Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli tarehe 23 Oktoba, 2018 amekutana na kufanya mazungumzo na Rais Mstaafu wa Awamu ya Nne Mhe. Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete, Ikulu Jijini Dar es Salaam. Baada ya mazungumzo yao Mhe. Rais Mstaafu Kikwete amesema wamekutana kwa utaratibu wa kawaida wa kusalimiana na kutakiana heri katika majukumu. Aidha, Mhe. Rais Mstaafu Kikwete amebainisha kuwa Mhe. Rais Magufuli anafanya kazi nzuri na amemtaka aendelee hivyo...
Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam limethibitisha kumhoji kwa saa kadhaa na kumwachia Waziri January Makamba kuhusiana na tukio la kutekwa kwa mfanyabiashara Mohammed Dewji. Kupitia ukurasa wake wa Twitter waziri huyo ameandika, hajakamatwa na polisi na kuwa yupo salama. “Polisi walinipigia simu kuniomba, kama rafiki wa Mohamedi Dewji, niwasaidie kama kuna chochote cha ziada ambacho Mo aliniambia kinachoweza kusaidia uchunguzi. Niliwaeleza wakasema kinafanana na alichowaeleza, wakanishukuru. Wamefanya hivi pia kwa wanafamilia....
Afisa mkuu wa polisi wa kanda ya Dar es salaam Lazaro Mombasa aliyetembelea nyumbani kwao Dewji kuthibitisha kurejea kwake nyumbani, watu waliomkamata walikuwa na lafudhi ya mojawapo ya lugha za mataifa ya Afrika Kusini. Aliongezea kwamba hatua hiyo imethibitisha wazi kwamba waliomteka sio watanzania. Mo Dewji; Ninawashukuru Watanzania kwa kuniombea ”Nataka kuuthibitishia umma wa Tanzania kwamba nimefika nyumbani kwa akina Mo Dewji nimeongea naye niko na kikosi cha makachero hapa na ndugu yetu ni mzima kama IGP alivyozungumza na umma...
Mkuu wa Jeshi la Polisi (IGP) Simon Sirro amesema polisi wamepata maelezo muhimu kuhusu gari lililotumiwa na watu waliomteka mfanyabiashara Mo Dewji. Amesema gari hilo lilitokea nchi jirani ambayo hakuitaja na kueleza kuwa liliingia nchini Tanzania mnamo 1 Septemba, amewaonesha wanahabari picha za gari hilo ambapo amesema wanaomba maelezo zaidi. Kamanda Sirro amesema wanafuatilia kwa pamoja na polisi wa kimataifa wa Interpol. Amesema kufikia sasa hawafahamu iwapo gari hilo bado lipo Tanzania na akawaomba wananchi kutoa taarifa kwa polisi...
Picha kutoka Ikulu Dar Es Salaam mahali ambapo Mhe. Rais Dkt. John Pombe Magufuli leo tarehe 19 Oktoba, 2018 anakutana na wachezaji wa Timu ya Taifa (Taifa Stars) na baadaye kula nao chakula cha mchana. Hii nikufuatia Timu ya Taifa (taifa stars) kushinda mechi dhidi ya Cape Verde iliyochezwa mwanzoni mwa wiki hii, mchezo huo ulimalizika taifa stars 2 – Cape Verde 0 magoli yalifungwa na Mbwana Sammatta na Simon Msuva. Pia Raisi Magufuli amezugumza na timu ya taifa na amesema “Mh...
Waziri wa Mambo ya Ndani, Kangi Lugola amesimikwa kuwa Chifu wa kabila la Wasafwa kutoka mkoani Mbeya kama ishara ya kupambana na adui atakaekuja mbele yake....
Tukio la kutekwa bilionea Mohammed Dewji, 43, Alhamisi ya wiki iliyopita bado limesalia kuwa ni fumbo lisilokuwa na jibu. Mpaka kufikia leo bado haijulikani ni akina nani waliomteka na wapi walipomficha na lipi hasa kusudio la kumteka mfanya biashara huyo maarufu kama Mo. Mo alikwapuliwa na watu wasiojulikana nje ya hoteli moja jijini Dar es Salaam alipokuwa akienda kufanya mazoezi. Toka hapo, giza nene limetanda juu ya tukio hilo, licha ya hatua kadhaa ambazo mamlaka za nchi na familia imezichukua....
Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Albert Chalamila, ametoa amri ya kuwekwa rumande saa 24, Katibu wa Chama cha Mapinduzi (CCM), kata ya Maanga, bwana Norasco Tibakawa kwa madai ya kula rambirambi ya shilingi...
Mbunge wa Arusha Mjini (CHADEMA), Godbless Lema ambaye pia ni Waziri Kivuli wa Wizara ya Mambo ya Ndani amemtaka Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola kujiuzulu kutokana na matukio ya utekaji yanayojitokeza nchini ikiwemo la mfanyabiashara ‘Mo Dewji’. Akizungumza na wanahabari leo Oktoba 16, Lema amesema kuwa kitendo cha waziri Lugola kuzuia watu kuzungumzia matukio ya utekwaji wa watu yanayojitokeza kwa sasa hapaswi kufanya hivyo badala yake ni kung’atuka ili kupisha kashfa. Lema amesema kuwa serikali inatakiwa...
Rais John .P Magufuli akiwa na wakimbiza mwenge wa Uhuru 2018 alipokutana nao Ikulu jijini Dar Oktoba 15, akiwa na Waziri Mkuu Kassim Majaliwa na Waziri katika ofisi ya WM (Sera, Bunge, vijana, Ajira na Wenye Ulemavu) Jesnista...
Siku 25 za majonzi kwa Magufuli, Kenyata, Museveni. Katika kipindi cha kuanzia septemba 20 hadi oktoba 14 mwaka huu zimekuwa siku za majonzi na chungu kwa baadhi ya Marais wanaounda Jumuiya ya Afrika Mashariki akiwemo Rais wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli, Rais wa Kenya Uhuru Kenyata, pamoja na Rais wa Uganda Yoweri Museveni. Katika kipindi hicho cha wiki 3, tumeshuhudia majonzi yakianzia kwa Rais wa Tanzania Dkt John Magufuli ambapo kulitokea ajali ya kivuko cha Mv Nyerere iliyozama katika...