Global News

OBAMA ALIHUTUBIA TAIFA LA MAREKANI
Global News

RAIS Barack Obama amesema  harakati za kupambana na magaidi wa dola la Kiislamu zitahitaji muda, lakini zitafanikiwa. Obama ameahidi hayo katika hotuba, juu ya hali ya nchi  inayotolewa na Rais kila mwaka nchini Marekani ambapo katika hotuba  hiyo, Rais Obama amelitaka Bunge la nchi yake lipitishe azimio la kuiruhusu Marekani itumie nguvu za kijeshi dhidi ya dola la kiislamu. Rais huyo ameeleza kuwa uongozi wa Marekani katika harakati za kupambana na dola  la kiislamu umewazuia wapiganaji  wa kundi hilo kusonga...

Like
242
0
Wednesday, 21 January 2015
WAZIRI WA USALAMA AWAOMBA RADHI WANAFUNZI KENYA
Global News

WAZIRI wa Usalama Nchini Kenya Joseph Nkaissery amewaomba radhi wanafunzi wa shule ya msingi waliofyatuliwa gesi ya kutoa machozi wakati walipokuwa wakiandamana kupinga unyakuzi wa kipande cha ardhi ambacho kilikuwa uwanja wao wa kuchezea. Bwana Nkaissery amempa Mvamizi wa ardhi hiyo siku moja kuondoa sehemu ya ukuta iliobaki baada ya wanafunzi kuuangusha na kisha kuondoka katika eneo hilo. Ameongeza kwamba serikali itaweka uzio katika ardhi hiyo na kuiacha kuwa uwanja wa kuchezea wanafunzi...

Like
412
0
Tuesday, 20 January 2015
PAPA FRANCIS AZUNGUMZIA FAMILIA
Global News

KIONGOZI wa kanisa katoliki duniani ameunga mkono haki ya wazazi kuchagua ukubwa wa familia zao. Amesema waumini wazuri wa Kanisa katoliki hawapaswi kuzaa bila ya mpangilio. Kiongozi wa Kanisa katoliki duniani amelalamikia mawazo ya nchi za magharibi kuhusu kudhibiti uzazi na haki za wapenzi wa jinsia moja kuwa yamezidi kushinikizwa katika familia za nchi zinazoendelea....

Like
232
0
Tuesday, 20 January 2015
ZAMBIA KUPIGA KURA LEO
Global News

HATIMAYE leo wananchi wa Zambia wanapiga kura kuchagua Rais wa nchi hiyo, kufuatia kifo cha Rais wa nchi hiyo Michael Sata Oktoba mwaka jana. Chama tawala cha PF kinauhakika wa kushinda katika uchaguzi huo licha ya kukabiliwa na upinzani mkali kutoka upinzani. Waangalizi wa kikanda katika uchaguzi huo, wanasema wameridhishwa na maandalizi ya zoezi zima la upigaji kura.Uchaguzi huo unatarajiwa kuwa na upinzani mkali kati ya Edgar Lungu anayegombea nafasi hiyo kupitia chama tawala na mpinzani wake HAKAINDE Hichilema kutoka...

Like
263
0
Tuesday, 20 January 2015
NGUVU YA DOLA YATUMIKA KUZUIA WAANDAMANAJI CONGO
Global News

POLISI nchini Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo wamewafyatulia risasi waandamanaji kwenye mji mkuu Kinshasa walio na hasira katika kile kinachoonekana kama jitihada za kutaka kuongoza uongozi wa rais Joseph Kabila. Watu kadha walitolewa eneo la katikati mwa mji wakiwa na majeraha ya risasi ambapo pia kulitokea makabiliano kwenye chuo kikuu cha mji huo. Milio ya risasi iliripotiwa katika maandamano mengine katika mji ulio mashariki wa Goma....

Like
285
0
Monday, 19 January 2015
MAELFU WALIOKWAMA KUTOKANA NA MAFURIKO WAOKOLEWA MALAWI
Global News

UTAWALA nchini Malawi umesema kuwa umewaokoa maelfu ya watu ambao walikuwa wamekwama kutokana na mafuriko ambayo yameikumba nchi hiyo. Wanajeshi walitumia mashua na ndege za helikopta kuwahamisha watu kwenda maeneo yaliyoinuka kufuatia kuharibiwa kwa barabara na madaraja. Takriban watu 200 wameripotiwa kufariki dunia huku wengine laki 2 wakilazimika kuhama makazi yao....

Like
228
0
Monday, 19 January 2015
KUTANA NA DARAJA LA MAJI DUNIANI
Global News

Hili ni daraja linalopatikana nchini Ujerumani Ujenzi wa daraja hili lenye maajabu yake duniani ulianza mnamo mwaka 1930 ambapo halikukamilika kufuatia vita kuu ya pili ya dunia hivyo ujenzi wake ulisimamishwa hadi mnamo mwaka 1997 mradi wa ujenzi uliendelezwa na lilifunguliwa rasmi mwaka 2003. Daraja hili limekuwa likitumika na watu kusafirishia bidhaa kwa njia ya meli za mizigo lakini pia watu hutumia kuvuka upande mmoja kwenda mwingine na zaidi limekuwa kivutio kikubwa cha utalii Daraja hili limepewa jina la Magdeburg...

Like
455
0
Monday, 19 January 2015
PAPA FRANCIS AREJEA MJINI ROME
Global News

KIONGOZI wa Kanisa Katoliki duniani Papa Francis  anarejea mjini Rome leo baada ya ziara ya wiki moja barani Asia ambako aliwavutia mamilioni ya watu na kuuwasilisha ujumbe wa kuwatetea  masikini. Baba Mtakatifu alizitembelea Sri Lanka na Ufilipino katika ziara yake ya pili katika bara hilo, mnamo muda wa miezi mitano. Hapo jana kiongozi huyo wa Kanisa Katoliki aliongoza sala iliyohudhuriwa na waumini milioni sita katika mji mkuu wa Ufilipino, Manila. Na katika ujumbe wake,Papa Francis kwa mara nyingine amewataka  watu...

Like
310
0
Monday, 19 January 2015
GODON BROWN AMEUTAKA ULIMWENGU KULAANI VITENDO VYA BOKO HARAM KUTUMIA WATOTO
Global News

MJUMBE maalum wa Umoja wa Mataifa anayehusika na Elimu GORDON BROWN, ameutaka Ulimwengu kulaani kutumiwa kwa Wasichana wadogo na kundi la waasi wa Boko Haram nchini Nigeria, kama washambuliaji wa kujitoa mhanga kwa kujilipua. BROWN ambaye ni Waziri Mkuu wa Zamani wa Uingereza, amekiita kitendo hicho kuwa  Unyama mpya, wa waasi hao. Matamshi yake yamekuja baada ya ripoti kwamba Boko Haram imewatumia wasichana watatu kufanya mashambulizi Kaskazini Mashariki mwa Nigeria mwishoni mwa Wiki...

Like
277
0
Friday, 16 January 2015
JOHN KERRY AINGIA PARIS KUJADILI MAPAMBANO DHIDI YA UGAIDI
Global News

WAZIRI wa Mambo ya Nchi za nje wa Marekani JOHN KERRY amefanya mazungumzo leo na Waziri mwenzake wa Ufaransa LAURENT FABIUS mjini Paris, kuelezea mshikamano wa nchi yake na watu wa Ufaransa, baada ya shambulio la kigaidi wiki iliopita. KERRY amemueleza FABIUS kwamba hakuweza kuhudhuria maandamano ya Mshikano Jumapili iliopita kwa sababu ya ziara iliyopangwa tangu awali nchini...

Like
258
0
Friday, 16 January 2015
KACHERO WA ISRAEL AKAMATWA NA KUNDI LA HEZBOLLAH
Global News

KIONGOZI wa kundi la wapiganaji wa Kilebanoni la Hezbollah amethibitisha taarifa zinazodai kuwepo mmoja wa viongozi wa juu ndani ya kundi hilo anatuhumiwa kutumwa na Israel kuwapepeleza. Shekh Sheikh Hassan Nasrallah amesema kiongozi huyo anayetuhumiwa tayari anashikiliwa na kundi hilo tangu abainike miezi mitano wakati akifanya kazi kwenye idara ya usalama ya kundi hilo la Hezbollah. Kauli ya Shekh Nasrallah imekuja siku chache baada ya kutolewa taarifa kupitia vyombo vya habari vya Lebanon zinazodai kuwepoa kwa ofisa wa ngazi za...

Like
263
0
Friday, 16 January 2015