Slider

BARCELONA YAAGA MICHUANO YA UEFA
Slider

Klabu ya soka ya Barcelona Jumatano ilivuliwa taji la Ligi ya Mabingwa Ulaya baada ya kuchapwa mabao 2-0 na Atletico Madrid huku Mabao yote ya Altletico Madrid yakifungwa na Antoine Griez-mann na bao la pili likifungwa kwa mara nyingine na Antoine kwa njia ya penalti . Kwa matokeo hayo Atletico Madrid wanasonga mbele kwa ushindi wa jumla ya mabao 3 -2 baada ya awali kufungwa 2-1 na Barcelona katika Uwanja wa Camp Nou. Katika mchezo mwingine Bayern Munich imefakiwa kutinga...

Like
340
0
Thursday, 14 April 2016
VIDEO YA BOKO HARAM YAONESHA WASICHANA NA CHIBOK
Global News

KANDA ya video iliyotumwa kwa maafisa wa serikali ya Nigeria kutoka kwa kundi la wapiganaji wa Boko Haram imewaonesha baadhi ya wasichana waliotekwa eneo la Chibok wakiwa hai. Taarifa zaidi zinaeleza kwamba ni kipindi cha miaka miwili sasa tangu kutekwa kwa wasichana 276 kutoka shule moja katika mji wa Chibok nchini humo. Hata hivyo ni wasichana 15 tu, wanaoonekana kwenye kanda hiyo ya video ambayo inaaminika ilipigwa Siku ya sikukuu ya Krismasi mwaka...

Like
271
0
Thursday, 14 April 2016
UHUSIANO WA ZIKA NA VICHWA VIDOGO WATHIBITISHWA
Global News

KITUO cha Taifa cha Kudhibiti Magonjwa nchini Marekani (CDC) kimethibitisha kwamba virusi vya Zika husababisha watoto kuzaliwa na vichwa vidogo na ubongo kudumaa. Hayo yamejiri kufuatia kuwepo kwa mjadala mkubwa na sintofahamu kuhusu uhusiano kati ya virusi hivyo na watoto kuzaliwa na vichwa vidogo tangu kuongezeka kwa visa vya watoto kuzaliwa na vichwa vidogo Brazil. Mkurugenzi mkuu wa CDC Tom Frieden amesema hakuna shaka kwamba virusi vya Zika vinasababisha watoto kuzalwia na vichwa vidogo, tatizo ambalo kwa Kiingereza hujulikana kama...

Like
261
0
Thursday, 14 April 2016
KUBENEA AHUKUMIWA KIFUNGO CHA NJE MIEZI MITATU KWA KUMTUSI PAUL MAKONDA
Local News

MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Kisutu imemuhukumu mbunge wa Jimbo la Ubungo kupitia chama cha (CHADEMA) Saeed Kubenea kifungo cha nje cha miezi mitatu kutokana na kosa la kutumia lugha ya matusi dhidi ya aliyekuwa Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Mheshimiwa Paul Makonda ambaye kwa sasa ni Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam.   Akisoma hukumu hiyo jana Jijini Dar es Salaam Hakimu Mkazi wa Mahakama ya Kisutu Thomas Simba amesema kuwa mahakama imeamua kumpa mshitakiwa adhabu ya kifungo hicho kwa kuwa ndilo kosa lake la...

Like
362
0
Thursday, 14 April 2016
UFUATILIAJI WA AGENDA 2030 UNAHITAJI TAKWIMU SAHIHI
Local News

SERIKALI imesema kuwa takwimu sahihi zinahitajika katika kufuatilia utekelezaji wa malengo ya maendeleo Endelevu. Hayo yameelezwa na mwakilishi wa kudumu wa Tanzania katika umoja wa Mataifa Balozi Tuvako Manongi wakati wa mkutano wa 49 wa kamisheni ya Umoja wa Mataifa kuhusu idadi ya watu na maendeleo. Balozi Manongi...

Like
247
0
Thursday, 14 April 2016
UMOJA WA ULAYA WALAANI HATUA YA RAIS WA MACEDONIA KUWASAMEHE WANASIASA WALIOHUSISHWA NA UFISADI
Global News

MUUNGANO wa ulaya umelaani hatua ya rais wa Macedonia, Gjorge Ivanov, kuwasamehe wanasiasa waliohusishwa na ufisadi. Kamishna anayehusika na upanuzi wa muungano huo Johannes Hahn, amesema kuwa msamaha huo hauambatani na uelewa wake wa sheria na hivyo, unahatarisha lengo la Macedonia kuwa mwanachama wa muungano huo. Taifa hilo limekumbwa na mzozo unaohusiana na madai kwamba chama tawala na wakuu wa idara ya ujasusi , walidukua simu za zaidi ya watu alfu ishirini wakiwemo waandishi wa habari na maafisa wa idara...

Like
209
0
Wednesday, 13 April 2016
MACHAR AREJEA SUDAN KUSINI
Local News

KIONGOZI wa waasi nchini Sudan Kusini, Riek Machar, amerejea nchini humo kwa mara ya kwanza katika kipindi cha zaidi ya miaka miwili kama sehemu ya utekelezwaji wa mkataba wa amani. Atakapowasili mjini Juba, Bwana Machar anatarajiwa kuchukua wadhfa wake wa makamu wa rais. Msemaji wake amethibitisha kwamba bwana Machar alikuwa katika makao makuu ya waasi yaliyo katika mji wa Pagak mpakani na taifa jirani la...

Like
266
0
Wednesday, 13 April 2016
ASKOFU MATHIAS JOSEPH AFARIKI DUNIA
Local News

  ASKOFU msitaafu wa Jimbo Katoliki la Dodoma, Mhashamu Askofu Mathias Joseph Issuja, amefariki dunia.   Askofu isuja ambaye alizaliwa mwaka 1929 alipata daraja hilo Takatifu mwaka 1972 ambapo aliwekwa wakfu na Hayati Kardinali Laurean Rugambwa na kustaafu mwaka 2005 akiwa Askofu wa Jimbo la Dodoma.   Efm imezungumza kwa njia ya simu na Katibu mkuu wa Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania-TEC, Padri Raymond saba ambaye amesema kuwa Askofu mstaafu Issuja, amefariki usiku wa kuamkia leo huko katika Hospitali ya...

Like
463
0
Wednesday, 13 April 2016
KESI YA HANI YAANZA AFRIKA KUSINI
Global News

KESI ya serikali ya Afrika Kusini inayopinga kuachiliwa awali kwa muuaji wa shujaa aliyepinga ubaguzi wa rangi Chris Hani imeanza kusikilizwa katika mahakama kuu mjini Pretoria nchini Afrika kusini. Waziri wa sheria Michael Misutha anaamini kuwa mahakama ilifanya makosa wakati ilipotoa uamuzi kuwa raia wa Poland Janusz Walus aachiliwe huru. Kuachiliwa kwake kulizua ghadhabu sehemu nyingi nchini Afrika Kusini huku Mkewe Hani akiutaja uamuzi huo kuwa ni huzuni kubwa kwa Afrika Kusini.....

Like
248
0
Tuesday, 12 April 2016
WAZIRI WA MAMBO YA NJE WA ITALY AWASILI LIBYA
Global News

WAZIRI wa mambo ya nje wa Italia amewasili mjini Tripoli Libya, kwa mazungumzo na kiongozi wa serikali mpya ya umoja wa kitaifa nchini Libya Fayez Seraj. Paolo Gentiloni ni afisa mkuu wa kwanza wa bara la Ulaya kufanya ziara rasmi nchini Libya tangu utawala mpya unaoungwa mkono na Umoja wa mataifa kuwekwa katika mji mkuu wa Libya majuma mawili yaliyopita. Italia pamoja na mataifa kadhaa ya dola za kimagharibi yaliyoitawala Libya miaka iliyopita yameahidi kuisaidia serikali hiyo mpya kwa imani...

Like
368
0
Tuesday, 12 April 2016
JANUARY MAKAMBA AKUTANA NA UJUMBE WA KAMATI YA FEDHA YA BUNGE LA FINLAND
Local News

WAZIRI wa Nchi ofisi ya makamu wa Rais, Muungano na Mazingira Mheshimiwa January Makamba amekutana na kufanya mazungumzo na ujumbe wa kamati ya fedha ya Bunge la Finland.   Katika mazungumzo yao yaliyofanyika leo Jijini Dar es salaam, wabunge hao wameipongeza serikali ya Tanzania kwa jitihada inazozifanya za kulinda na kuhifadhi mazingira.   Awali akiwakaribisha wabunge hao, Waziri Makamba amesema Tanzania inajivunia uhusiano bora uliopo baina yake na Finland na kuwashukuru wabunge hao kwa kufanya ziara yao...

Like
327
0
Tuesday, 12 April 2016