WIZARA ya Afya na Ustawi wa Jamii imewataka viongozi wa ngazi zote nchini kuanzia ngazi ya jamii hadi mkoa kuwaelimisha ipasavyo wananchi kushiriki kikamilifu katika kampeni ya utoaji chanjo ya kutibu magonjwa yasiyoambukiza ikiwemo Surua na Rubella. Wito huo umetolewa na Kaimu Katibu Mkuu wa Wizara Dokta DONAN MMBANDO… Mbali na hayo pia Dokta MMBANDO amebainisha mikakati mbalimbali inayoandaliwa na serikali katika kujiweka sawa kupambana na ugonjwa hatari wa...
KAMPUNI mbalimbali za Mawasiliano Ulimwenguni zimekutana kwenye Mkutano wa CAPACITY AFRICA 2014 wakishirikiana na Tanzania kupitia Wizara ya Mawasiliano Sayansi na Teknolojia. Akizungumza katika mkutano huo Naibu waziri wa Mawasiliano sayansi na teknolojia, JANUARY MAKAMBA amesema lengo la mkutano huo ni MAKAMBA…. Kwa upande wake mkuu wa masoko na mauzo wa kampuni ya simu Tanzania- TTCL, PETER NGOTA, amezungumzia pia mipango mbalimbali ya kampuni hiyo Wakifurahia fursa zilizojitokeza Wananchi walioudhuria mkutano huo walikuwa na haya ya...
FAMILIA ya Rais mstaafu wa awamu ya pili wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar Aboud Jumbe Mwinyi imekanusha baadhi ya taarifa zilizoripoti na Vyombo vya habari nchini kuwa hali ya kiongozi huyo ni mbaya kutokana na kusumbuliwa na maradhi ya ugonjwa wa Moyo. Akizungumza na EFM kutoka Hospitali ya Taifa Muhimbili Mkurugenzi Idara ya Uvuvi Zanzibar, MUSA ABDULI JUMBE amesema kuwa BABA yake anasumbuliwa na tatizo la umri kuwa mkubwa. Amefafanua kuwa kwa sasa BABA yake anaendelea vizuri na si mgonjwa...
BAADHI ya wakazi wa eneo la Michungani Kimara Jijini Dar es salaam wapo hatarini kukumbwa na magonjwa ya mlipuko baada ya Mto unaopita karibu na nyumba zao kutiririshwa maji machafu ambayo yamechanganyika na harufu kali inayotoka machinjio ya Kimara katika eneo hilo. Wakizungumza na EFM wakazi hao wamesema kuwa kutokana na hali hiyo wanalazimika kuwafungia ndani watoto wao ili kuwaepusha na madhara mbalimbali ya ki afya Wanananchi…Kimara Hata hivyo kituo hiki kilizungumza na Uongozi wa Serikali ya Mtaa wa Makaroni...
JAMII imetakiwa kuachana na dhana potofu ya kuwakata watoto Kimeo na badala yake wawapeleke hospital kuangalia afya zao. Hayo yamebainishwa na DR SALEHE NGOLE wakati akizungumza na E Fm jijini Dar es salaam na kusema kuwa ukataji wa kimeo kwa njia ya kienyeji ni kinyume kiafya hivyo kunaweza kumsababishia mgonjwa, madhara na badala yake wawapeleke hospital kwaajili ya matibabu zaidi… ...
KAMATI ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo-CHADEMA imekutana kujadili maazimio 11 ya kikao cha pili ya chama hicho. Akiongea na waandishi wa habari jijini Dar es salaam Mwenyekiti wa kamati kuu ya Chadema Mheshimiwa FREEMAN MBOWE amesema kuwa miongoni mwa mambo yatakayojadiliwa na kamati hiyo ni pamoja na uteuzi wa bodi ya wadhamini wa chama hicho… zaidi Mh. Mbowe amesema...
WATANZANIA leo wanaadhimisha kumbukumbu ya miaka 15 tangu kufariki kwa Hayati baba wa Taifa Mwalimu Julius Nyerere . Kufuatia maadhimisho hayo, Wananchi jijini Dar es salaam wamewataka viongozi wa serikali kufuata miongozo na maadili mbalimbali katika kujenga, kulinda na kudumisha amani ya Nchi. Akiongea na EFM mmoja wa wananchi amesema pamoja na juhudi za viongozi waliopo madarakani bado zipo changamoto mbalimbali. Hayati baba wa taifa Julius Nyerere alifariki Dunia Oktoba 14 mwaka 1999. ***...
Jukwaa la Katiba Tanzania- JUKATA limewasihi wananchi kushiriki katika kuhamasishana na kupata Elimu itakayowawezesha Kuisoma na Kuielewa Katiba inayopendekezwa ili kujiandaa na zoezi la upigaji Kura za Katiba hiyo. Wito huo umetolewa jijini Dar es salaam na mwenyekiti wa JUKATA- DEUS KIBAMBA Pia imesema inaunga mkono makubaliano kati ya Vyama vya Siasa na Mheshimiwa Rais juu ya kufanyika kwa kura ya maoni baada ya Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2015 Amesema kuwa ili uelimishaji ufanikiwe kwa kiasi kikubwa ni vyema kwa...
Kuelekea kuadhimisha siku ya Kumbukumbu Kifo cha Baba wa Taifa Hayati Mwalimu JULIUS NYERERE Taasisi ya Mwalimu Nyerere foundation, Makumbusho ya Taifa na Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania-JWTZ wameandaa maonyesho na mdahalo wa kumuenzi Baba wa Taifa ili kujenga, kulinda na kudumisha amani ya nchi. Mdahalo huo pamoja na maonesho kwa pamoja vitafanyika katika jumba la Makumbusho jijini Dar es salaam kuanzia Oktoba 13 hadi 17 baadhi ya Watanzania wamekua na maoni tofauti juu ya namna ambavyo...
Picha ni askari wa kikosi cha barabarani walioonyesha utovu wa nidhamu kufuatia kitendo chao cha kupiga picha za kimapenzi wakiwa na sare za kazi Kamanda wa Jeshi la Polisi Henry Mwaibambe amewataja askari hao kuwa ni PC Asuma Mpaji Mwasumbi mwenye namba F.7788,PC Fadhili Linga mwenye namba G 2122 na PC Veronica Nazaremo Mdeme na wote walikuwa askari wa kikosi cha usalama barabarani wilayani Missenyi. idara ya polisi ni moja ya vitengo vya serikali vinavyolalamikiwa kwa utovu wa maadili kwenye...
Serikali Kupitia Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii imepeleka madaktari Watano kusaidia kutoa huduma za Kitabibu katika nchi zilizoathirika na Ugonjwa wa Ebola.Hapa Dokta MMBANDO anafafanua Mbali na hayo MMBANDO ametoa tahadhari kwa Ugonjwa mpya uliojitokeza katika nchi ya Uganda ambao utapelekea kufungwa kwa mipaka kati ya Tanzania nchi hiyo...