Global News

VIKWAZO ZAIDI DHIDI YA URUSI KUJADILIWA BRUSSELS
Global News

MAWAZIRI wa mambo ya nje kutoka Ulaya watakutana mjini Brussels kujadili vikwazo zaidi dhidi ya Urusi kufuatia mashambulizi ya Mashariki mwa Ukraine. Mkutano huu wa dharula umeitishwa baada ya raia 30 kuuawa kwa makombora, mauaji yaliyotekelezwa na Waasi wanaodaiwa waliungwa mkono na Urusi na kushambulia bandari ya Mariupol Mwishoni mwa wiki iliyopita. Majeshi ya NATO yamesema mamia ya vifaru vya Urusi, Magari ya Silaha yalikua Mashariki mwa Ukraine, ingawa Urusi imekana kujihusisha moja kwa moja na mashambulizi hayo.  ...

Like
251
0
Thursday, 29 January 2015
JAPAN KUCHUNGUZA SAUTI INAYOHISIWA KUWA NI YA MWANDISHI ALIESHIKILIWA MATEKA NA IS
Global News

JAPAN inachunguza sauti iliyorekodiwa ambayo inawezakana ni ya mwandishi wa habari wa Japan aliyeshikiliwa mateka na wapiganaji wa Islamic state. Sauti hiyo inarudia tishio la kumuua rubani wa Jordan aliyetekwa mateka na wapiganaji hao hadi Jordan itakapomwachia huru mwanamke wa Iran aliyehusika na shambulizi la bomu. Famili ya Rubani na mpiganaji mwenye asili ya Jordan anayeshikiliwa mateka na kundi la wanamgambo wa hao wameendelea kuweka shinikizo kwa Serikali ya Jordan kufanya kila iwezalo kuokoa maisha yake. Jordan imeahidi kumuachia...

Like
246
0
Thursday, 29 January 2015
IKULU YA MAREAKANI YATOA TAARIFA YA WASIWASI JUU YA KUONGEZEKA KWA MAPIGANO MASHARIKI YA UKRAINE
Global News

IKULU ya Marekani imearifu kwamba rais Barack Obama na Kansela wa Ujerumani Angela Merkel wamezungumzia wasiwasi wao juu ya hatua ya kuongezeka mapigano mashariki ya Ukraine. Mazungumzo ya viongozi hao kwa njia ya simu yamefanyika jana wakati rais Obama alipokuwa anarejea nyumbani baada ya kumaliza ziara yake nchini India na Saudi Arabia. Ikulu ya Marekani imesema Obama na Merkel wamekubaliana juu ya haja ya kuibebesha dhamana Urusi kwa kuwaunga mkono waasi wanaopigania kujitenga pamoja na kushindwa kutekeleza ahadi zake chini...

Like
317
0
Wednesday, 28 January 2015
WAASI SUDANI KUSINI WAWAACHIA HURU WATOTO
Global News

WAASI Nchini Sudani kusini wamewaachia huru kundi la kwanza la watoto waliokuwa wamechukuliwa kuwa wanajeshi, kundi hilo la watoto lililotegemewa kuachiwa wiki chache zijazo.   Shirika la kimataifa la kuhudumia watoto, UNICEF, limesema Watoto mia mbili na themanini, wengine wakiwa wadogo wa mpaka umri wa miaka 11 walikabidhiwa katika jimbo la jonglei kwa ajili ya kukutanishwa na Familia zao.   Kundi la walioachiwa ni sehemu ya Jeshi la waasi linaloongozwa na David Yau Yau ambaye alisaini mkataba wa amani na...

Like
353
0
Wednesday, 28 January 2015
RAIS WA BANK YA DUNIA ATOA TAHADHARI JUU YA MAPAMBANO YA EBOLA AFRIKA MAGHARIBI
Global News

RAIS wa Benki ya Dunia Jim Yong Kim ametaadharisha kuwa ni hatari kwa kuwa dunia haijajiandaa kupambana na ugonjwa wa Ebola Afrika Magharibi. Akiongea mjini Washington, Kim, amesema ni muhimu kwa Serikali, mashirika, Mashirika ya misaada na makampuni ya Bima kufanya kazi pamoja kujiandaa kukabiliana na maradhi hayo siku za usoni. Zaidi ya Watu 8,500 wamepoteza maisha hasa nchini sierra leone, Guinea na Liberia. Kim amesema Ebola imekuwa tishio ikizingatiwa idadi ya Watu waliopoteza maisha na kuathiri uchumi katika nchi...

Like
312
0
Wednesday, 28 January 2015
WAJUMBE NA WADAU KUTOKA MATAIFA KADHAA DUNIANI KUFANYA MKUTANO WA KIMATAIFA KUJADILI BIASHARA HARAMU YA PEMBE ZA WANYAMA
Global News

MKUTANO wa Kimataifa utakaojadili jinsi ya kukabiliana na biashara haramu ya pembe za wanyama wanaokabiliwa na tishio kubwa la kuangamia unatarajiwa kuanza leo katika mbuga ya wanyama ya Ol Pajeta iliyoko kaskazini mwa kenya. Wajumbe kutoka mataifa kadhaa duniani na wadau wote wa sekta ya utalii na wanyama pori nchini kenya wanatarajiwa kuhudhuria mkutano huo ambao utaangazia jinsi ya kuhifadhi vifaru weupe ambao kwa mujibu wa takwimu za mwaka uliopita ni chini ya vifaru elfu tano kati ya hao kuna...

Like
278
0
Tuesday, 27 January 2015
OXFAM YATAKA MATAIFA YA AFRIKA MAGHARIBI YALIYOATHIRIWA NA EBOLA YASAIDIWE KIFEDHA
Global News

SHIRIKA la misaada la Oxfam limetoa wito wa kutolewa kwa msaada wa thamani ya mamilioni ya dola kusaidia nchi za Afrika Magharibi zilizoathiriwa na Ebola, mradi huu wa msaada unaitwa Marshall Plan. Zaidi ya Watuelfu 8,500 wamepoteza maisha kutokana na ugonjwa wa Ebola, wengi wao nchini Sierra Leone,Guinea na Liberia. Mradi wa Marshall ulitumika baada ya vita ya pili ya Dunia kwa ajili ya kuwanusuru waathirika barani Ulaya. Oxfam imetoa wito kwa jamii ya kimataifa kuridhia mpango wa utoaji misaada...

Like
260
0
Tuesday, 27 January 2015
WATOTO WA HOSNI MUBARAK WAACHILIWA HURU
Global News

  WATOTO wawili wa aliyekuwa Rais wa Misri Hosni Mubarak wameachiliwa kutoka jela, miaka minne baada ya kukamatwa na kuzuiliwa kwa pamoja na baba yao. Wakuu wa gereza wanasema kuwa Gamal na Alaa Mubarak wote wafanyabiashara maarufu wameachiliwa mapema leo Jumatatu. Juma lililopita mahakama iliamuru kuachiliwa kwao huku kesi dhidi yao kuhusu ufisadi na ubadhirifu wa mali ya umma, ikiendelea....

Like
292
0
Monday, 26 January 2015
MSAFARA WA KIJESHI WASHAMBULIWA NA WATU WASIOJULIKANA MALI
Global News

RIPOTI kutoka nchini Mali zinasema kuwa watu wasiojulikana wameshambulia msafara wa kijeshi karibu na mji wa Timbuktu. Shambulizi hilo linajiri wakati ambapo kiwango cha mashambulizi kimeongezeka siku za hivi majuzi. Wiki iliyopita watu waliokuwa na silaha waliishambulia kambi moja ya umoja wa mataifa na kumuua mlinda amani mmoja kutoka Chad....

Like
291
0
Monday, 26 January 2015
OBAMA KUWEKA HISTORIA INDIA LEO
Global News

RAIS wa Marekani Barack Obama amekuwa rais wa kwanza wa Marekani kuwa mgeni rasmi katika gwaride la siku ya Jamhuri nchini inayoadhimishwa  nchini India leo siku moja baada ya kusifu enzi mpya ya urafiki kati ya nchi hizo mbili. Mwaliko huo wa kuhudhuria sherehe hizo muhimu za India za kuuonyesha ulimwengu uwezo wake wa kijeshi na tamaduni mbalimbali za India zinaonyesha ni kwa kiasi gani Rais Obama ana uhusiano wa karibu na Waziri mkuu wa India Narendra Modi. Baadaye hii...

Like
258
0
Monday, 26 January 2015
BARAZA LA USALAMA LA UN KUFANYA MIKUTANO YA DHARURA LEO
Global News

BARAZA la usalama la Umoja wa Mataifa linatarajiwa kufanya mikutano ya dharura hii leo kuijadili mizozo ya Ukraine na Yemen. Lithuania imesema iliwasilisha ombi kufanyike mkutano wa wazi kuhusu mzozo wa Ukraine. Baraza hilo la usalama limekutana takriban mara 30 kuujadili mzozo wa Ukraine tangu uanze lakini limeshindwa kuchukua hatua madhubuti kutokana na wanachama wa kudumu kama Urusi kutumia kura ya turufu kupinga maamuzi....

Like
282
0
Monday, 26 January 2015