JUMLA ya Wanafunzi wa Kike 45 na Mwalimu Mmoja wamekubwa na ugonjwa wa ajabu ambao haujapata dawa hadi sasa kwenye Kata ya Chingungwe Wilaya ya Tandahimba Mkoa wa Mtwara. Baraza la Madiwani la Wilaya ya Tandahimba limeelezwa kuwa ugonjwa huo unawakumba watoto wa Kike tu ambapo huanguka na kupoteza fahamu pindi waingiapo maeneo ya shule ya Sekondari ya Chingungwe. Akito taarifa ya utekelezaji wa Mradi ya Kata ya Chingungwe kwenye Baraza la Madiwani Diwani HALIMA MCHUNGA amebainisha kuwa watoto hao wa...
VITUO 111 vya kuandikisha wapiga kura na kupigia kura vimeandaliwa katika Manispaa ya Mtwara Mikindani Mkoani humo. Kauli hiyo imetolewa na Mkurugenzi wa Manispaa hiyo LIMBAKISYE SHIMWELA wakati akizungumza na Waandishi wa Habari ofisini kwake kuhusu idadi ya Vituo hivyo ambavyo tayari vimeandaliwa kwa ajili ya uchaguzi wa Serikali za Mitaa. Amebainisha kuwa Serikali imejiandaa kufanya Uchaguzi huo ifikapo Desemba 14 mwaka huu na kwamba anaamini utafanyika kwa mafanikio makubwa ili taifa lipate viongozi Bora....
WATAALAM, wa maswala ya uchumi nchini wametakiwa kupima na kutazama kipato cha wananchi wanapofanya tathmini za ukuwaji wa uchumi badala ya kutaja viwango vya ukuaji wa serikali wakati wananchi ni masikini. Hayo yamebainishwa leo jijini Dar es salaam na Naibu Waziri wa fedha na Mbunge wa Mkuranga Mheshimiwa ADAM MALIMA alipokuwa akifungua warsha ya siku nne, kujadili ripoti ya ukuwaji wa uchumi kwa nchi za Afrika unaofanyika kwa ufadhili wa Benki ya maendeleo ya Afrika ambapo amesema walengwa hasa...
WAZIRI MKUU Mheshimiwa MIZENGO PINDA amewataka wakulima na wafugaji nchini hususani wa wilayani Kiteto mkoani Manyara kuishi kwa kufuata sheria na taratibu zilizowekwa pamoja na kuondoa tofauti zao za ukabila ili kuondokana na migogoro ya muda mrefu na kuliletea Taifa maendeleo. Waziri PINDA ametoa wito huo leo Bungeni mjini Dodoma wakati akiwasilisha ripoti na kauli ya serikali juu ya namna serikali inavyoendelea kuchukua hatua mbalimbali za kutatua mgogoro huo. Mbali na hayo pia mheshimiwa Pinda amesema kuwa serikali imejiwekea...
ZAIDI YA WANAFUNZI 200 wa Shule ya KAC iliyopo Kisongo mjini Arusha wamenufaika na Elimu ya Mazingira na umuhimu wa kupenda Utalii huku lengo likiwa ni kuwajengea uwezo wa kuzitambua fursa. Pia Elimu hiyo mpaka sasa imeweza kuzaa matunda shuleni hapo kwani wanafunzi hao wameanzisha Umoja yaani CLUBS wa kupambana na Masuala hayo kuanzia shuleni hadi katika jamii inayowazunguka. Akizungumza katika mahafali ya Nne ya Shule hiyo Mkurugenzi Mtendaji Profesa CALVIN MAREALLE amebainisha kuwa mpango huo umeanza rasmi mwaka 2010...
IMEELEZWA kuwa vitendo vya Ukatili wa Jinsia kwa Watoto vimeongezeka katika Mkoa wa Dar es salaam katika kipindi cha January hadi September mwaka huu. Taarifa iliyotolewa na Chama Cha Waandishi wa Habari wanawake Tanzania-TAMWA imeeleza kuwa katika miezi tisa Pekee vitendo hivyo vimefikia 519. Zanzibar imeshika nafasi ya Pili kwa kuwa na ongezeko kubwa la vitendo vya ukatili wa Jinsia ikiwa na idadi ya 219, ikifuatiwa na Shinyanga 69, Mara 62,Tabora 55,Morogoro 36, Kagera 32 na Pwani...
WATANZANIA wametakiwa kuelekeza nguvu katika kuendeleza taaluma ya sayansi, tekinolojia na mawasiliano ili kuinua uchumi wa nchi kupitia ukuaji wa tekinolojia unaoendelea kwa kasi duniani. Hayo yamesemwa leo na Waziri wa mawasiliano sayansi na tekinolojia Profesa MAKAME MBARAWA alipokuwa mgeni rasmi katika mkutano wa kutathmini mafanikio ya miaka minne yatokanayo na mpango wa maendeleo ya tekinolojia kwa msaada wa serikali ya Italia. Aidha Profesa Mbarawa amesema katika kipindi hicho cha miaka mine, Tanzania imeshatengeneza wataalamu wengi...
BUNGE la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania limepitisha Azimio kuhusu Tanzania kuridhia itifaki ya kuanzisha tume ya utafiti wa Afya katika nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki kwa lengo la kuiwezesha Jumuiya kupata ushauri wa masuala ya kiafya hali itakayoimarisha huduma hiyo kwa wananchi. Akitoa Hoja rasmi ya Azimio hilo leo Bungeni mjini Dodoma Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii Dokta SEIF RASHID amesema umuhimu wa azimio katika utekelezaji wa Utafiti huo utakuwa katika kiwango cha kuridhisha katika...
RAIS wa Liberia ELLEN JOHNSON SIRLEAF ameondoa sheria ya hali ya hatari ambayo ilikuwa imetangazwa nchini humo katika juhudi za kudhibiti kuenea kwa maradhi ya Ebola, ambayo yaliizonga nchi hiyo na nyingine mbili jirani katika kanda ya Afrika Magharibi. Katika hotuba yake kwa taifa Rais SIRLEAF amesema kuondolewa kwa sheria hiyo hakumaanishi kwamba mlipuko wa ugonjwa huo umemalizika. Amebainisha kuwa Maendeleo ya kutosha yamepatikana katika vita dhidi ya maradhi hayo kuwezesha kuondolewa kwa sheria...
MVUA kubwa ya mawe iliyoambatana na upepo mkali imenyesha na kusababisha maafa katika Wilaya ya Bunda mkoani Mara ikiwa ni pamoja na watoto wawili kujeruhiwa na mmoja kuvunjika mkono kutokana na kuangukiwa ukuta wa nyumba. Katika tukio la kwanza Mvua ya mawe iliyoambatana na upepo mkali imenyesha katika kijiji cha Nyabehu Kata ya Guta ambapo watoto wawili wamejeruhiwa na mmoja kuvunjika mkono. Kwa mujibu wa Diwani wa Kata ya Guta MWITA MWANGIERA amebainisha kuwa Mvua imenyesha kwa zaidi ya saa...
NAIBU Waziri wa Ustawi wa Jamii Dokta STEVEN KEBWE amesema Tanzania ni nchi ya Nane kati ya nchi 10 zinazoongoza kwa kuwa na watu wanaougua sukari Barani Afrika. Dokta KEBWE ameeleza hayo alipokuwa akitoa tamko kuhusu siku ya Kisukari inayoadhimishwa leo Duniani. Amebainisha kuwa nchini Maadhimisho hayo yanafanyika yakiwa na Kauli Mbiu isemayo ULAJI UNAOFAA HUANZA NA MLO WA...