BALOZI wa Marekani nchini Korea Kusini ameshambuliwa kwa kisu usoni na pia katika kifundo cha mkono wake na mshambuliaji aliyekuwa akipiga kelele kuhusiana na suala la kugawanywa kwa kipande cha ardhi ya jumuiya yao. Mara tu baada ya shambulio hilo Rais wa Marekani Barack Obama amemtakia uponaji wa haraka msaidizi wake wa zamani Mark Lippert akimuombea uponaji wa haraka baada tu ya shambulio lililofanywa wakati wa hotuba ya asubuhi. Balozi huyo mwenye umri wa miaka 42 alikimbizwa hospitalini ambako alifanyiwa...
Mwanaume mmoja mwenye umri wa miaka 44 amehukumiwa kutumikia kifungo cha miaka 75 jela nchini Kenya Hukumu hiyo imetolewa na mahakama ya watoto ya Nakuru baada ya kukutwa na hatia ya kushiriki mapenzi na mototo wake mwenye umri wa miaka 12 na kumuambukiza virusi vya...
MEYA wa mji wa Ferguson, jimboni Missouri, ametangaza hatua zitakazochukuliwa kufuatia ripoti iliyoonyesha ushahidi dhidi ya polisi wa mjini humo kujihusisha na vitendo vya ubaguzi wa rangi. Meya JAMES KNOWLES amesema mwajiriwa mmoja toka Idara ya Polisi amefukuzwa kazi na wengine wawili wamelazimishwa kwenda likizo baada ya kushutumiwa kutuma barua pepe yenye ujumbe wa kibaguzi. KNOWLES amewaambia Waandishi wa Habari kuwa Idara itaongeza namba ya Maafisa wasio wazungu na kujikita...
MVUTANO kati ya Serikali ya Kenya na vyombo vya habari kuhusu kuhamia mfumo wa Digitali kutoka Analogia ambao umesababisha Vituo vinne vikubwa vya Televisheni nchini humo kutorusha matangazo hivi sasa umeisha. Vituo hivyo mfumo wake wa Analogia ulizimwa,vitaanza kurusha matangazo yake tena. Makubaliano hayo yamefikiwa March 03 mwaka huu kati ya Serikali na Vituo hivyo vikubwa vya Televisheni nchini Kenya NTV, QTV, KTN na Citizen TV ambavyo vimekubaliwa kurusha matangazo yao jijini Nairobi chini ya Mtandao wa Africa Digital Networks...
WATU wawili raia wa Australia waliopatikana na hatia ya kusafirisha dawa za kulevywa wamehamishwa kutoka jela mjini Bali nchini Indonesia leo na kupelekwa katika kisiwa kimoja nchini humo ambako watauwawa kwa kupigwa risasi. Kwa mujibu wa ripoti za vyombo vya habari nchini Australia, hatua hiyo ya adhabu ya kifo kwa Myuran Sukumaran na Andrew Chan imeongeza wasiwasi wa kidiplomasia, huku kukiwa na maombi ya msamaha kwa watu ...
RAIS Barack Obama wa Marekani, ametupilia mbali onyo alilotoa waziri mkuu wa Israel kuhusu mpango wa Iran wa Nuclear katika hotuba yake tata kwa bunge la Marekani. Rais Obama amesema Benjamin Netanyahu alishindwa kutoa suluhisho mbadala kuhusu suala kuu la jinsi ya kuizuia Teheran kutengeza silaha za Nuclear. Waziri Mkuu Netanyahu ambaye alialikwa kuhutubia bunge na viongozi wa chama cha Republican alishutumu mkataba uliowekwa kati ya mataifa ya magharibi na Iran na kudai kuwa ni hatari . ...
VIONGOZI wa nchi za Magharibi wamekubaliana kwamba hatua kali kutoka kwa Jumuiya ya Kimataifa zitahitajika iwapo kutatokea ukiukaji wa utekelezaji wa Mkataba wa kusitisha mapigano nchini Ukraine. Mkataba huo umesainiwa Mjini Minsk nchini Belarus Febrauari 12 mwaka huu kati ya majeshi ya Serikali ya Ukraine na Waasi wanaoiunga mkono Urusi. Rais wa Marekani BARACK OBAMA, mwenzake wa Ufaransa FRANCOIS HOLLANDE, Kansela wa Ujerumani ANGELA MERKEL, Waziri Mkuu wa Uingereza DAVID CAMERON na Waziri Mkuu wa Italia MATTEO RENZI wameshiriki katika...
WAZIRI Mkuu wa Israel BENJAMIN NETANYAHU amelionya Bunge la Marekani kwamba mkataba na Iran uliopendekezwa hautazuia wala kupunguza uwezo wake wa kutengeneza mabomu ya nyuklia. Akilihutubia bunge hilo Bwana NETANYAHU amezikosoa juhudi za Rais wa Marekani BARACK OBAMA kutafuta makubaliano na Iran kuhusu mpango wake wa nyuklia wenye utata. Bwana NETANYAHU ameonya kwamba utawala wa Bwana OBAMA unaifungulia mlango Iran kuelekea kutengeneza bomu la nyuklia. ...
KANSELA wa Ujerumani ANGELA MERKEL ameeleza kuunga kwake mkono mpango mpya wa uwekezaji katika Bara la Ulaya. Mpango huo wa Uwekezaji umependekezwa mwaka jana na Rais wa Halmashauri ya Umoja wa Ulaya JEAN-CLAUDE JUNCKER ambapo ni mpango wa Euro Bilioni 300 wa kuifanya bora miundo Mbinu katika mataifa ya Ulaya. MERKEL ameeleza uungaji wake mkono katika mpango huo , lakini amesema mageuzi zaidi na makubaliano ya Biashara huru na...
WAZIRI wa Mambo ya Kigeni wa Ukraine PAVLO KLIMKIN ameonesha wasiwasi wake kuhusiana na matarajio kwamba makubaliano yanayoungwa mkono na Umoja wa Mataifa ya kusitisha mapigano na waasi wanaoiunga mkono Urusi yataendelea, wakati akitoa wito wa kuongezeka kwa kikosi cha Kimataifa cha kuangalia makubaliano hayo. Bwana KLIMKIN amewaambia Waandishi Habari mjini Tokyo kwamba hali katika eneo la mapigano ni mbaya na ya wasi wasi licha ya...
IRAQ imeanzisha operesheni kubwa ya kuukomboa mji wa Tikrit unaodhibitiwa na kundi la Dola la Kiislamu. Wanajeshi Elfu-30 wa Iraq na wapiganaji wakisadiwa na ndege za kivita wamezishambulia ngome za wapiganaji wa jihadi wa kundi hilo ndani ya mji huo na maeneo yanaozunguka, katika harakati inayoelezwa kuwa kubwa kabisa kuwahi kufanywa kuyakomboa maeneo yanayodhibitiwa na Dola la Kiislamu. Vikosi vya Serikali ya Iraq vimekuwa vikisonga mbele kuelekea maeneo ya Kaskazini huku vikipata ushindi dhidi ya kundi hilo lakini mji wa...