UINGEREZA inapanga kuwapatia mafunzo wanajeshi wa serikali ya Ukraine. Waziri mkuu wa Uingereza David Cameron amesema mjini London kuwa kundi la wataalamu wa kijeshi watapelekwa katika jamhuri hiyo ya zamani ya Kisovieti wiki ijayo. Kwa mujibu wa shirika moja la habari la Uingereza, kundi hilo litakuwa na wanajeshi 75, japokuwa hakuzungumzia uwezekano wa kupatiwa silaha wanajeshi wa Ukraine....
WAZIRI wa Mambo ya Nchi za Nje wa Libya Mohammed Dayri ameonya kuwa Libya inaweza kugeuka Syria kutokana na kuzidi kupata nguvu makundi ya itikadi kali. Amezitolea wito nchi za magharibi ziwapatie silaha wanajeshi wa Libya ili waweze kupambana na waasi. Awamu nyingine ya mazungumzo ya kusaka ufumbuzi wa amani ilikuwa ifanyike kesho nchini Moroko, lakini yameakhirishwa baada ya bunge la Libya linalotambuliwa kimataifa kusema halitatuma wawakilishi kutokana na mashambulio ya hivi karibuni yaliyoangamiza maisha ya zaidi ya watu 40....
UINGEREZA imekuwa nchi ya kwanza kuidhinisha sheria itakayoruhusu uzaaji wa watoto wenye vinasaba, DNA kutoka kwa wanawake wawili na mwanamume mmoja. Sheria hiyo ilioimarishwa imepita kikwazo chake cha mwisho baada ya kuidhinishwa na bunge la taifa hilo. Sheria hiyo sasa itadhibiti utoaji wa leseni kwa wanaotaka kutengeneza watoto hao kwa lengo la kuvilinda vizazi hivyo kutorithi magonjwa mabaya. Mtoto wa kwanza huenda akazaliwa kabla ya mwaka 2016....
SHIRIKA la kutetea haki za binaadam la Amnesty International limetoa wito kwa Wanachama watano wa kudumu wa Baraza la usalama la umoja wa Mataifa kutumia kura yao ya Veto kwa maswala yahusuyo mauaji ya halaiki. Shirika hilo limesema kuwa mara kadhaa wamekuwa wakiweka maslahi ya nchi mbele kuliko maswala ya haki za binaadam. Katika Ripoti yake ya mwaka, Amnesty International imesema mwaka 2014 ulikuwa mwaka wenye matukio mabaya kwa mamilioni ya Watu waliokuwa kwenye maeneo yenye migogoro, na kusikitishwa na...
SHIRIKA la haki za binaadamu la Amnesty International limezikosoa serikali ulimwenguni kwa kushindwa kuwalinda mamilioni ya raia dhidi mauaji yanayofanywa na vyombo vya dola na makundi yenye silaha. Ripoti ya kila mwaka iliyochapishwa leo na shirika hilo inaelezea hatua ambazo zimechukuliwa na ulimwengu dhidi ya migogoro nchini Nigeria na Syria kuwa ni za kutia aibu. Amnesty International inayalaumu mataifa tajiri duniani kwa kutumia nguvu na fedha nyingi kuwazuia watu kuingia kwenye mataifa hayo, kuliko kuwasaidia watu kuishi....
TAKRIBANI watu 30 wameuawa katika mashambulizi mawili tofauti katika vituo vya mabasi kaskazini mwa Nigeria. Katika mashambulizi ya kwanza, mshambuliaji wa kujitoa muhanga alikimbia basi lililosheheni abiria katika mji wa Potiskum, ambapo alijiripua na kuwauwa watu 16 pamoja naye. Rais Goodluck Jonathan amesema kundi la Boko Haram linahusika na mashambulizi yote mawili. Katika taarifa nyengine, majeshi ya Chad yanayoshiriki vita dhidi ya Boko Haram, yanaripotiwa kuwauwa wanamgambo 207 kwenye mji wa mpakani mwa Nigeria na...
RAIS Vladimir Putin wa Urusi amesema haoni uwezekano wa kuzuka vita kati Ukraine na nchi yake. Rais Putin ameongeza kuwa haoni sababu ya kukutana na maafisa wa Ufaransa, Ukraine na Ujerumani kujadili suluhisho, na kuongeza kwamba hali itarejea kama kawaida taratibu. Mawaziri wa mambo ya kigeni wa nchi hizo wanakutana leo mjini Paris kujadili usitishaji mapigano mashariki mwa Ukraine....
KUNDI la Islamic State limewateka nyara watu 90 wa jamii ya wakristo kutoka katika kijiji kimoja kazkazini mwa Syria. Tukio hilo la utekaji nyara limefanyika mapema leo alfajiri, baada ya wanamgambo hao kuchukua udhibiti wa vijiji kadhaa kutoka kwa walinda usalama wa kabila la Wakurdi. Wanamgambo hao walivamia kituo cha Radio na kuchukua udhibiti wa mawasiliano na kuanza kutangaza Radioni, kuwa wamewateka nyara wale wanaojiita watetezi wa...
KOREA ya Kusini na Marekani zimetangaza hivi leo kwamba zitaanza mazoezi yao ya kila mwaka ya kijeshi tarehe 2 mwezi ujao, hatua inayotazamiwa kuongeza mzozo na Korea Kaskazini.Serikali ya Korea Kaskazini ilikuwa imeahidi kusitisha majaribio yake ya silaha za nyuklia, endapo mazoezi hayo yangefutwa mwaka huu, lakini Marekani ililikataa pendekezo hilo ikiliita “kitisho” cha kufanya jaribio la nne la nyuklia. Mazoezi hayo ya pamoja ndicho kiini cha mzozo wa mara kwa mara kwenye Rasi ya Korea, ambayo Korea Kaskazini huyachukulia...
UTURUKI imeshutumu Uingereza kwamba imechukua muda mrefu kuijulisha nchi hiyo kuhusu wanafunzi wa kike watatu waliokuwa wakisoma London Uingereza kwamba walisafiri kwenda nchini Syria kwa lengo la kujiunga na Islamic State. Inaelezwa kuwa wanafunzi hao walipanda ndege ya shirika la ndege la Uturuki kutoka Uingereza na walihitaji hati ya kusafiri na visa kuingia Uturuki. Sakata la wanafunzi hao wa kike kutoka London kwenda kujiunga na wapiganaji wa Islamic State limekuwa likishtua wengi. Huku serikali ya Uturuki inasema ingechukua hatua kama...
INAKADIRIWA kuwa wachimbaji wapatao mia tano wameokolewa na magari ya zima moto kutoka machimboni baada ya kuwa wamebanwa chini ya mashimo yenye kina kirefu katika machimbo ya madini nchini Afrika Kusini. Moto mkubwa uliripuka mapema umbali wa zaidi ya kilomita mbili katika machimbo ya mgodi wa Kusasalethu Magharibi mwa mji wa Johannesburg. Mmiliki wa mgodi huo ni kampuni ya Harmony Gold wameeleza kuwa waliwaokowa wanaume zaidi ya mia nne na themanini na sita waliokuwa zamu siku hiyo...