa kutokana...

Like
317
0
Wednesday, 27 January 2016
MKUU WA MKOA WA PWANI ATOA SIKU 7 ZA KUTUMBUA MAJIPU
Local News

MKUU wa Mkoa wa Pwani Mhandisi Evarist Ndikilo ametoa muda wa siku saba kwa watendaji wa mitaa, watendaji wa kata na  wazazi wenye watoto waliofaulu kuingia kidato cha kwanza lakini hadi sasa wameshindwa  kuwapeleka shule wanafunzi hao, kuwapeleka shule haraka watoto wanafunzi hao.   Mhandisi Ndikilo ametoa agizo hilo wakati wa ziara yake ya siku moja katika halmashauri ya mji wa Kibaha  wakati akizungumza na watumishi na watendaji mbalimbali wa serikali na vyama vya siasa ambapo amesema kuwa mzazi ambaye...

Like
345
0
Wednesday, 27 January 2016
PEP GUARDIOLA AIKANA MAN CITY NA KUICHAGUA MAN U
Slider

Pep Guardiola aishangaza dunia, aikana Manchester City na kuwachagua mahasimu wao Manchester United, amtaka mlinda mlango wa Barcelona Claudio Bravo kujumuika nae. Wakati huo huo viongozi ndani ya Manchester United wanahofia kumkosa Ryan Giggs iwapo Lois Van Gaal atatimuliwa bila yeye kupewa...

Like
269
0
Wednesday, 27 January 2016
SIMBA YAIFUNGUKIA TFF
Slider

Simba yatoa msimamo wake juu ya panga pangua ya ratiba ya ligi kuu Tanzania bara msimu huu, Tff yashushiwa lawama kwa mabadiliko ya ratiba baada ya kuiruhusu Azam Fc kwenda kushiriki mashindano ya kualikwa nchini Zambia Simba ndio bingwa ligi kuu ya kandanda Tanzania bara msimu huu, niulizeni baada ya miezi mine kauli ya MANARA, wewe unasemaje? Danny Lianga bado ni mchezaji wa Simba na hana matatizo na...

Like
295
0
Wednesday, 27 January 2016
ELITREA: WANAUME WAPEWA AGIZO LA KUOA MKE ZAIDI YA MMOJA, KIFUNGO CHA MAISHA KUWAKABILI WATAKAOPUUZA
Entertanment

Wanaume nchini Elitrea wamepewa amri ya kuoa angalau wake wawili au zaidi kwa kila mwanaume huku adhabu ya kifungo cha maisha jela kutolewa kwa atakaekaidi amri hiyo ya serikali. Kwa mujibu wa serikali agizo hilo limetolewa kufuatia uwepo wa idadi ndogo ya wanaume ikilinganishwa na idadi ya wanawake ikiwa ni matokeo ya vita kati ya taifa hilo na Ethiopia. Serikali nchini humo imewathibitishia raia wake kuwa itagharamia sherehe za harusi na nyumba kwa wanandoa Kwa mujibu wa tovuti ya Afkinsider.com ...

Like
634
0
Wednesday, 27 January 2016
UGAIDI: 900 WASHIKILIWA NA POLISI SENEGAL
Global News

POLISI nchini Senegal wamewakamata watu wapatao mia tisa katika kamata kamata ya watu wanaoshukiwa kujihusisha na ugaidi. Zoezi hilo limefanyika mwishoni mwa juma lililopita katika mji mkuu wa Dakar karibu na mtaa wa Thies huku Jeshi la ulinzi likitoa angalizo tangu shambulio lililowahi kutokea mapema mwezi huu katika hoteli iliyoko mji mkuu wa Burkina Faso. Hata hivyo wiki iliyopita waziri wa mambo ya ndani wa nchi hiyo Abdoulaye Daouda Diallo amezitaka hoteli zote nchini humo kuongeza ulinzi ili kuzuia matukio...

Like
237
0
Wednesday, 27 January 2016