Sports

DONDOO ZA MCHEZO WA CRICKET
Slider

Mchezaji wa zamani wa timu ya taifa ya Australia Matthew Hayden ameshangazwa na maamuzi ya timu ya taifa ya England ya kumuacha nahodha wa zamani wa timu hiyo, Kevin Pietersen. Matthew amesema kitendo cha England kumuacha mmoja kati ya wachezaji hodari kabisa kuwahi kutokea katika ardhi ya nchi ya England kinaonyesha wazi hawapo teyari kwenda kushindana na timu kama India na Australia. England wametangaza majina ya wachezaji 15 watakaoshiriki michuano ya kombe la dunia huku ikimteua Eoin Morgan kuwa nahodha...

Like
363
0
Monday, 22 December 2014
ERIC ABIDAL ATANGAZA KUSTAAFU SOKA
Slider

Beki wa Kimataifa wa Ufaransa na klabu ya Olympiacos, Eric Abidal ametangaza kustaafu kucheza soka ikiwa ni takribani miaka kumi na nne toka aanze kucheza soka la kulipwa. Abidal alijiunga na klabu ya Olympiacos msimu huu na kusaini mkataba wa miaka miwili uliokuwa uishe msimu wa 205/2016 lakini ameamua kuuvunja kwasababu za kiafya. Beki huyo wa kushoto amekuwa akisumbuliwa na ugonjwa wa kansa toka mwaka 2011 na kumfanya akose michezo mingi akiwa na klabu ya FC Barcelona walioamua kumpa heshima...

Like
214
0
Friday, 19 December 2014
FA YAMUADHIBU BALLOTELI KUFUATIA VITENDO VYA UBAGUZI WA RANGI
Slider

Chama cha soka cha nchini England (FA) kimemuadhibu mshambuliaji wa klabu ya Liverpool, Mario Balloteli kwa kumfungia kutocheza mchezo mmoja wa ligi kuu nchini England na kumtaka alipe fidia ya kiasi cha paundi ishirini na tano elfu baada ya mchezaji huyo kukutwa na hatia ya vitendo vya ubaguzi. Hatua hiyo imefikiwa na chama hicho baada ya Muitaliano huyo kutuma ujumbe ulionyesha vitendo vya kibaguzi katika mtandao wa kijamii wa twitter kwa kuandika “ruka juu kama mtu mweusi ila tafuta fedha...

Like
251
0
Friday, 19 December 2014
AZAM YASHINDWA KUTAMBA KWA URA
Slider

Mabingwa wa Tanzania Bara, Azam FC jana usiku walipokea kichapo cha pili mfululizo katika ziara yao ya huko nchini Uganda. Wanalambalamba hao imechapwa goli 1-0 dhidi ya URA katika mchezo uliochezwa jijini Kampal, Uganda. Kikosi hicho ambacho kipo chini ya kocha Mcameroon Joseph Marius Omog na Mganda, George “Best” Nsimbe imeweka kambi Uganda kujiandaa na Ligi kuu ya Vodacom Tanzania Bara iliyosimama kwa mwezi mmoja, ambayo itarejea wiki ijayo. Katika dirisha dogo la usajili Azam FC imewasajili beki Serge Wawa...

Like
273
0
Thursday, 18 December 2014
RAHEEM STERLING AIPELEKA LIVERPOOL NUSU FAINALI CAPITAL ONE CUP
Slider

Kiungo wa kimataifa wa England Raheem Sterling aipeleka klabu ya Liverpool katika hatua ya nusu fainali ya kombe la ligi (Capital One Cup) baada ya kufunga magoli mawili katika mchezo dhidi ya klabu ya Bournemouth. Liverpool iliingia katika mchezo huo wa robo fainali ikiwa na jeraha la kuchapwa magoli matatu kwa sifuri dhidi ya mahasimu wao Manchester Unired, ilipata goli la kwanza mnamo dakika ya 20 kupitia kwa Sterling kabla ya Lazar Markovic kuongeza goli la pili mnamo dakika ya...

Like
283
0
Thursday, 18 December 2014
FORMULA 1 – LANGALANGA LEWIS AHAIDI MAKUBWA BAADA YA USHINDI
Slider

  Dereva wa magari ya Mercedes, Lewis Hamilton ameahidi kufanya makubwa zaidi katika mashindano mashindano ya Formula 1 baaada ya kufanikiwa kubeba taji la mwaka huu. Hamilton amefanikiwa kubeba taji kwa tofauti ya alama sitini na saba dhidi ya mpinzani wake wa karibu, Nico Rosberg likiwa ni taji lake la pili baada ya lile la kwanza kulitwaa mwaka 2008 akiwa na timu ya McLaren. Akiwa ni mmoja kati ya madereva saba kuwahi kutwaa taji hilo mara mbili katika historia ya...

Like
229
0
Monday, 24 November 2014
HATMA YA MAKUNDI KUFAHAMIKA COPA AMERIKA
Slider

Mataifa mbalimbali kutoka barani Amerika ya Kusini yatajua hatma yao katika upangwaji wa makundi ya michuano ya Copa Amerika inayotarajiwa kufanyika mwaka 2015 huko nchini Chile. Katika jiji la Vina Del Mar mataifa kumi na mbili yatagawanywa katika makundi matatu yatakayojumuisha timu nne kila kundi kwenye hatua ya kwanza. Chile ambaye ndio mwenyeji wa michuano hiyo amewekwa katika kapu namba moja pamoja na timu ya Brazil na Argentina huku Uruguay ambaye ni bingwa mtetezi wa michuano hiyo amewekwa katika kapu...

Like
291
0
Monday, 24 November 2014
CASILLAS AWANIA TUZO YA GOLIKIPA BORA 2014
Slider

Iker Casillas ateuliwa kuwania tuzo ya golikipa bora katika kikosi cha shirikisho la soka duniani (FIFA) cha mwaka 2014. Casillas ambaye ni golikipa wa klabu ya Real Madrid na timu ya taifa ya Hispania amejumuishwa katika kiny’ang’anyiro hicho pamoja na Manuel Neuer (Bayern Munich, Germany), Gigi Buffon (Juventus, Italy), Thibaut Courtois (Chelsea, Ubelgiji) na Claudio Bravo (FC Barcelona, Chile). Kujumuishwa kwa nahodha huyo wa Hispania kumewashangaza watu wengi kwani Casilllas alicheza mechi mbili tu katika msimu wa 2013/2014 ndani ya...

Like
329
0
Monday, 24 November 2014
BARTOMEU AMMWAGIA SIFA MESSI
Slider

Rais wa klabu ya FC Barcelona amemmwagia sifa nahodha wa timu ya taifa ya Argentina na mshambuliaji wa klabu hiyo, Lionel Messi kuwa ndio mchezaji bora kabisa kuwahi kutokea. Josep Maria Bartomeu ambaye ni rais wa klabu ya Barcelona inayonolewa na kocha Luis Enrique amezungumza hayo baada ya kushuhudia Messi akivunja rekodi ya magoli ndani ya La Liga iliyokuwa ikishikiliwa na marehemu Telmo Zarra. Messi mwenye umri wa miaka ishirini na saba amefikisha jumla ya magoli mia mbili na hamsini...

Like
202
0
Monday, 24 November 2014
DJOKOVIC AVUNJA REKODI YA IVAN LENDL
Slider

Bingwa namba moja katika mchezo wa Tennis, Novak atawazwa kuwa mshindi wa michuano ya ATP World Tour Finals huko jijini London baada ya Roger Federer kushindwa kucheza mchezo wa fainali kutokana na maumivu ya mgongo. Federer aliyeshinda kwa seti 4-6 7-5 7-6(8-6) ndani masaa mawili na dakika arobaini na nane siku ya jumamosi dhidi ya Wawrinka ameomba radhi kutokana na kitendo hicho. Huu ni ubingwa wan ne kwa MSerbia Djokovic ikiwa ni mara yake ya tatu mfululizo kutwaa taji hilo...

Like
301
0
Monday, 17 November 2014
VAN GHAL KUMKOSA KIUNGO BLIND MECHI ZIJAZO
Slider

Kiungo wa timu ya taifa ya Uholanzi na klabu ya Manchester United, Daley Blind anaweza kukaa nje ya uwanja kwa muda wa wiki sita baada ya kupata jeraha la goti katika mchezo wa kuwania kuingia michuano ya Ulaya mwaka 2016 huko nchini Ufaransa. Katika mchezo huo ambao timu ya Taifa ya Uholanzi iliibuka na ushindi mnono wa magoli 6-0 dhidi ya Latvia, Blind aliumia mnamo dakika ya 20 ya mchezo kwa kugongana na mchezaji Eduards Visnakovs. Kuumia kwa kiungo huyo...

Like
231
0
Monday, 17 November 2014