TENNIS Bingwa namba moja katika mchezo wa Tennis, Novak Djokovic ameanza vizuri michuano ya ATP World Tour kwa kumchakaza bingwa wa michuano ya wazi ya Marekani (US OPEN), Marin Cilic kwa seti 6-1 6-1 huko O2 Arena jijini London. Djokovic anayesaka taji la tatu mfululizo katika michuano hiyo ikiwa ni rekodi iliyowekwa mara ya mwisho na aliyekuwa kocha wa Andy Murray, Ivan Lendl ilimchukua Mserbia huyo dakika 56 tu kuweza kumpoteza mpinzani wake raia wa Croatia. Katika mchezo mwengine wa...
Wachezaji watano watajwa kuweza kuwania tuzo ya mchezaji bora wa bara la Afrika inayotolewa na Shirika la utangazaji habari nchini Uingereza (BBC). Wachezaji waliopata nafasi ya kuingia katika kiny’ang’anyiro hicho ni Yaya Toure (Ivory Coast, Man City), Yacine Brahimi (Algeria, Porto), Vicent Enyeama (Nigeria, Lille), Gervinho (Ivory Coast, Roma) na Pierre Emerick Aubameyang (Gabon, Borussia Dortmund). Tuzo hiyo inayoshikiliwa na mchezaji wa timu ya Taifa ya Ivory Coast na klabu ya Man City, Yaya Toure inatoa nafasi kwa mashabiki wa...
Kiungo wa kimataifa wa Brazil Oscar Dos Santos Emboaba Jr. asaini mkataba wa miaka mitano ndani ya klabu ya Chelsea utakaomfunga ndani ya Stamford Bridge mpaka mwaka 2019. Oscar alijiunga na Chelsea msimu wa mwaka 2012 akitokea klabu ya Internacional kwa dau lililoripotiwa kuwa ni kiasi cha paundi million 20 chini ya utawala wa kocha Di Matteo. Chelsea inayonolewa na kocha Jose Mourinho imekuwa katika kiwango kizuri sana msimu ikiwa inaongoza ligi kuu nchini England bila ya kupoteza mchezo wowote...
Aliyekuwa kocha wa kikosi cha Manchester United, David Moyes ameteuliwa kuwa Meneja mpya wa klabu ya Real Sociedad inayokipiga ndani ya ligi kuu nchini Hispania (LA LIGA). Moyes amesaini mkataba wa miezi kumi na nane akichukua nafasi ya kocha aliyefungashiwa virago Jacob Arraste ikiwa ni miezi nane tu toka alipotimuliwa ndani ya Manchester United. Klabu ya Real Sociedad inashika nafasi ya kumi na tano katika msimamo wa La Liga ikiwa imejikusanyia jumla ya alama tisa tu sawa na vilabu vinne...
TENNIS Pazia la michuano ya ATP World Tour limefunguliwa rasmi hapo jana usiku katika viwanja vya O2 huko jijini London nchini England. Andy Murray anayetokea katika visiwa hivyo vya Uingereza amejikutan akipokea kichapo kikali cha seti 6-4 6-4 kutoka kwa MJapan Kei Nishikori ambaye ni mara yake ya kwanza kushiriki katika michuano hiyo ya kufunga mashindano ya mwaka. Kichapo hicho kinamuweka Murray katika wakati mgumu sana ndani ya kundi B linalojumuisha mchezaji bingwa namba mbili duniani, Roger Federer anayeshikilia rekodi...
FORMULA 1 – LANGALANGA Dereva wa timu ya Mercedes Nico Rosberg apunguza tofauti ya alama katika msimamo wa mashindano ya langalanga (Formula 1) baada ya kuibuka kidedea kwenye mashinadno ya huko nchini Brazil (Brazilian Grand Prix). Raia huyo wa nchini Ujerumani mwenye upinzani mkubwa na dereva mwenzake Lewis Hamilton ilimchukua saa moja dakika thelathini na sekunde mbili ikiwa ni ushindi wake wa tano msimu huu. Hamilton anaongoza msimamo wa mashindano hayo akiwa na jumla ya alama 334 dhidi ya Rosber...
Wachezaji wa Tennis Nchini watakutana mjini Arusha siku ya Jumamosi tayari kwaajili yamichuano ya kupandisha viwango vyao ilikujiwekatayari kwa mashindanombalimbali ya kimataifa Kocha wa mchezo huo Kiango Kipingu ameiambia E.sport kuwa wachezaji hao wanaianza safari yao leo kuelekea Arusha huku chama cha Tennis taifa kikiwakimegharamia safari hiyo...
Wanachama Yanga waibuka na kukosoa mfumo wakocha Mbrazil Maxio Maxmokuendelea kuwatumia wachezaji wa kigeni – Jaja na Countinhokatika kila mechi hatakamawachezaji haowanaonekana hawapo vizuri kimchezo Akizungumza na E.sport mwanachama aliyewahi kuwania nafasi ya Mwenyekiti klabu hiyo ya Jangwani John Jambele amesema mfumo huo wa kocha maximo pamoja nakuchelewa kufanyamaamuzi kubadilisha wachezaji kutokana na ugumu wamechi husika umechangia kupoteza mechi zao mbili tangu ilipoanzakutimuaVumbi Msemaji wa Yanga Baraka Kizuguto ameipinga kauli...
Kamati ya utendaji ya Klabu ya Simba imekutana jana kuzungumzia suala la Wachezaji watatu waliowasimamishwa kutokana naUtovu wa nidhamu, Lakini kikao hicho kimeshindwa kutoamajibu kuhusu hatima ya wachezaji hao Wachezaji hao ni pamoja na Shabani Kisiga, Haroun Chanongona, Amry Kiemba ambao wamesimamishwa mara baada ya mchezo wa kati ya Simba dhidi ya Tanzania prison uliopigwa katika dimba la Sokoine huko mkoani mbeya na timu hizo kwenda sare ya kufunganabao 1-1 Msemaji wa Simba Hamphrey Nyasio, Amezungumza na E.sport na kuthibitisha...
CECAFA yakuna kichwa kumpata mwenyeji wa mashindano ya Challenge mwaka huu ni baada ya Ethopia kujitoa dakika ya mwisho Afisa habari wa CECAFA Rodgers Mulindwaalipozungumza n E.sport kutoka mjini Kampala nchini Uganda amesema baraza hilo kwa sasa lipo katika mazungumzo mazito na nchi YaSudani kuona uwezekano wakubeba jukumu hilo la uenyeji wa challenge...
Dereva wa kimataifa kutoka nchini Brazil, Felipe Nasr ameteuliwa kuitumikia timu ya Sauber yenye maskani yake huko nchini Uswisi katika michuano ya langalanga msimu wa 2015. Felipe aliyekuwa ni dereva wa akiba wa timu ya Williams atajiunga na timu inayoshika nafasi ya 10 katika msimamo wa ligi huku wakishindwa kukusanya alama yoyote. Uteuzi huo unamaanisha kuwa madereva wawili wa sasa Adrian Sutil na Esteban Gutierez watakuwa huru kujiunga na timu nyengine ndani ya klabu hiyo ifikapo mwishoni mwa msimu huu....